Tido anahama TBC anakwenda kwa Lowassa

inaweza ikawa ni uzushi hii habari.

Hayo ya kufanya kazi yeyote mahala popote ni kwa watu ambao wanatafuta kula au ujuzi/uzoefu.

Ukiwa na hadhi ya Tido lazima uchague unafanya nini na wapi.Hatafuti kula yule. Kwa miaka yote hiyo na nyadhifa zote hizo alishajijenga. Kumfanyia kazi lowasa na si umma haiwezi ikawa ndoto yake.
 
Ni kweli wadau, nimehakikishiwa kuwa Tido anaondoka TBC kwa kuwa umri wake wa kustaafu umefika na nimedokezwa kuwa amekataa Mkataba mwingine.
 
Kuna siku mtazamaji mmoja aliuliza Juma Nkamia yupo wapi? jibu la Marin Hassan lilinishangaza sana kwani alijibu yeye hawezi kujibu, management ndio inaweza kujibu.

Eti jamani naye Nkamia kaondoka/kafukuzwa au Marin alinogesha tu, maana najua ana bifu kali sana na Nkamia
 

nkamia yuko VOA-voice of america nahisi ana mkataba mzuri huko.
 
Tido is not a public servant no does he hold any public office. Ana weza kuhamia popote anapo taka kwa sababu zozote zile alizo nazo. When it comes to a career one chooses the path he/she thinks will suit him/her best. Muache aende. Akifanikiwa au kushindwa huko itakua juu yake.
 

GT; huyo jamaa kwenye avatar yako amefanana sana na Tido mwenyewe...Teh teh teh!
 
Mkataba wake ukiisha atakuwa na umri wa miaka 64. Umri wa kustaafu kwa WaTZ ni miaka 60 kwa lazima. Jamani mwenzenu akagange njaa wapi ili amalizie maisha yake ??? Yeye ni mtu wa Media, hajui aina nyingine ya ujasiria mali, sasa ataishi vipi ?? Basi msaidieni kumtafutia media house nyingine apart from Lowassa TV and Radio Ltd.
 
nkamia yuko VOA-voice of america nahisi ana mkataba mzuri huko.

Na yule dada aitwaye Grace Chingalambe yuko wapi siku izi, make hakuaga na pete, au kachukuliwa jumla na jamaa kamkataza kutangaza?
 
Jamani mkubwa mamvi mbona unaendelea kutuumiza..........
 
Shida hapo wana JF ni nini? Mbona ni kitu cha kawaida mtu baada ya kustaafu unatafuta pa kupotozea muda na angalau kutop off pension? Je Tido angehamia ITV, Star Tv, au yeyote ungeleta mada? Kwa kuwa anahamia kwa Lowassa ndio iwe issue sio? Leteni hoja za maana na sio umbea wa kike hapa.
 
 
Lazima kuhamia kwa Lowassa iwe issue kwa sababu huyu Lowassa anatuhumiwa kuihujumu nchi na alijiuzulu uwaziri mkuu kwa sababu hiyo!
 
I don't see the reason to discuss the life carreer of Tido Mhando hapa. Kila mtu anachagua anapopaona panamfaa kufanya kazi either kimaslahi na mazingira mazuri ya kazi pia. Kuhama kwake hakutapunguza chochote TBC kwani wapo wataoziba nafasi hiyo.
 
Money money money! Habari corporation iliuzwa; nini Tido, mwache aende
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…