eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,214
- 15,853
Umenena ukweli, tatizo tayari tushaonekana ni shimo la takataka, kuanzia chemicals zao, vifaa vya tech, entertainents, nguo, viatu, chupi, brassieres, na hata vyakula vilivyo expire...
Nimependa pale ulipomuingiza Mchina, huyu bwana anawapagawisha sana Ulaya na Marekani, wanamuogopa kufa, Mchina anasambaza huduma zake kila sehemu hasa Dunia ya 3, tena kwa bei nzuri, kwa ubora..Kifupi kwa sasa narudia maneno ya JPM, kuna vita ya uchumi kali mno, Mchina, Ulaya na Marekani wote wanaigombania Dunia ya 3, wote wanataka kuendeleza nguvu zao kiuchumi na kimali, lazima nasi tujiulize tunataka nini kwao, lazima tuwe na msimamo na siyo kuwa kama kigori anayegombaniwa ni nani atamtoa bikira na kumfaidi..
Tusipojitambuwa tumwekwisha, tena na tena, lazima nasi kabla ya kuwapa mwili wetu lazima tuwape masharti, je wakubwa zetu wanalielewa hili?!
umenena vyema. China, Ulaya na marekani wana sera kuielekea au kushirikiana na Afrika. lkn swali ni je Afrika ina sera au mikakati ya makusudi ya pamoja kuelekea washirika hawa?? kama hamna inabidi kitu kifanyike. hatuwezi tukawa watu wa kupokea maagizo ya nini cha kufanya siku zote. lazima tuwe na dira na muelekeo, yeyote anayekuja kwetu lazima ajue sisi sera na muelekeo wetu ni nini!! siyo kuja kutuagiza.