Tetesi: TIC imedorora, wawekezaji wayeyuka!

Tetesi: TIC imedorora, wawekezaji wayeyuka!

Waende zao, hatuwahitaji kwasasa, tunajenga viwanda kwa " hela zetu". Kwanza tumeondoa masharti magumu, ukiwa na vyerehani vinne unapewa hadhi ya umiliki wa kiwanda, kwahiyo wasitusumbue tutakua na mivijiwanda mingi tu bila msaada wao
 
Huu ni msimamo hasi kwa uwekezaji.
Viongozi si wawekezaji, wao wako upande wa matumizi tu ya kodi, hawazalishi.

Sasa juzi sheria ya Arbitration imepitishwa Bungeni.
Ati mkikosana na muwekezaji itakuwa marufuku kwenda kukubaliana nje ya nchi(Arbitration), kwa taratibu za kimataifa.

Nategemea hili ndo litawakimbiza kabisa hata wale wachache waliokuwa na mawazo ya kuja Tanzania.
Time will tell.
Kweli mambo mengine yanafurahisha yaani muwekezaji na akili zake na pesa zake aje acheze kamali kwa kukubali usuluhishi wa hizi mahakama zetu ambazo zinaongozwa na mtu mmoja!!!huyo huyo kila siku ndio anakurupuka kuvunja mikataba hala ukimbilie kwenye mahakama zake??!huko kwenye mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya uwekezaji sio kwamba tunashindwa kwa figisufigisu bali ni ulafi wa viongozi wetu waliotanguliza matumbo yao mbele wakati wa kusaini mikataba hiyo!!!leo mnaanza walaumu wazungu kuwa wanatuonea??hata hivyo kwenye mali asili,madini ni wapi ambako kumebakia hakujaibiwa??
 
kipaumbele cha awamu hii ni 'kuwakomesha' walizonazo, mwenyenazo akiwemo mwekezaji anaweza kufanywa chochote dakika yoyote ( in jiwe voice)
Nchi ya ajabu kweli tra walikuwa kila mwaka wanakukadiria kodi unayotakiwa kuilipa na unailipa baada ya kujirizisha kuwa ndio unastahili kulipa!!baada ya miaka mitano wanakuja na kukwambia kuwa kumbe walikosea makadirio ya kodi ,wali kadiria kidogo hivyo kila mwaka kuna tofauti ya milioni kama 300!!hivyo una deni la 1.5 bilioni!!!haaaaa wakati hiyo pesa hata kuitia mkononi hujawahi,ndio kinachowakuta wau sasa!!!!ndio wanakuja mala ohooo tukae chini tujadiriane jinsi ya kuyafuta!!!kuna jamaa mmoja alikuwa muuza vinywaji vya jumla anadaiwa zaidi ya bilioni 300!!!
 
Kuna tetesi kuwa idadi ya wawekezaji wapya kupitia kituo cha Uwekezaji, TIC imepungua sana ndani ya miaka miwili iliyopita.

Waekezaji wengi, inaelezwa, wanachungulia hali na kuahidi kurudi, lakini wanaishia.

Tujitahidi Watanzania tuwekeze wenyewe.
Ubabe unawatia hofu wawekezaji wa nje au ndani.

Kuna wafanyabiashara kibao wanabugudhiwa sana awamu hii. Na fimbo inayotumika ni TRA. Hili linakuja kutokana na kutokuwa na utawala wa sheria.

Mfanyabiashara akitofautiana tuu na mwanasiasa TRA wanatumwa na unaitwa mhujumu uchumi/mkwepa kodi kwenye majukwaa ya kisiasa badala ya mahakama itende haki kwa uhuru
 
Huu ni msimamo hasi kwa uwekezaji.
Viongozi si wawekezaji, wao wako upande wa matumizi tu ya kodi, hawazalishi.

Sasa juzi sheria ya Arbitration imepitishwa Bungeni.
Ati mkikosana na muwekezaji itakuwa marufuku kwenda kukubaliana nje ya nchi(Arbitration), kwa taratibu za kimataifa.

Nategemea hili ndo litawakimbiza kabisa hata wale wachache waliokuwa na mawazo ya kuja Tanzania.
Time will tell.
Umesema kweli mkuu.
Wao wanasiasa wanajiona wako sawa wakati wote.

Najiuliza ile kesi ya jamaa wa milioni 7/dakika iliishaje? Aliunganishwa Mrema kwenye hii kesi.
 
Kuna tetesi kuwa idadi ya wawekezaji wapya kupitia kituo cha Uwekezaji, TIC imepungua sana ndani ya miaka miwili iliyopita.

Waekezaji wengi, inaelezwa, wanachungulia hali na kuahidi kurudi, lakini wanaishia.

Tujitahidi Watanzania tuwekeze wenyewe.
Wawekezaji Serious lazima watakuja tu, ila wapigaji lazima waingie Mitini this is TZ Mpya Baba Mwenye Mali kaamka usingizini.
 
Wawekezaji Serious lazima watakuja tu, ila wapigaji lazima waingie Mitini this is TZ Mpya Baba Mwenye Mali kaamka usingizini.
Mkuu kuamka kiakili zaidi ni kuwekeza mwenyewe.
Hakuna mtu "serious" atatoka kwao kuja pigwa kodi na levies za kimagumashi na hivyo kuongeza gharama za uzalishaji.
Kama wewe unaweza kuhimili kodi, tozo, maduhuli na levies zilizo nyingi na bado ukafanya biashara ya faida, basi changamkia fursa hiyo, kakope na uingie kazini.
 
Ndugu yangu tuombe umri tu TZ inakuja kuwa Nchi nzuri mno, wenye mtazamo huru/Chanya wanalijua hili.
Tatizo kubwa litakalo tusumbua ni wazamiaji toka Nchi zingine kuja kutafuta maisha hapa TZ.
 
Ndugu yangu tuombe umri tu TZ inakuja kuwa Nchi nzuri mno, wenye mtazamo huru/Chanya wanalijua hili.
Tatizo kubwa litakalo tusumbua ni wazamiaji toka Nchi zingine kuja kutafuta maisha hapa TZ.
Wishful thinking!
Ati nchi ya asali na maziwa, wakati mnapumzika kwenye vivuli vya mikorosho mkitazama na kukodolea wageni airport, ili mpate mtu wa kumpiga kodi ili uendelee kuishi kwa mgongo wa "mfadhili" au "muwekezaji"!!
Maisha ya kuijidharau hayo!
 
Tutaishia kuilaumu TIC na wanaweza wakatumbuliwa wakuu wake au hata Taasisi/kituo chenyewe kuvunjwa kabisa

Lakini kwa uhakika kabisa tunajua tatizo halisi liko wapi. Ni hadi pale Tanzania kama nchi itakataa maneno ya mtu mmoja hata awe na cheo gani ndio yawe sheria za nchi

Kwamba kwamba katiba, sera, sheria, kanuni na taratibu zote za nchi zinawekwa pembeni na zinakoma pale kiongozi huyo anapotoa kauli kwa jinsi anavyopenda yeye,hilo ndio tatizo

Hakuna mwekezaji makini atakae tia mguu hapo, tutaishia kupata wababaishaji, wapigaji na ma opportunists tu

Mkuu umesema ukweli mtupu. Usizunguke kusema mtu mmoja, sema tatizo ni rais.
 
Ndugu yangu tuombe umri tu TZ inakuja kuwa Nchi nzuri mno, wenye mtazamo huru/Chanya wanalijua hili.
Tatizo kubwa litakalo tusumbua ni wazamiaji toka Nchi zingine kuja kutafuta maisha hapa TZ.

Mkuu unaota wewe, hayo maneno unamezeshwa na wazalendo uchwara ambao hawajawahi kufanya biashara yoyote na hawana lolote wajualo kuhusu biashara. Kwa sera hizi nchi hii inaenda kuwa fukara moja kwa moja. Hizi hadithi za nchi kuwa nchi bora alikuwa nazo Nyerere, akataifisha mali za matajiri. Kilichokuja kutokea ni wananchi kuvaa viraka na hadi anatoka madarakani nchi ilikuwa imekuwa masikini wa kutupwa.
 
Kuna mzungu namfahamu baada ya hiyo arbitration kuongelewa bungeni amesitisha kuja kuwekeza Tanzania. Alikuwa na mpango wa kufungua Viwanda vya kusindika na kuuza ulaya Samaki wa ziwa Tanganyika. Lakini pia kuna uwekezaji wa Kilimo cha Chai na Korosho.

Nimesikitika sana tena sana kwa cash flow plan yake investment yake ilikuwa inatengeneza ajira kibao nikiwemo Mimi.

Naiomba serikali iache kukurupuka tunaoumia ni RAIA.
 
[emoji23] [emoji12] Hapa kazi tu .
Watanzania wengi pumbavu sana. Kwa hiyo mnashangilia uwekezaji usio na tija. Ina maana gani mtu aje kuwekeza bila manufaa kwa nchi. Bora tubaki bila hao wezi
 
Back
Top Bottom