TID anasikitisha sana, apewe msaada wa haraka

TID anasikitisha sana, apewe msaada wa haraka

Binafsi, nilibahatika kukutana na msanii wa kike wa kurap aliyewahi kutamba enzi hizo (jina nalisitiri), maana alihamia kwa muda jirani na nyumba niliyokuwa naishi last year. She is too talkative, na ni aina fulani ya watu ambao ni rahisi sana kuzoeana nao, so tulizoeana na nilifanikiwa kumuuliza masuala flani flani hivi kuhusu Muziki na wasanii...

Katika maelezo ya bidada huyu, alisema wasanii wengi wanatumia ngada. Wengi sana. Na alisema muda ukifika tutawaona dhahiri. Nikamuuliza kwani wewe hujawahi kushtua? Akakataa kata kata, akadai yeye ana vitu vyake tu, ila ngada anaiheshimu kupindukia, anaiogopa kama Ukoma!

Hakuishia hapo, alisema wengi pia ni waathirika wa HIV, na alinitajia mpaka majina (nayahifadhi), na akasema muda ukifika kila kigawe lazima kitaguswa. Alikuwa akisisitiza Muda tu. Kwamba kila kitu kitakuwa wazi muda ukifika!

Kuhusu TID pia nilimuuliza...Hakunijibu, lakini akasema 'Kinondoni haifai'.. Alinitolea mifano mingi na ushahidi mwingi kuhusu wasanii wa Kinondoni coz yeye mwenyewe alitokea huko. Alitaja historia na matukio. Aliwataja mpaka wanasiasa wakubwa na wafanyabiashara wakubwa wenye majina (huwezi kuamini) ambao wamechangia kwa kiwango kikubwa kuwaharibu wasanii..

Itoshe!

Ningetamani ufunguke zaidi....kufichaficha ni kutesana tu
 
Tatizo kuiga,Anajifanya Boby Brown wa bongo
Na pale kitaa kwao ngada ndio station.Bro wake mwenyewe nae ni mshiriki mkubwa kwenye hiyo biashara.
 
View attachment 225471

Mfano ni Chid Benz, dada wa watu kwa moyo wa msaada akamuomba amsaidie jamaa kutokana na hali aliyokuwa nayo but akaambulia matusi pamoja na kipigo kikali.

Dada wa watu bila hiyana akamsamehe maana na yeye kapitia huko na anajua watu wa hivi wasivyopenda kuambiwa ukweli.

Sasa hivi Chid yupo? Angalia muonekano wake kwa sasa, Na sasa hivi ana kesi ya kukutwa na kete wakati akisafiri kuelekea kwenye show Mtwara.

Mungu aliamua kumuumbua baada ya kumdhalilisha Ray C kwa kumpiga.

Amekuwa kama kibabu maskini,na wazazi wazae
 
ngada ni tatizo ,wasanii wanaiga huu upuuzi baada ya muda woote kwisha.tid ana saut nzur kama asingeingia kwenye matakataka haya angekuwa mbal sana
 
Mteja ni shoga wa pili, magari mengi bado hayajaanza kuwaka yakianza itakuwa mcharuko..madude siku hizi si ya mabongofleva peke yao ata mabongomuvi wamepokea kijiti. Tatizo la Mzee Warioba ni misosi anavunga misosi na vumbi bila misosi lazima utupambie magazeti. Na hasira zinamjia vipi maniga kibao wanakula madude alafu habari inakuwa mzee tu na watu wanawajua.

Mwana nimejaribu kurudia kusoma lakini chenga tupu!
 
Mr. Confident mimi nadhani huhitaji kuwa na wasi wasi. Hujataja jina la mtoa taarifa. Pili kutumia madawa hakuna siri kwani mwisho wa siku utadhihirika tu. Kwa kuwa ukianza kutumia madawa unakuwa dependent on ngada na unapoikosa unakuwa doro. Sasa hapo utaficha nini na mwili unajionyesha kabisa kwamba wewe ni teja?!!

Nakubaliana na huyo msanii aliyetoa taarifa hizo ni muda tu ndo utadhihirisha hayo yote.
 
Mifano tayari wameshaiona kwa wasanii wenzao (Langa, Ngwea na Mabovu) wote wamepotea kwa upuuzi huo lakini bado hawataki kujirekebisha. So waacheni wafe tu maana washashindikana
 
Mi nampongeza sana kwa matumizi ya madawa...na aendelee tu.shida ni pesa za serikal kupitia misafara ya jk kwenda kwenye mazishi ndio zinanisumbua.

"Elimu ni muhim sana sio lazima ikuwezeshe kupata ajira"
 
Haya madawa ni shida Ila Mungu atahukumu tu kama ss tutashindwa kuchukua hatua. Inaangamiza wengi sana na wengi wanaoangamia ni hawa nyota ambao wana kipato tayari hili ni janga kama biashara ya utumwa inaharibu nguvu kazi na rasilimali watu na fedha pia
 
Back
Top Bottom