TID: Huwa nahonga fedha ili muziki wangu upigwe redioni, watu wamenitenga isipokuwa Makonda

TID: Huwa nahonga fedha ili muziki wangu upigwe redioni, watu wamenitenga isipokuwa Makonda

Kuacha madawa kazi sana.
Mpuuzi tu huyu, watu wamemtenga kwa sababu kaacha madawa wa kulevya? Wote wamemtenga kwa sababu hiyo isipokuwa Makonda! Huu ni udhalilishaji kwa watanzania kwani anamaanisha asiyetumia madawa ya kulevya nchi hii ni Makonda tu? Maana huwezi kumchukia mvuta bangi wakati na wewe unavuta!!
 
La kuvunda halina ubani. Kama ubunifu umeshamtupa mkono ni vyema akae kando ili kuwapisha wengine asitafute visingizio visivyo na msingi. Je hebu tujiulize kama ni kweli huwa wanahongwa mbona hatujasikia mtangazaji aliyekamatwa na PCCB? Mtu kama TID hawezi kushindwa kuwakamata Madj wapenda rushwa. Mbona alipotamba na ZEZE hatukusikia hizo habari? Hivi anataka kutueleza kwamba Darassa alihonga ili kupaisha ule wimbo wa Muziki?
 
vipi diamond ambaye ni mlezi wake????? tafakari acha chuki,

Diamond ana mizizi na singi mkubwa wa mashabiki, japo hili la Bashite limemyumbisha kidogo kwa mashabiki kugawanyika ,japo kazi zake zinapigwa kama kawaida.

Yaani upendo wa mashabiki kwake umepungua nikiambiwa nieleze kwa mstari mmoja

Pia anabebwa na uteam , sasa TID hana team ya kumbeba akitikiswa kidogo tu kilioooo.


Kimavi cha Bashite kimewakuta pia Bongo movie wanajutaaa ,haqasikilizwi na mashabiki wanakula matusi tu
 
'Huwa nahonga' kumbe tatizo ni wewe mwenyewe, sasa unamlaumu nani?

Tengeneza pini kali uone kama haijawa kinyume chake (vice versa)

Hebu cheki na darasa akwambie yeye anahonga kiasi gani, kwani ile ngoma yake imechezwa mpaka inakuwa kufuru.

Sasa kama unaendesha gari la mkaa utaacha kubeba 'kikomboleo' na bararabarani jamaa wapo? hebu endesha Range Rover Vogue latest uone utakavyotesa barabarani....yaani badala ya kupigwa mkono wewe utakuwa unapewa tano kila ukiwakuta wazee.
 
Sio ajabu, mi mwenyewe kaka yangu anatumia madawa ya kulevya familia nzima inaonekana tumemtenga japo ukweli ni kwamba yy ndio kajitenga kutokana na mambo yake ya ajabuajabu
 
Nilikua fan mkubwa sana wa TID, kipindi anatoa album ya kwanza ya Sauti ya Gharama nilijua fika atakuwa international musician.. ila alijipoteza mwenyewe... anachotakwa sasa apumzike muziki wa majukwaani, ajipange kiafya na muda huo arecord nyimbo. Then aanze upya-rebranding..after one year arudi upya na haya mambo ya bashite yatakua yameisha
 
Back
Top Bottom