Farolito
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 12,001
- 27,175
Poa nitakuchekiaKaka tusaidiane taarifa, watu tuko kwenye mateso ya magonjwa na hatujui hatma yetu, nisaidie mawasiliano yake inbox kama hutojali.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Poa nitakuchekiaKaka tusaidiane taarifa, watu tuko kwenye mateso ya magonjwa na hatujui hatma yetu, nisaidie mawasiliano yake inbox kama hutojali.
Nadhani serikali ishugulike na kudhibiti gharama tu ikiwezekana iingie hata kwenye bima ili huduma hii iwe nafuu kwa watu,Magufuli alithamini tiba hii ndio maana kuna wakati alitaka kila hospitali wawepo ili mtu aamue anaelekea upande upi wa tiba.Mkuu mpaka hawa watu wanaonekana matapeli ni gharama zao za dawa,dawa ni aghali mno kulinganisha na uhalisia wa kipato chetu,kipimo Chao ni elfu ishirini tu,vipimo hospitali zetu ni zaidi ya hao jamaa nimepiga mri hospitali ya rufaa mbeya,pamoja na mambo yetu Yale ilimigharimu laki Tano,na ufumbuzi wa tatizo sijapata huu tuiteje ni utapeli ama sayansi? Ukiwa mgonjwa unajaribu Kila kitu na huwezi hesabu hasara km unaumwa ukiona unauwezo wakuhesabu hasara kuwa umepona
Umemuelimisha viuri,Kitu kingine lazima wajue hizi ni Tiba lishe zinafanya kazi taratibu kwa sababu lazima ziingie mwilini kama lishe kwa hio muda pia wa kutumia dawa lazima uwe mrefu ili kupona tofauti na hospitali ambako ukifika unahoma unatundikiwa drip moja kwa moja inaingia kwenye damu baada ya muda unaruhusiwa kutoka.Ndugu zangu utapeli uko kila mahali,lakini haimaanishi kuwa hakuna uhalisia.Kwenye tiba mbadala tunatibu magonjwa mengi Sana ambayo katika hosp zetu yameshindikana.Mgonjwa anakuja ametembea hosp nyingi na zote kubwa kwa majina lakini Bado hajapona au kupata nafuu ya ugonjwa wake,lakini akitumia dawa zetu anaendelea vizuri na kupona kabisa.
Changamoto iliyopo ni kwamba watu wanaamini ukitibiwa ni lazima upone tu Jambo ambalo siyo sahihi.Kuna level ya ugonjwa ambayo pia ni ngumu kupona maana pengine umeugua muda mrefu na ugonjwa umeshaharibu kila kitu na unaelekea mwisho.Kwa hiyo Kama ambavyo unaweza kufariki au kutokupona hata Kama umeenda India,Bugando,Mhimbili n.k ndivyo ambavyo hata kwenye tiba zetu unaweza usipone.
Nilichonacho uhakika ni kuwa, ikiwa mtu atawahi ugonjwa ukiwa Bado haujaharibu mifumo yake mhimu kupona ni lazima,dawa za mimea Zina nguvu na miujiza mikubwa kulikoni wengi wanavyofikri na hata kuziponda.Wengi wamesaidiwa kupitia tiba hizi hususani magonjwa yasiyo ya kuambukiza Kama presha,kisukari,bawasiri,vidonda vya tumbo,uzazi na mengine mengi.
Kwa hiyo tusitukane ukunga na uzazi ungalipo,Kama ulishindwa kupata msaada sehemu,Basi Kuna mwingine alipata kupitia hapohapo
Ni kweli kabisa hakuna kipimo cha kupima mwili mzima na kubaini magonjwa. Ni utapeli tu.Umasikini na ujinga ni jambo baya sana. Watu wa tiba mbadala wanatapeli sana watu.
Ususani kwenye mambo wanayosema ni vipimo eti wana kipimo cha kupiga mwili mzima, na hicho kipimo mtu anashika kama pensel wanakutajia magonjwa kibao.
Pia wana kipimo kama kioo unaweka mkono wako kwenye kioo, wanasema eti linasoma mwili mzima.
Sasa hivi vipimo hata hospitali za serikali au hata hospitali kubwa kwa hapa ya tanzania hakuna.
Ninachoona ni umasikini na ujinga wa elimu ndomana watu wanaibiwa serikali iangalie watu wanatapeliwa sana.
Kaka tusaidiane taarifa, watu tuko kwenye mateso ya magonjwa na hatujui hatma yetu, nisaidie mawasiliano yake inbox kama hutojali.
Kuna mmoja alimwambia mgonjwa eti damu yake imeganda..!! Yaani..!!Umasikini na ujinga ni jambo baya sana. Watu wa tiba mbadala wanatapeli sana watu.
Ususani kwenye mambo wanayosema ni vipimo eti wana kipimo cha kupiga mwili mzima, na hicho kipimo mtu anashika kama pensel wanakutajia magonjwa kibao.
Pia wana kipimo kama kioo unaweka mkono wako kwenye kioo, wanasema eti linasoma mwili mzima.
Sasa hivi vipimo hata hospitali za serikali au hata hospitali kubwa kwa hapa ya tanzania hakuna.
Ninachoona ni umasikini na ujinga wa elimu ndomana watu wanaibiwa serikali iangalie watu wanatapeliwa sana.