...tick-tick!...Mke kanogewa na Ufisadi; Mume hajui la kufanya

Mbu endelea kuomba maana unaweza kuta maongezi yenu yote yapo kwenye hard disk somewhere.Sasa kama ushauri waku unaegemea kwao zaidi ya kuacha ufisadi wakianguka wanakuvuta na wewe!Sweet eh?

...ha ha ha!, najua sana hilo...
...'nawasaidia' kuunganisha the dots! (kwa manufaa ya taifa)
 
DAH..!!!!!!!!!!!! ZA MWIZI AROBAINI!!!! ANYDAY KITANUKA!!!!!:lol: Dah..jamaa lazima awe mpole.....anaweza pewa talaka faster!!! :tongue:

...anazibwa mdomo kwa Vogue bana, talaka ya nini?
Labda jamaa aliuze fasta fasta kabla jamaa wa Anti Corruption hawajavamia!
HA HA HA!

Haki ya mungu si maisha haya. Walking on egg shells.
Nyumbani pakipigwa hodi, mbio dirishani anachungulia, nani?
Keshawaagiza hausigeli na mlizi, akija mgeni yeyote wasiyemjua, ambiwe hayupo!

Akiwa anarejea nyumbani, anazunguka mitaa miwili mitatu kuhakikisha hakuna anayemfuatilia na gari.
Akipigiwa simu na Private number, au namba asiyoijua hapokei!
Hana amani tena na maisha anayoishi,... anavaa mkofia mkuuubwa kuficha uso!
Hata kazini kwake utendaji wa kazi ushaathirika...

Akishafukuzwa kazi si ndio balaa zaidi?
Anyway, naendelea kumpa moyo mshkaji.
Tunaamini "mungu hatomtupa mja wake!" 😛ray:
 
Hayo yote na bado mama haoni hatari?Mume tu ndo mwenye wasiwasi!Kweli sikio la kufa halisikii dawa!
 
Reactions: Mbu
Tatizo la wizi, ukishapata huachi kuiba. Huyo baba aingie kwenye maombi Mungu ni mwaminifu atatenda miujiza. Ila sasa huyo mama nae asikie siyo siku zote ni jumapili, likibumburuka tu watarudi utoto.

Haya utandawazi wa na WAMAMA
 
Reactions: Mbu
mkuu mbu avatar yako ya zamani kwa nini umibadili? zamani ulitia fora na kina fidel, masanilo na ..
 
Reactions: Mbu
mkuu mbu avatar yako ya zamani kwa nini umibadili? zamani ulitia fora na kina fidel, masanilo na ..

...eti eeh?
aaah, upepo wa mageuzi kaskazini mwa jangwa la sahara umepelekea member wengi kutumia Avatar za sura zao/zinazofanana na wao,
nami nikajionea acha niendane na mabadiliko. Sikujua nachusha na hiki kipara changu.
Haya basi, ngoja nikatafute kwenye kapu zile picha za mdudu!

...but wait....d'u mean kwa picha hii nishajikamatisha kwa jamaa wa UWT? Uwiii!
 
ha ha ha "beyond empowerment" kuna mdada mmoja anafanya PhD ya hii kitu. Du wakiwezeshwa ni noma.
 
Reactions: Mbu
Mmmmmmmh!!!
Mama anataka kufuta machungu yote aliyokutana nayo kwenye safari ya maisha!!!
Sasa dah!!! Hii mikato mikato hii itakuja kumuumbua. Tena hiyo migari ya kutia wasiwasi hiyo. Pole baba, sasa baba si kichea cha familia mbona hakukataa hayo mapato ya udhalimu tangia mwanzo?

Na najua analetewa gari ananyamaza na atalitumia, kwa nini asimkateze mke wake? Mmmmmm huyu baba naye sio kiongozi mzuri, anajifanya hapendi tabia ya mkewe, kumbe ba yeye anavitumia vizuri vijesenti vya wizi!!!

Kha mbu, hapa ndo tunataka kuona ukichwa wa mwanaume ktk kuhakikisha nyumba haipati mapato ya udhalimu bwana!!! Vipi kama huyo mama hadi dili likamilike kuna mtu anapata uroda kwanza ndo kinaeleweka? Unadhani anafanikisha hayo madili peke yake? Nyuma yake kuna mwanaume lol. Mmmmmh mwanaume hapa kachemsha......mshauri asimame kama mwanaume kama kweli haipendi tabia ya mke wake.
 
yea..alafu watu wanalia na ufisadi! Ushauri mwingi humu umeelekezwa kumsaidia katika kuiba! Tz imeisha, imeoza, inanuka kama jalala!
njaa nyingi tu!
 

...Jamani LD, hivi kuna uwezekano wa kuwa na kichwa bila moyo wa familia? Huyo mama ndio heartbeats bana.
Halafu unamlazimisha mwanaume "asimame dede" wakati mifuko inatoka vumbi? Hata wanawe watamuasi. Yataka moyo kuukumbatia Umaskini!

yea..alafu watu wanalia na ufisadi! Ushauri mwingi humu umeelekezwa kumsaidia katika kuiba! Tz imeisha, imeoza, inanuka kama jalala!
njaa nyingi tu!

...naam, naam... "Mwenye njaa hachagui Uji!"
 
asalaaaaalaa yaani kama namuona mzee wa watu akihaha! do..........kweli umasikini mbaya!
 
Reactions: Mbu
Tafuta movie inaitwa MAD MONEY iangalie ukiwa na huyo rafiki yako. Story ni kama uliyoielezea hapa mume alijaribu kumzuia mkewe kuiba bila mafanikio mpaka wakashikwa. MAD MONEY starring. Queen Latifah and Diane Keaton.
 
 
Basi kama ameshindwa kuwa mvumilivu, akubali matokeo bwana!!!
Yani yeye asubirie tu, litakalo mpata ajue alilitaka mwenyewe.

...Amen LD, Amen...hata mimi nawaombea waendelee tu "for better or worse til death do them apart!"
 
Da ! Huyu mama au dada safi saaana,, mi nimempenda sana sana hasa anapoijali familia yake, anamthamini mumewe bila kujali kuwa yeye sasa mambo safi.....mi naamini anafanya hivyo ksb ana hasira na umasikini hakuipenda hata kidogo ile hali waliyokuwa wakiishi mwanzo na nahisi alijiwekea nadhiri moyoni mwake kuwa siku akivipata vijisenti lazima abadili hali ya maisha ya famili yake.,,kwa hili kweli big up!!!

Ila afanye kwa tahadhali kuubwa sana manake akishtukiwa tu ofisini kwake basi itakuwa imekula kwake....hizo investment azisambaze asiziweke zote sehemu moja (dar)...ilo la kuridhika mimi sijalielewa, hivi kweli kuna mtu analidhika na mali?? Au kila mtu ana hamu ya kuongezea zaidi ya kile alichonacho.......umasikini mbaya sana....

Big up mwanamke na endelea kuithamini familia yako ili mzidi kubarikiwa zaidi, na mpaka mumewe kafikia uamuzi wa kuomba ushauri inaonesha kuwa kati yao kuna mapenzi na kuthaminiana ndiyo maana hataki mkewe apate matatizo....lililo muhimu ni kufanya kwa tahadhari kubwa sana sana kwani nusa nusa nao hawalali.......asije kuishia lupango...
 
Reactions: Mbu

Mie nakukubali sana sana Michelle kwa ushauri wako mzuri. Ningepata mke km ww ......u r real great thinker!
 

...dah, aisee! ...uchambuzi, maoni na ushauri yako yamenivutia sana.
It's all about LOVE ndio maana huyu mama kaamua 'kujivisha mabomu' ya kujitolea mhanga.

Hii kesi imenikumbusha Sarah Martin Simbaulanga.
Mnh, Mw'Mungu atawanusuru hawa rafiki zangu. Kama jamaa wameinyaka hii, bandarini hakukaliki,
linaviziwa Range Rover Vogue litashushwa tokea container gani. ...Mtihani!
 
hayo magari anayonunua ndo yanamjengea kaburi lake

Aweke hela kwenye immovable assets na amfungulie mumewe biashara endelevu ili ikiwa noma waendelee ku maintain good life

si unajua TZ ukifanya ufisadi wakikustukia unasimamishwa kazi tu kiaina au ikiwa noma unapewa 5 yrs kama LIYUMBA then unatoka unapeta, mali huwa hawazitaifishi akina DPP.

Afu iyo ndoa imetulia, iko safi.
 
Nahisi kama mume yupo mguu ndani mguu nje yani anafurahia vitu vya ufisadi huku roho ikimuuma kama siku watashtukiwa. Kwakweli ikigundulika wataishi maisha ya shida sana mana mali zao zote zitafilisiwa. Kwahiyo mume kwenye kumshauri mkewe afikirie mbeleni siyo mwisho wa hatua zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…