TID ni aina ya watu ambao kwenye jamii inapaswa tuwe nao makini sana

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Katika jamii yoyote ile ya watu, kuna baadhi ya watu ambao ni mabingwa wa kung'ata na kupuliza , akiwa na wewe atakusifia na kukupa kila aina ya sifa na kujifanya ni mwema sana kwako na kuwaponda vibaya mno wale ambao wapo kinyume na wewe ila ukimpa kisogo tu kibao kinageuka kwako wewe sasa ndo atakuongelea vibaya na wale aliokuwa anawaponda ataenda kuwapelekea umbea na kukuponda wewe.

Sasa huyu jamaa anayejiita Top In Dar au ukipenda muite mzee kigogo ,Warioba, mzee wa kuganda hewani , mzee wa inakuja inakata ni dizaini ya hao watu.

T.I.D anajua sana kumpaka mtu mafuta kwa mgongo wa chupa ila sasa ukimpa kisogo tu utapondwa ile mbaya.

Mfano mzuri ni kuhusu ushindani uliopo kati ya Wasafi/Diamond Platnumz na Clouds Media jamaa akiwa kwa Diamond anamsifia kinoma na kumpa kila aina ya sifa , akienda Clouds inakuwa kinyume chake anasifia sana Clouds na kumponda mbaya Diamond Platnumz.

T.I.D aligombana mpaka na swahiba wake wa kitambo QChillah kutokana na tabia hii hii ya majungu na ufitini sasa sijajua kukaa kinondoni kumemfanya kuwa na tabia hizi, maana kinondoni kunaongoza kuwa na watu wanafiki wanafiki.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
KwahiYo Na wao wanaiga.... Halafu bado wanakataa uwezo walionao clouds katika ubunifu
Watakwambia hakuna kipya chini ya jua. Clouds ni sawa na azam halafu wasafi ni akina Mo kila zao la azam wanaiga
Hahahaha

Nakumbuka ya Clouds ,Dar mpk Moro ,Kisaki ,train ya Tazara

MTC | 101| [emoji769]
 
Kwaiyo ingekua ww ndio Diamond ,kigoma ungeenda kwa pipa sio mkuu? Hebu tupeni ubunifu ukiacha kwenda na Train sehem kama kigoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha Pro WCB __Bhana. So hizi siku zote alizokuwa anakwenda na ndege ilikuwaje... Kwanini hakuanza yeye kwenda na train mpaka asubiri clouds wafanye

Simchukii diamond na appreciate hustle zake.. But truth must be told clouds wapo vizuri Mano kwenye ubunifu
 
Kwaiyo siku zote hizo alikua anaenda kutimiza miaka miangapi? Hivi unajua uzito na maana ya hili tukio?

Relax team kiba...punguza negativity utaishi sana bila stress [emoji2][emoji2]

Am out mkuu...
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwaiyo siku zote hizo alikua anaenda kutimiza miaka miangapi? Hivi unajua uzito na maana ya hili tukio?

Relax team kiba...punguza negativity utaishi sana bila stress [emoji2][emoji2]

Am out mkuu...

Sent using Jamii Forums mobile app
Imagine... Nimeshakuwa team kiba πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ my foot.. Usiku mwema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…