Jamani kuwa na taasisi nyingi siyo jambo baya. Kwanza inaleta ufanisi na pili inaongeza ajira. Baba zenu, kaka na dada zenu, wadogo zenu n.k wanafanya kazi huko. Kama zisingekuwepo wangepata kazi wapi? Pili kazi ya serikali siyo kupunguza matumizi. Sasa ipunguze matumizi ili iweje. Kazi ya serikali ni kuhakikisha pia wananchi wake wabapata kipato cha kuspend ili mzunguko wa fedha uendelee na maisha yaendelee. Serikali leo ikisema inaelekeza fedha zote kwenye muradi ya elimu na afya tu watu kibao wataathirika hata waliojiajiri na walioko kwenye private sector
Tanzania ni mwendo wa kuchuma, baadae ndo wanavutagana wenyewe kila mmoja anataka awe juuvya mwingine!
Kuna TFDA, TBS, Mkemia mkuu, pharmacist association nini sijui nao walishakuwa na mgogoro na TFDA kwa mwingiliano wa kazi. kuna mwingiliano wa kimaslahi kati ya Shirika la petrol na Eruwa hiii nayo ilitakiwa kuunganishwa na kuongeza idara badala ya sasa kuwa na mrundikano wa taasisi ambao mwisho wa siku ni mzigo tu.
Lowassa 2015 vunja huu upuuzi!
Tunakoelekea Huko mtashauri hata shule za msingi na secondari ziunganishwe na Kuwe na shule moja tu Tanzania nzima.Hapo hapo kuna DUCE, MUCE na UDSM School of Education wote wanatoa/wanafundisha walimu but kila taasisi ina mkuu na ana entitlement zote kuanzia V8/Vx mpya, posho na kuwekwa kwenye bodi kibao za kutafuna pesa safari kila kukicha