Tiba mbadala na vipimo vya kitapeli

Nadhani serikali ishugulike na kudhibiti gharama tu ikiwezekana iingie hata kwenye bima ili huduma hii iwe nafuu kwa watu,Magufuli alithamini tiba hii ndio maana kuna wakati alitaka kila hospitali wawepo ili mtu aamue anaelekea upande upi wa tiba.

Lakini pia gharama za dawa wakati mwingine zinatokana na aina ya ugonjwa ulionao,mtu kaugua figo kwa miaka mingi anatumia dialysis mfano au ameshindwa kubadili figo Leo anataka akienda Tiba mbadala apone kwa elfu sitini itawezekanaje?wakati dialysis ya Siku moja tu alikuwa labda anatumia 250,000/-
 
Umemuelimisha viuri,Kitu kingine lazima wajue hizi ni Tiba lishe zinafanya kazi taratibu kwa sababu lazima ziingie mwilini kama lishe kwa hio muda pia wa kutumia dawa lazima uwe mrefu ili kupona tofauti na hospitali ambako ukifika unahoma unatundikiwa drip moja kwa moja inaingia kwenye damu baada ya muda unaruhusiwa kutoka.
 
Ni kweli kabisa hakuna kipimo cha kupima mwili mzima na kubaini magonjwa. Ni utapeli tu.

Mtu akiumwa akienda kwa daktari akajieleza dalili anazopata ndizo humsaidia daktari kujua aina ya uchunguzi na vipimo vya kumfanyia, na ndiyo maana huwezi ukafanyiwa vipimo vyote vilivyopo hospitalini kwa wakati mmoja.

Hivi vinavyoitwa vipimo vya mwili mzima havipo popote pale ni huko mtaani tu wanadanganya. Wengine wanaenda na kuambiwa wana magonjwa makubwa ambayo kiuhalisia hata hamna.
 
Shida nyingine ni wagonjwa wenyewe.Mtu Ana tatizo la miaka mitano na zaidi na ameshatumia tiba mbalimbali ikashindikana,lakini anakuja unaiona kabisa kwa dawa ulizonazo atapona.Unampatia dozi halafu baada ya siku mbili anakwambia sioni nafuu yoyote. Yaani anataka apone ndani ya siku mbili ugonjwa sugu alioishi nao kwa miaka Saba! Hi ni ajabu! From no where anakata tamaa kutumia dawa na anaitelekeza na hell keshatoa. Mfano watu wengi wa shida ya nguvu za kiume wana changamoto hii,anataka atumie dozi siku mbili ya tatu aalike demu wake aangalie matokeo....!! Ndiyo maana badala ya kupewa tiba ya kudumu wanachanganyiwa booster za Viagra ili akimeza tu asisimuke.Jambo ambalo linaendelea kumuua taratibu.
Tukubali pia tiba inahitaji utulivu na kujipa muda,ukifuatilia vizuri na kukubali kujipa muda was kutibu tatizo unapona kabisa.
 
Kuna mmoja alimwambia mgonjwa eti damu yake imeganda..!! Yaani..!!
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, shika sana elimu, usiache aende zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…