Tiba ya harufu mbaya ya kinywa

Tiba ya harufu mbaya ya kinywa

clemence mtei

Senior Member
Joined
Feb 11, 2014
Posts
101
Reaction score
24
Naomba msaada nimetumia dawa na hospitali zote kupata suluhu ya harufu mbaya ya kinywa. Naswaki vizuri ulimi, meno na kwa dawa mpaka za 50k.

Nimetumia karafuu, tangawizi na aina nyingine za madawa ya dukani na asili ila changamoto ipo pale pale nikiongea na mtu anakimbilia kushika pua na kugeuza uso

Naomba msaada wadau. Changamoto inanikosesha raha.
 
Pole sana kaka, najua unavyojisikia maana harufu ya kinywa inakata stimu sana. Huwezi kula hata denda 😛😛
 
Naomba msaada nimetumia dawa na hospitali zote kupata suluhu ya harufu mbaya ya kinywa. Naswaki vizuri ulimi, meno na kwa dawa mpaka za 50k.

Nimetumia karafuu, tangawizi na aina nyingine za madawa ya dukani na asili ila changamoto ipo pale pale nikiongea na mtu anakimbilia kushika pua na kugeuza uso

Naomba msaada wadau. Changamoto inanikosesha raha.

Pole sana.

Ni muhimu ukaonana na daktari ufanyiwe uchunguzi zaidi ili kuweza kubaini chanzo cha tatizo lako.

Pia kama hujawahi kuonana na daktari wa kinywa na meno uonane naye akuchunguze, akufanyie usafi wa kinywa na meno na atakufundisha namna nzuri kusafisha kinywa na meno.

Kila la kheri.
 
Hydrogen Peroxide
Ya Kusukutua Mara Mbili Kwa Siku
20250306_213126.jpg
20250306_213135.jpg
 
Naomba msaada nimetumia dawa na hospitali zote kupata suluhu ya harufu mbaya ya kinywa. Naswaki vizuri ulimi, meno na kwa dawa mpaka za 50k.

Nimetumia karafuu, tangawizi na aina nyingine za madawa ya dukani na asili ila changamoto ipo pale pale nikiongea na mtu anakimbilia kushika pua na kugeuza uso

Naomba msaada wadau. Changamoto inanikosesha raha.
Na hii imevunja ndoa nyingi
 
Pole sana.

Ni muhimu ukaonana na daktari ufanyiwe uchunguzi zaidi ili kuweza kubaini chanzo cha tatizo lako.

Pia kama hujawahi kuonana na daktari wa kinywa na meno uonane naye akuchunguze, akufanyie usafi wa kinywa na meno na atakufundisha namna nzuri kusafisha kinywa na meno.

Kila la kheri.
Ni ushauri mzuri hapa ni ngumu kupata jibu la tatizo lake kwa sababu hakuna anaejua chanzo.
 
Sio kila harufu mbaya inayotokea mdomoni basi chanzo chake ni mdomoni, muda mwingine harufu hutomea tumboni ukiwa na changamoto za
-kansa, kufeli Kwa in na other metabolic diseases
-GERD
-Diabets
-magonjwa ya Figo na ini
-sjoggrens syndrome
Matumizi ya baadhi ya madawa
Na mwisho ni mfumo wako wa maisha kama uvutaji wa sigara, pombe na vitu vyenye caffeine
Hivyo jitahidi uende kwenye uchunguzi Ili kujua chazo halisi Cha hiyo harufu
 
Siyo Harufu zote zinatokea mdomoni zingine zinatokea tumboni usimalize hela kununua misakwi wahi kwa wataalamu
 
Anza kutumia chai ya majani ya limao bila sukari,asubuhi kabla hujala chochote na jioni baada yamlo walau vikombe viwili!!

Una tatizo la indigestion na harufu sii ya mdomoni Bali tumboni!!

Kwa usiku unawezaukaweka vipunje kama sita vya vitunguu swaum vilivyo katwakatwa vidogonakuviweka kwenye chai hiyo ya moto!
 
Hapo unahangaika na dalili lakini tatizo la msingi hujahangaika nalo.Tatizo liko tumboni.
 
Pole, punguza vyakula vyenye asidi nyingi. Safisha mfumo wako wa lymphatic system kwa ujumla. Then penda kunywa maji maji mara kwa mara unaweza penda kutafuna bazoka. Usiache kutumia karafuu punje mojamoja pindi unapoona unahitaji kuwasiliana na watu usisite ku-DM ukihitaji ushauri zaidi. Utakuwa sawa. Pia ningenda kujua kama hili tatizo ulizaliwa nalo au la
 
Back
Top Bottom