Thread ya Show ya "I am Zuchu": Kutoa Tsh. million 5 kumuona Zuchu kwenye VVIP inaitaji uwe na utajiri wa Bakhresa

Thread ya Show ya "I am Zuchu": Kutoa Tsh. million 5 kumuona Zuchu kwenye VVIP inaitaji uwe na utajiri wa Bakhresa

Kwanza niwape pongezi Sana Wasafi namna walivyopamba ukumbi ulikuwa very nice na pia setting up ya jukwaa ilikuwa zuri Sana ikiwemo graphics zilizotumika on scene wakati msanii anaperfomance ilikuwa Ni fire Sana.WCB wanajua how to brand msanii na hii ndio tofauti yao na wasanii wengine I believe after hiyo show itapandisha value ya Zuchu Mara dufu.

Perfomance

Performance ya mboso dah was amazing kwa kweli amefanya wonders performance na ana deserve zile hela nyingi alizotuzwa.I think mbosso ndio msanii aliyetunzwa hela nyingi Sana.

Combination performance ya mboso & Zuchu

Moja Kati ya performance iliyonikosha kweli kweli nilipenda chemistry walionayo.

Combination ya Zuchu & Jide commando

Kumekuwa namsemo kwamba wanawake wanachukiana Sana lakini ushirikiano wa Jide na zuchu unaweza kutengeneza kitu kwenye Huu mziki.Walifanya something special as if Kama walikuwa na ngoma ya pamoja hapo kabla.Honestly nimependa Sana performance yao ya pamoja kiasi ambacho mashabiki wakataka warudie kuperform Mara 3.

Performance ya Zuchu

Kwanza kabisa ana confidence yake kaperform as if ana muda mrefu kwenye game I did like dress code yake ila nimependa zaidi performance ya wimbo wake wa "Nisamehe" nimependa alivyo calm na hisia kubwa aliyotumia Kama wimbo ulivyo, ukichanganya na voice yake ilivyo mzuri you get something good.Pia ametuonesha uwezo wake pia wa kudance huku aliimba kwa baadhi ya wimbo zake was amazing.

Combination ya mama yake na Zuchu

Waliua Sana aisee mama na mtoto.

performance ya Lavalava

Katika show zake zote za Lavalava hii ndio best show kuliko zote nilizowahi kuona kutoka kwake mzee aliua.


Ushauri wangu kwa baadhi ya udhaifu

Kuna watu wengi walibaki nje ambao walikosa tickets Wasafi wangejitahidi kuweka scene kubwa nje ya Ukumbi walau waone Nini kinajili ndani kuliko walivyowaacha.

La pili hili Ni moja Kati ya tatizo kubwa la watanzania wengi na nilichoona Jana watu kutokuja kwenye tukio kwenye muda uliopangwa watu hawapendi kuzingatia muda wasafi walipanga tukio nzima lianze saa 1 usiku Cha ajabu hata Diamond mwenyewe na Zuchu walikuja saa 2 usiku badala ya saa 1 usiku.
 
Chuchu hamna kitu. Ni lebel tu ndo inambeba. Now nimeelewa why alikaa miaka minne bila kusaigniwa. Hana kipaji,sauti mbaya,kutawala jukwaa hajui.
Diamond hivi kweli si bora ungemsign Ruby. Ruby ni moto kabarikiwa yule binti. Ni vile hana promo tu .Angekuwa Mwislam im sure angesainiwa pale wasafi.
 
Zuchu hana excuse kwa show mbovu ya jana. Amezaliwa na kulelewa na nguli wa performance Khadija Kopa, hata hajifunzi kwa mama yake? Miaka yote minne aliyosema alikuwa kwenye mafunzo huko usafini ndio utopolo gani ule?

Ieleweke nampenda sana mama yake, nimejikuta nampa sapoti sababu ya mama yake ila kaniangusha sana. Anapayuka kama yuko kilabuni ati anaperfom live na bendi!

Tazama mama yake aliposhika Mic, sawa uzoefu unachangia ila roho yangu ilisuuzika, she is the best. Ndiye pekee aliyeuchezesha ukumbi mzima bila kumsahau Jide huyu ni kiboko inafahamika, Mbosso na Dullah Makabila alinishangaza, anajua sana.
 
Kweli kabisa ni shoo ya kwanza kabisa Africa kwa Meneja wa msanii kupanda jukwaani akaita wasanii wake(Diamond,Ray Van) waje kuimba kumbe wameshakimbia ukumbini then Meneja mwenyewe akiwa amelewa akaamua nyimbo za wasanii wake zipigwe huku akiimba mwenyewe.

Very very ‘professional’.
safi sana mkuu naona hukuona chochote kizuri kwenye show upongeze bali we unaonaga negative tu. Hongera sana mkuu.
 
Back
Top Bottom