Tiba mbadala ya Cancer inapatikana wapi?

Tiba mbadala ya Cancer inapatikana wapi?

mama D

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
19,981
Reaction score
35,581
Habari za Jumapili wapendwa.

Kama kichwa habari kinavyojieleza, kuna dada wa rafiki yangu amepata hili tatizo la Cancer.

Alianza kuumwa mwaka jana June alikwenda hospital wakampa rufaa ya kwenda Ocean Road ambapo walithibitisha ana Cancer ya ziwa, ila mgonjwa na mume wake hawakuanza tiba yaani Chemotherapy wala hawakuishirikisha familia kuhusu hilo tatizo.

Mwezi wa 9 mwaka huu mgonjwa alizidiwa ziwa likawa linatoa damu familia yake ikaambiwa kuhusu tatizo na pia wakaambiwa mgonjwa ameshaanza kutumia mitishamba na baada ya muda ikaonekana anapata nafuu.

Leo hii mgonjwa amezidiwa tena lakini sasa tatizo halipo kwenye ziwa bali ameishiwa damu na yupo hospitali ya Wilaya. Na pia hataki kabisa kurudi Ocean Road na hataki tiba za hemotherapy

Wakuu mimi binafsi nimeshauguza wagonjwa wa Cancer, matibabu yatolewayo Ocean Road ni makali sana na madhara yake kwenye mwili ni makubwa sana. Nikiri tu kati wagonjwa niliokuwa nawafahamu na walioanza Chemotherapy hakuna aliyemaliza.

Lakini pia kuna ambae alikataa na akaamua kutumia tiba chakula naona yuko poa japo mwenyewe anatumia kila anachoambiwa (hana muongozo kamili toka kwa mtaalamu mmoja).

Wakuu naombeni msaada wenu haswa kwenye upatikanaji wa tiba mbadala Mungu akijalia tumuone dada yetu akiwa na afya njema tena.

Asanteni sana.

Cc Deceiver MziziMkavu
 
Kuna mizizi nimesikia inatoka Dongo Besh, ni dose tatu tofauti kila dose ni 50,000 unakunywa mwezi mmoja. Baadavya miezi mitatu ukipima uko clear. Si cancer tu hata HIV nisikiavyo.
Asante sana Sky Eclat unaweza kunisaidia mawasliano ya huyo mtu wa DongoBesh? Nashukuru umenitia moyo pia kwamba kupona kupo
 
Kuna mizizi nimesikia inatoka Dongo Besh, ni dose tatu tofauti kila dose ni 50,000 unakunywa mwezi mmoja. Baadavya miezi mitatu ukipima uko clear. Si cancer tu hata HIV nisikiavyo.
Yupo rafiki yangu mmoja yeye ni Myahudi, aligundulika na cancer ya Kongosho. Kwa macho yangu nilishuhudia alianza kula organic food, alipewa ushauri na Rabi huko kwenye Sinagogi.


Sasa hivi yuko clear.
Nimejifunza kitu kipya

MTC | 101| [emoji769]
 
Yupo Mama wa Rafiki yangu naye aligundurika kuwa na Cancer, alianza kutumia Mstaferi kuanzia Juice yake Kila siku Glasi 3 asubuhi kabla hajala mchana na usiku. Pia akawa anatumia na majani yake, Alikua na hari mbaya sana lakini Mstaferi ukampa nafuu kubwa. Baadaye akaanza kuchanganya na Organic food zingine kwa Sasa yupo Vizuri tu.

Miti na Matunda ni dawa.

Unaweza pia kucheck Mtandaoni maajabu ya Mstaferi.
 
Mnhhh nenda hospitali, magonjwa Kama cancer sio ya kuficha familia yako isijue.. wenyewe ndio watakuuguza ..na pia mimi sio mtaalamu lakini nahisi ukiwahi matibabu at early stages ya cancer kwa chemotherapy then unaweza kuongeza muda wako wa kuishi ama remission ..NYIE MNAOTOA MATIBABU ONGEENI NA WAGONJWA WAPENI OPTIONS ZOTE WALIZONAZO ILI WAJIANDAE VIZURI,ULIZENI MASWALI NA MUWAPE CHANCE WAGONJWA KUULIZA MASWALI
 
Back
Top Bottom