TIC, TAN-TRADE, EPZA, TTB & BRELA: Mrundikano wa Taasisi zinazofanya kazi zinazofanana

TIC, TAN-TRADE, EPZA, TTB & BRELA: Mrundikano wa Taasisi zinazofanya kazi zinazofanana

Asante JPM kwa kuunganisha baadhi ya wizara, japo kwenye makatibu wakuu nako umejaza wengi mno. Sasa hamia katika kupeleka muswada bungeni kuunganisha baadhi ya taasisi/wakala/mamlaka, mfano;TanTRADE, TIC, EPZA & TTB (wanafanya kazi almost zinafanana) na pia TACAIDS & National AIDS Program.
 
Baadhi ya mikoa inapaswa kuunganishwa, sikuona mantiki ya kugawa mkoa wa RUKWa na kuongeza mkoa wa KATAVI, East Africa Community (EAC) tunataka kuungana sisi tunazidi kuzalisha MIKOA/WILAYA mpya zaidi.
 
Huu upuuzi wa kuanzisha wakala lundo zinazodili na mambo yanayofanana ni kutokujielewa,tunapoteza fedha nyingi na kuongeza ukiritimba.Hivi majuzi Magu alianzsha mkoa eti wa Songwe for what? Mikoa,wilaya na tarafa havina tija badala yake wadecentralize kwenye local authorities
 
Mkoa wa Songwe ulianzishwa na yule Profesa aliyepita si Magu (rekebisha). Fikira TACAIDS ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Mpango wa Kudhibiti Ukimwi upo Wizara ya Afya. Huku kikosi cha kudhibiti Madawa ya Kulevya (JESHI LA POLISI) na kuna kitengo kingine cha KUDHIBITI MADAWA YA KULEVYA (chini ya Kamanda Shekiondo - chini ya ofisi ya Waziri Mkuu. Bongo janja janja nyingi sana aisee.
 
Taasisi nyingi zimekaa kiulaji tu. ama ziunganishwe au zifutiliwe mbali. Mfano TCU & NACTE wanafanya kazi zinazofanana sana lakini ni taasisi 2 zinazojitegemea.
 
Dar es Salaam Institute of Technology, Arusha Techinical College, National Institute of Transport, Mbeya Tech (sijui sasa inaitwaje) nazo hizi zinafanya kazi inayofanana zingefanywa taasisi moja
hapa ni sawa na kusema kuna Mzumbe sec school, Ilboru sec school, Tabora boys sec school, Nsumba sec school, Musoma tech school, Moshi tech school, Tanga school etc.... zote ziunganishwe tuwe na shule moja tu!! aiseeee
 
hapa ni sawa na kusema kuna Mzumbe sec school, Ilboru sec school, Tabora boys sec school, Nsumba sec school, Musoma tech school, Moshi tech school, Tanga school etc.... zote ziunganishwe tuwe na shule moja tu!! aiseeee
Maana yangu hautitaji kuwa na watu wenye shahada moja lakini kitaaluma wako tofauti sana kutokana na chuo alichosoma. Hizo shule ulizotaja zinafanya mtihani mmoja hivyo Division one ya Mzumbe Sec na Division one ya Ilboru upeo wao wa uelewa unalingana
 
Ndachuwa umemjibu jamaa kitaalamu mno wewe ni GREAT THINKER! taasis hiz hubuniwa na wasomi/wanasiasa kwa manufaa binafsi (VYEO/MARUPURUPU) tena wamegundua sasa kuanzisha kampasi mikoani bila kuajiri walimu huko mikoani ili kutunga safari (posho) kila uchao kwa walimu waliopo main campus (Dar). mfano eti Chuo cha utumishi wa umma wana kampasi Dar, Tabora, Mtwara, Tanga n.k. CBE...Dar, Dodoma, Mwanza n.k. DIT>>>Dar, Mwanza, TIA>>Dar, Mtwara, Mbeya, Singida n.k.
 
EWURA unaambiwa Mkurugenzi mkuu analipwa 36 Million (Tshs.) Daah hatari sana hii nchi. Na bora tungeona ufanisi wa hizo taasisi. Bado ni mazingaombwe tu pamoja na mishahara minono hivyo (Hapo bado anapewa GARI, V8, Simu analipiwa Airtime, NYUMBA) Safari za ndege ni Business Class na kufikia Hoteli ya hadhi ya Nyota 5.
 
RWANDA: Waliunganisha vyuo vikuu vyote vya Umma ns kuwa na 1 (UNIVERSITY OF RWANDA) sisi;
1. TRA vs ZANZIBAR REVENUE BOARD!!!
2. TZ investment Centre vs Tanzania Investment Bank vs TZ women's Bank vs TZ Agricultural Development Bank!!
NB:
Waziri wa Biashara Dr. Charles Mwijage (PhD) fuatilia haya.
***Wakora Waitu.
 
Umefika wakati wabunge wetu walione hili na kulisemea bungeni ili serikali ipeleke muswada bungeni kwa ajili ya marekebisho. Haiwezekani useme serikali inataka kubana matumiz na wakat una taasisi kibao kama TIRDO, CARMATEC, Bodi ya Maziwa, Tanzania Food & Nutrition Centre etc. ambazo tija yake ni ya mashaka
 
blessings! safari zimekata mazima, maana mpaka kibali, na hata hao maboss wachache wanaosafiri wanalazimishwa kupanda ndege za ajabu ajabu (ethiopian) kiukweli tumeathirika pakubwa hela hamna.
 
Dar es Salaam Institute of Technology, Arusha Techinical College, National Institute of Transport, Mbeya Tech (sijui sasa inaitwaje) nazo hizi zinafanya kazi inayofanana zingefanywa taasisi moja
Mkuu, kwani hizi ziko katika mkoa mmoja ? Huoni kuwa hivi ni vyuo vya ufundi katika mikoa hiyo ? Basi kwa mawazo yako, hata shule za Upili ziunganishwe maana unakuta wilaya moja inazo hata 50 !!!
 
Ukitaka kujua kama kazi zao zinashabihiana au la angalieni sheria iliyoanzisha kila taasisi. Mimi nina uhakika kila taasisi ina kazi zake ambazo zinatofautiana na taasisi nyingine. Tatizo ninaloliona ni ufanisi katika utendaji wa taasisi hizi unatokana na usimamizi dhaifu wa Serikali.
 
Back
Top Bottom