TID Afichua: Nilijuta kuwa msanii kutokana na kuzuia nyimbo zangu kwenye Redio kwa Miaka Mitano

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Legend wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed maarufu TID, amefunguka kuhusu majuto aliyoyapata akiwa msanii. Akizungumza kwenye mahojiano na My Reply Show, TID ameeleza kwamba kitendo cha baadhi ya vituo vya Redio kuzuia kucheza nyimbo zake kwa zaidi ya miaka mitano na kukosa matamasha yao amekiri kuwa hali hiyo ilimkatisha tamaa na kumfanya ajute kuwa msanii.
 
Pole sana Kwa TID Mnyama

Wakati mwengine pamoja na vipaji vikubwa walivyonavyo wasanii wetu, suala la nidhamu ya kazi ni muhimu sana kuwa nayo.

Kusema kweli, TID Mnyama ni Legendary mwenye kipaji na sauti adhimu sana

Hebu kasikilizeni Wimbo wa Zeze pamoja na wimbo wa Asha.

The guy is so so talented

Tumpe Maua yake akiwa hai tusisubiri afariki Dunia
 
Radio ni hizo tu? Matamasha wanaandaa wao tu? Think outside the box waachane na hii victim mentality.

Boss wa sinza pazuri alipofanyiwa figisu akafungua media yake mwenyewe. Hakuanza malalamiko all day. Badilika tokana na mazingira dunia haijawahi kumuonea mtu huruma.
 
Hilo halina ubishi, jamaa ana talanta kubwa sana
 
Changamoto ya wasanii wengi wa zamani ni ulaibu wa madawa ya kulevya pamoja na Bange

Otherwise wanavipaji vikubwa sana vya Muziki.

Kuna wakati nilitaka kuanzisha Mradi wa kufanya show na hao wasanii wa zamani as Wana nyimbo nyingi nzuri na bado Wana mashabiki wengi pia.

Bahati mbaya mambo hayakuniendea vizuri, ila baada ya Uchaguzi mwakani nitajaribu kufanya japo Kwa Mkoa mmoja uwe kama Pilot, biashara ikienda vizuri naweza kuendelea
 
Akili mgando. Mtu au company yeyote ile haiwezi kuua kipaji chako unless wewe mwenyewe ukubali kushindwa.
Inategemea mkuu, maana vipaji vingi pia viliingia kwenye tasnia kwa kubebwa bebwa sasa ilikuwa wakiingia kwenye mgogoro ilikuwa watu wanapandishiwa show yaani siku una show nao msanii wao ambae kipindi hicho ndo wanakuwa nae bega kwa bega ndo nae wanamwandalia show the same day, uki-cancel na wao Wana cancel na promotion za kutosha na ukifanya mchezo hata wadhamini wanaingizwa kwenye zengwe (hapa sasa kama huna kifua unatoka relini kumbe ulitakiwa ukomae na kipaji chako)
 
Changamoto ya wasanii wengi wa zamani ni ulaibu wa madawa ya kulevya pamoja na Bange

Otherwise wanavipaji vikubwa sana vya Muziki.

Kuna wakati nilitaka kuanzisha Mradi wa kufanya show na hao wasanii wa zamani as Wana nyimbo nyingi nzuri na bado Wana mashabiki wengi pia.

Bahati mbaya mambo hayakuniendea vizuri, ila baada ya Uchaguzi mwakani nitajaribu kufanya japo Kwa Mkoa mmoja uwe kama Pilot, biashara ikienda vizuri naweza kuendelea
Ukipata mdhamini wa kueleweka, utasepa na kijiji. Assume unabeba Wanaume TMK, Afande, Noorah, TID, Q Chief, Profesa, Wagosi nk, nani atakosa hiyo show?
 
Radio ni hizo tu? Matamasha wanaandaa wao tu? Think outside the box waachane na hii victim mentality.

Boss wa sinza pazuri alipofanyiwa figisu akafungua media yake mwenyewe. Hakuanza malalamiko all day. Badilika tokana na mazingira dunia haijawahi kumuonea mtu huruma.
Akitoa ngoma alikuwa anaziweka kwenye flash anazi-supply bodaboda na kwenye mabus ubungo stand, safarini nyimbo zao ni bandika bandua
 
Back
Top Bottom