...mnh, by the time vijana wa mzee wa Hosea wanaidaka hii, jamaa watakuwa weshabadilisha system ya ku feed info kwenye mtandao. TAKUKURU wakivamia ofisi wanapewa mafaili yenye vumbi, ...wakati wanayapekua, wakipiga chafya mfululizo, ...wajanja wanafyonza (kuondoa) evidence kwa USB.
Mume huyu ana info zote za madhambi ya mkewe, ila kiapo cha ndoa na 'Ukweli wa maisha' vinamfunga.
Mbona wewe kakwambia??
Alafu we ungekua TAKUKURU bila yeye kujua ingekuaje???Na wewe kiapo cha urafiki kingekufunga?
hiyo yote ni sehem ya rusha roho na hayo mahela anayoiba pengine alitakiwa akuwe na at least magorofa sita mbezi (mbu atafafanua hii). mimi mwenyewe natamani nimjue ili anijaffarai nami nimshyrose banji. hela tam bana. washenzi wamecancell loan yangu
Mwambie mume asiwe na wasiwasi itakuwa anajua anavyojichotea huko ofisini aisee! Ila magari ni rahisi kushitukiwa ofisini ila angeinvest kwenye nyumba anunue share kwenye makampuni mbalimbali, ofisini hawawezi jua, ndio maana kuna msemo unasema mwenye gari zuri asiringe kwani watu wakiamua kutembea na nyumba zao anaweza jiona takataka. ila huyo dada anaonekana ana kaushamba ka magari vile!
Mbu hii Topic nimecheka saana nitachangia kesho:A S-coffee:
Kama unawafahamu waambie wa waendelee kukaa kwenye position punguze speed, watumishi wa serikali wanatumiaga vigari vya ajabu hata kama wana pesa kiasi gani ilizao...sidhani ni kaushamba, ila ni mshabiki wa ile tabia ya rusha roho. Ni kweli usemayo kuhusu nyumba, lakini huenda anaamini wataouona uzuri wa nyumnba yake ni majirani tu wakati azma ni kila mtaa ataokatisha watu wabakie "e bana wee, waleee...!"
It's hillarious, lakini ndio hivyo tena. Mshipa wa woga ushamtoka.
...ha ha! ...haya bana.
Very interesting.......
Mama fisadi.....mzee kakwama....ila akasahau dhambi ya kwanza ni kukubali vinono vya mara ya kwanza....akitegemea mke ataacha....!
Alinywe tu aisee...he is part of it!
Honestly Naogopa kuoa! Km mambo ni haya bora nibakie single!
Mwambie mume asiwe na wasiwasi itakuwa anajua anavyojichotea huko ofisini aisee! Ila magari ni rahisi kushitukiwa ofisini ila angeinvest kwenye nyumba anunue share kwenye makampuni mbalimbali, ofisini hawawezi jua, ndio maana kuna msemo unasema mwenye gari zuri asiringe kwani watu wakiamua kutembea na nyumba zao anaweza jiona takataka. ila huyo dada
anaonekana ana kaushamba ka magari
vile!
Mbu usikute umekatiwa kitu kidogo ili ufiche siri!Kumbuka..mficha fisadi ni sawa na fisadi!Siku wakidakwa wanakutaja kama mshauri/mshawishi mkuu!
HIvi, ni nani ambaye akipata nafasi ya kula kidogo naye hatokula kama kwa kufanya hivyo anajihakikishia maisha mzuri yeye na familia yake? Ni lazima tujue kuwa vita dhidi ya ufisadi ni pana sana kwani inatugusa hata sisi wenyewe kwa namna moja au nyingine. Japo si wote tunaweza kuingia mikataba mibovu na si wote tunaweza kuchota mabilioni lakini ni wangapi kati yetu ambao wanajua wakiongoza sifuri moja au wakigeuza sita kuwa nane au tano kuwa mbili ni tofauti kati ya kumalizia kibanda na kuendelea kulala kwa mama mwenye nyumba?