Tido Mhando: Kuna Haja Gani ya kufanya Kipindi Cha Michezo Saa Sita Kwa Siku

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933

View: https://www.instagram.com/reel/DY0O1QAIDfv/?igsh=MTV3MnRxaTQwdXNxOA==
Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Bw. Tido Mhando, amewataka Waandishi wa Habari nchini kutafakari upya wajibu wao katika kuijenga jamii kupitia maudhui yenye tija, akieleza kuwa ipo haja ya kurejesha hadhi na nguvu ya taaluma hiyo katika kujenga fikra na maendeleo ya taifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Bw. Mhando amesema pamoja na JAB kusimamia utoaji wa ithibati kwa kuzingatia vigezo vya elimu na sheria, bado kuna umuhimu wa Waandishi wa Habari kuendelea kujengewa uwezo kupitia mafunzo ya kitaaluma.

“Tukitazama baadhi ya vyombo vyetu vya habari, iwe ni magazeti, redio au televisheni, mambo ya kufikirisha kwa kiasi kikubwa yamepungua. Waandishi wa Habari wanapaswa kutafakari kama hiyo ndiyo taswira wanayotaka kuiacha katika jamii ya Watanzania,” amesema.

Amesisitiza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuunda mtazamo wa jamii, hivyo kuna wajibu wa kuhakikisha maudhui yanayotolewa yanajenga uelewa, yanakuza maendeleo na yanalinda maslahi ya taifa.

“Tunachosimamia ni kuhakikisha Mwandishi wa Habari anayepata ithibati anakuwa na kiwango cha elimu kisichopungua Diploma, lakini tunataka pia Waandishi wa Habari waendelee kupata mafunzo ili waweze kuimarika zaidi kitaaluma,” amesema.

Amesema kuna haja ya sekta ya habari kutafakari aina ya maudhui yanayopewa kipaumbele, akisisitiza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kujenga fikra na mwelekeo wa jamii.
Source tumaini media
 
Anyway, bado sio kesi hata ikiwa n saa 20 kwa siku.

Kuna baadhi ya channel n za sports tuu, Sasa mnataka waweke nn tofauti na sports?

Huyo mzee c alikuwa CEO wa Azam, mbona kusema wasionyeshe michezo saa 24 hata kama channel yao n ya michezo tuu.?
Aliogopa kusema ukweli ili asikose kupewa iyskrimu ya bure na bakhresa.
 
Anyway, bado sio kesi hata ikiwa n saa 20 kwa siku.

Kuna baadhi ya channel n za sports tuu, Sasa mnataka waweke nn tofauti na sports?

Huyo mzee c alikuwa CEO wa Azam, mbona kusema wasionyeshe michezo saa 24 hata kama channel yao n ya michezo tuu.?
Kuna Watanzania washamba sana.

Hawajui channel za michezo 24 hours?
 
Kuna Watanzania washamba sana.

Hawajui channel za michezo 24 hours?
Angeanza na Azam alipokuwa CEO hapo, angewaambia wapige na siasa.

Na bado anaweza kuwaambia mana c n mwenyekiti wa bodi ithibati, afanye hvy tuone nguvu yake kama mwenyekiti
 
Hapana, kuna point nawakubali.

Watangazaji wengi walikuwa wapiga kelele na hana elimu, afadhali tumeondolewa noise pollution
Tatizo lenu Watanzania wengi mnaangalia matatizo kinyumenyume.

Badala ya kuongeza elimu kwa wananchi ili wakatae waandishi wajinga, mnawapa watu wa ithibati kazi ya kuwafikiria wananchi kwa niaba yao.

Ukishaipa kamati kazi ya kufikiria kwa niaba ya wananchi ushaharibu hapo.

Ndiyo mwanzo wa mambo ya George Orwell 1984 hapo.

Mtapigwa censorship na kuikubali tu kama kitu muhimu.
 
Ujinga wa JAB niliishaukataa, hauna tija kwa waandishi chipukizi
 
View: https://www.instagram.com/reel/DY0O1QAIDfv/?igsh=MTV3MnRxaTQwdXNxOA==
Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Bw. Tido Mhando, amewataka Waandishi wa Habari nchini kutafakari upya wajibu wao katika kuijenga jamii kupitia maudhui yenye tija, akieleza kuwa ipo haja ya kurejesha hadhi na nguvu ya taaluma hiyo katika kujenga fikra na maendeleo ya taifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Bw. Mhando amesema pamoja na JAB kusimamia utoaji wa ithibati kwa kuzingatia vigezo vya elimu na sheria, bado kuna umuhimu wa Waandishi wa Habari kuendelea kujengewa uwezo kupitia mafunzo ya kitaaluma.

“Tukitazama baadhi ya vyombo vyetu vya habari, iwe ni magazeti, redio au televisheni, mambo ya kufikirisha kwa kiasi kikubwa yamepungua. Waandishi wa Habari wanapaswa kutafakari kama hiyo ndiyo taswira wanayotaka kuiacha katika jamii ya Watanzania,” amesema.

Amesisitiza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuunda mtazamo wa jamii, hivyo kuna wajibu wa kuhakikisha maudhui yanayotolewa yanajenga uelewa, yanakuza maendeleo na yanalinda maslahi ya taifa.

“Tunachosimamia ni kuhakikisha Mwandishi wa Habari anayepata ithibati anakuwa na kiwango cha elimu kisichopungua Diploma, lakini tunataka pia Waandishi wa Habari waendelee kupata mafunzo ili waweze kuimarika zaidi kitaaluma,” amesema.

Amesema kuna haja ya sekta ya habari kutafakari aina ya maudhui yanayopewa kipaumbele, akisisitiza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kujenga fikra na mwelekeo wa jamii.
Source tumaini media

Mnataka kuzipangia TV/Radio stations kipindi? Mtawasaidia kulipa kodi na mishahara ya wafanyakazi wao?
 
Mfumo ndiyo unataka hivyo
Watu wakijadili mambo ya siasa nk wanajuwa nini wanachokutana nacho
Huyo tido asijifanye haijuwi
Hali halisi wanayokutana nayo waandishi na watangazaji

Ova
 
Back
Top Bottom