Thumbs-Up kwa Designer nguo za Rais Samia Suluhu Hassan

Anaeweza kubadiki hata mara 10 yeye hanunui nguo ila serkali ndiyo inayo mnunulia
 
Acheni mchezo bana.

Mama yetu ni mtu smart sana anajua kupangilia nguo sio mchezo.

Wanawake muige mfano wake sio wengine nguo mnavaa hadi siku kumi, wengine nguo ya sendoff ndio hiyohiyo hadi harusi hapana lazima mjifunze kwa Mama yetu..

Mama anapiga vitu vya kueleweka na wanaomshonea wanampatia acha kabisa, ile ndio haiba ya uongozi sasa.

Yaani mama akisalimia kidogo tu kama kuna kipengele cha maji ya kunywa kabla ya kunywa maji lazima abadilishe nguo.

Mama Uganda alienda kapiga kitu kingine haaa wakati wa kurudi ashabadilisha kabisa haya ndio maneno sasa. Mama kwa miaka minne atabadilisha nguo pea 2920.
 
Tuwe fair. Hivi kweli SSH mnamuita mama yenu kwa kumpenda au kujipendekeza? Mbona hatukusikia marais waliopita mkiwaita baba zenu? Je akiondoka kwenye ulaji mtaendelea kumuita mama yenu? Janet aliitwa mama kipenzi leo mnamuita mjane wa Jiwe. Kujipendekeza kitu mbaya sana.
 

Kwani unaona Bongo movie wanamuita tena Makonda Kaka yetu? Kwani mbona Magufuli tulimuita Jemedari wetu au haukumbuki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…