Ticket za Abood za usafirishaji mizigo zinamuumiza mtumaji

Ticket za Abood za usafirishaji mizigo zinamuumiza mtumaji

Naambatanisha ticket ya mzigo (tena nikiwa ndani ya bus).

kipengele namba 5 na namba 7 hazitakiwi kuwa hivyo.

Abood badilisheni huu utaratibu wa ticket,kwa kuwa haiwezekani mtu alipe ticket ya mzigo na upo kwenye "boot" ya bus ila mzigo ukipotea hamuwajibiki; haifai.

View attachment 1782896
Sasa iko kipengele number #5, wale wafanyakazi wakupokea mizigo siwanaweza wakaiba mzigo wako wakigundua ni wa thamani kubwa, halafu ukawa huna pakwenda kuwashtaki kulingana na ayo mashart sijui terms zao
 
Hapo wanajifurahisha tu na haya masharti sababu sheria inachoangalja katika mikataba, huwa wanaangalia je hakuna upande umependelewa. Ukiangalia sharti hilo la 5 na la 7 mahakama inaweza ikatengua sababu yamewekwa kwa upendeleo wa mtu mmoja.
Sio mahakama hata tume ya ushindani wanaweza kutengua hata zile risiti wanazoandika mzigo ukinunuliwa hauwezi kurudishwa ni batili kwa mujiba wa fcc sema wengi hawana uelewa
 
Una roho nzuri hadi unawasanua.

Mimi ningehamiq bus jingine tu, mabus ni mengi mno sasa hivi.
 
Back
Top Bottom