Habari za wakati huu ndugu zangu wa JamiiForums,
Ninaandika ombi hili hapa nikiwa na simanzi kubwa kutokana na hali ngumu anayopitia mama yangu mzazi.
Mama anasumbuliwa na makovu makubwa katika maeneo ya shingo, mgongoni na kifua (kama inavyoonekana kwenye picha), ambayo yanamletea maumivu makali sana.
Hali yake kwa sasa ni mbaya kiasi cha kumfanya ashindwe kulala usiku wala kuwa na amani mchana. Mara kwa mara huwa analia kutokana na miwasho mikubwa, maumivu, na wakati mwingine anasema makovu hayo yanawaka moto kwa ndani. Tumejaribu kutumia dawa mbalimbali tulizoelekezwa na madaktari lakini hakuna nafuu iliyopatikana, na hata dawa za maumivu zimekuwa hazisaidii tena.
Sababu ya kupatikana kwake, ni ajali aliyoipata kipindi Cha usichana wake na kumuachia majereha makubwa ambayo baada ya kupona yakamuachia makovu makubwa yaliyovimba.
Mama anateseka sana na tunatamani kuona anapata nafuu. Kupitia jukwaa hili lenye watu wa kada mbalimbali naomba ushauri na pia kufaham mambo yafuatayo:
1. Je, kuna mtu aliyewahi kukutana na hali ya namna hii na akafanikiwa kupata suluhu au tiba?
2. Ni hospitali gani hapa Tanzania au madaktari bingwa ambao wanaweza kushughulikia tatizo la aina hii kwa ufanisi?
3. Je, kuna njia za kitaalam (kama vile sindano au upasuaji maalum) zinazoweza kupunguza au kuondoa mateso haya?
Tunaomba msaada wa ushauri, maelekezo, au mawasiliano ya vituo vya afya vinaweza kusaidia. Ntanguliza shukrani.