#COVID19 Tiba ya wagonjwa wa Corona Tanzania iko juu mno, Watanzania hawawezi kuimudu

Kajeba

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2020
Posts
1,057
Reaction score
2,364
Wakuu,

Nimekaa natafakari juu ya affordability ya matibabu ya gonjwa la corona hapa nchini na nimebaini kwamba haina urafiki na watanzania wenye vipato vya kati na chini

Hakika mwananchi wa kawaida hawezi kumudu gharama za kuwekewa mtungi wa oxgyen labda ziwe zinatolewa bure

Nasema hivi kwa sababu nimejaribu kufikiri zaidi pale ambapo kuna mzee wa miaka kama 60 alipatwa na ugonjwa huu wiki sasa na amepona now amejikarantini nyumbani kwake

Kilichomponya ni pesa alizokuwa nazo naweza kusema hivyo, kwani bill ya hospitali kwa muda wa siku 6 iliyotumika ni zaidi y 3.5

Najiuliza zaidi hivi ikatokea wewe mwenzangu na mimi pangu pakavu tia mchuzi ukakumbwa na sekeseke la covid 19 utaweza mudu gharama za huduma hii ili kunusuru maisha yako?

Ifike mahali sasa Serikali ibebe gharama zote zinazohusu wagonjwa wa Corona hapa nchini
 
Tiba gani ?

Dr. Dorothy si alituonyesha tiba jamani: malimau, tangawizi, kitunguu na pilipili kichaa ndio mnalalamika ?

Bupiji sauna 5000/= unajifukizisha , au zile sio tiba ?
 
Chanjo ikiletwa tutaweza gharamia au ndio wataweza akina mbowe pekee yao huku akiwaacha akina Erythrocyte wakiteketea na ukapuku wao?
Kinga ni bora kuliko tiba, sisi waswahili tuchukue tahadhari mapema

kinga ni bora kuliko tiba
 
nina miaka 20 sasa sijawahi kuwa na njaa , sina wasiwasi wowote wa kumudu matibabu popote duniani
 
Hii inchi taabu tupu

sijui serkali inafanya yote hayo kwa manufaa ya nani
omba mungu sana lisikupate!

yupo mama mstaafu pensheni yote karibu imeisha kwa kumuuguza tuu kovid..
 
Kwa nchi za wenzetu na majirani zetu pia hii inatolewa bure bila shaka
Chanjo ikiletwa tutaweza gharamia au ndio wataweza akina mbowe pekee yao huku akiwaacha akina Erythrocyte wakiteketea na ukapuku wao?
Kinga ni bora kuliko tiba, sisi waswahili tuchukue tahadhari mapema

kinga ni bora kuliko tiba
 
Wakuu,

Nimekaa natafakari juu ya affordability ya matibabu ya gonjwa la corona hapa nchini na nimebaini kwamba haina urafiki na watanzania wenye vipato vya kati na chini

Hakika mwananchi wa kawaida hawezi kumudu gharama za kuwekewa mtungi wa oxgyen labda ziwe zinatolewa bure

Nasema hivi kwa sababu nimejaribu kufikiri zaidi pale ambapo kuna mzee wa miaka kama 60 alipatwa na ugonjwa huu wiki sasa na amepona now amejikarantini nyumbani kwake

Kilichomponya ni pesa alizokuwa nazo naweza kusema hivyo, kwani bill ya hospitali kwa muda wa siku 6 iliyotumika ni zaidi y 3.5

Najiuliza zaidi hivi ikatokea wewe mwenzangu na mimi pangu pakavu tia mchuzi ukakumbwa na sekeseke la covid 19 utaweza mudu gharama za huduma hii ili kunusuru maisha yako?

Ifike mahali sasa Serikali ibebe gharama zote zinazohusu wagonjwa wa Corona hapa nchini
Nakwambia hivi viongozi wengi wa kiafrika wanafaidika sana na hii COVID19, tena kuna wengine wanaomba labda isiishe kwani ni sehemu ya kupiga pesa kutoka kwa mabeberu, na kuzifanyia mambo mengine tu, ila wananchi ndio wanaumia!!ukiangalia , vipimo unalipia, gesi unalipia, mask mnanunua, sanitizer, hivyo hivyo, hayo mabilioni yanatumika wapi?mfano uganda nako mtu akilazwa siku moja tu karibia dola 1000!!!hospitali binafsi, anaulizwa waziri anasema" jamani tusiumizane hivyo sisi wote ni Waganda"wao wanachowaza ni kushindana kwa kutoa takwimu tu za vifo na maambukizi ili mpunga uzidi kuingia tu!!mfano mzuri hapa kwetu yale mabilioni ya IMF, kipindi kile ndio imeanza, huku taasisi kibao binafsi zikawa zinachangia kila leo mabilioni, na vifaa tiba, lakini kwenda kupima corona ulikuwa unachajiwa pesa!!!
 
Back
Top Bottom