Ticket za Abood za usafirishaji mizigo zinamuumiza mtumaji

Ticket za Abood za usafirishaji mizigo zinamuumiza mtumaji

The Spirit of Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2020
Posts
1,045
Reaction score
1,868
Naambatanisha ticket ya mzigo (tena nikiwa ndani ya bus).

kipengele namba 5 na namba 7 hazitakiwi kuwa hivyo.

Abood badilisheni huu utaratibu wa ticket,kwa kuwa haiwezekani mtu alipe ticket ya mzigo na upo kwenye "boot" ya bus ila mzigo ukipotea hamuwajibiki; haifai.

20210513_160401.jpg
 
Hata masharti ya kutuma mzigo kwa tractor hayapo hivi. Hapa unaweza kutuma mzigo mjinga mmoja akautamani akauchukua ukienda kupokea wanakwambia usinisumbue mzigo umepotea chapa mwendo na hauna la kunifanya soma masharti. Mzee abood wewe ni muislamu hii ni dhuluma ya wazi wazi
 
Wanakwepa lawama.
Naambatanisha ticket ya mzigo (tena nikiwa ndani ya bus).

kipengele namba 5 na namba 7 hazitakiwi kuwa hivyo.

Abood badilisheni huu utaratibu wa ticket,kwa kuwa haiwezekani mtu alipe ticket ya mzigo na upo kwenye "boot" ya bus ila mzigo ukipotea hamuwajibiki; haifai.

View attachment 1782896
 
Mwarabu wa Kilosa sijui kawaje siku hizi, huduma za mabasi nafikiri kahamishia kwenye malori, basi zake pia zimechookaa, BM, Al-Saedy, New Force wanamuacha mbali, katika gari 10 gari 7 hazina A.c., hata Dar Moro, yutong anabahilia mafuta sijui ndiyo kukongoroka tu! Aendelee na bunge!

Watanzania tukizongwa na competition, basi nongwa biashara tunamuachia Mungu. Ndiyo maana tunawaogopa majirani kufanya nao biashara.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Naambatanisha ticket ya mzigo (tena nikiwa ndani ya bus).

kipengele namba 5 na namba 7 hazitakiwi kuwa hivyo.

Abood badilisheni huu utaratibu wa ticket,kwa kuwa haiwezekani mtu alipe ticket ya mzigo na upo kwenye "boot" ya bus ila mzigo ukipotea hamuwajibiki; haifai.

View attachment 1782896
yani nisafirishe inch 65 yangu ya tv alafu wanambie imeibiwa nikae kimya labda hawanijui vizuri
 
Huo ni utaratibu wa mabasi yote sio Abood tu. Mimi siipendi kabisa sheria hiyo
Kuna malalamiko mengi sana ya abiria kuibiwa laptops kwenye hayo mabasi, sasa naanza kuona chanzo huenda ni deals zilikuwa zinasukwa kupitia kipengele hicho
 
Hapo wanajifurahisha tu na haya masharti sababu sheria inachoangalja katika mikataba, huwa wanaangalia je hakuna upande umependelewa. Ukiangalia sharti hilo la 5 na la 7 mahakama inaweza ikatengua sababu yamewekwa kwa upendeleo wa mtu mmoja.
 
Na kuna mahali abiria huwa wanaibiwa sana, sijui kama sheria ilishabadilishwa, ila unakuta abiria amesafiri na mzigo wa chini ya kilo 20 anatozwa nauli ya mzigo, wakati sheria inamtaka msafiri kulipia kilo ya 21 na kuendelea
 
Na kuna mahali watu huwa wanaibiwa sana, sijui kama sheria ilishabadiliswa, ila unakuta abiria amesafiri na mzigo wa chini ya kilo 20 anatozwa nauli ya mzigo, wakati sheria inamtaka msafiri kulipia kilo ya 21 na kuendelea
Wengi huwa wanapigwa sana kwenye hii kitu. Wajinga ndo waliwao aisee
 
Kampuni ya hovyo kabisa hii. Nimewahi kupanda na mzigo kugeuza nyuma tiketi nikasema huu ni UTAPELI wa wazi kabisa. Sitegemei tena kusafiri kwenye gari kama hilo ambalo halina usalama wa Raia na Mali yake
 
Kwa hio Mzigo ukiibiwa offisini kwao wao hawawajibiki, yaani Mwenye mzigo anatakiwa yeye ndo atoe security?
Hizi kampuni uchwara ni shida sana, no bora kutumia gharama kubwa kutuma DHL ambao ni full guarantee
 
Back
Top Bottom