Tigo na Vodacom achaneni na tabia hizi or otherwise mtoe posho kwa wateja wenu

Trainee

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
2,660
Reaction score
3,501
Unawapa taarifa ya mtandao kusuasua wanalazimisha kukuelekeza settings za simu usipokuwa makini wanajidai wameshasolve tatizo na wanakukatia simu

Kwa yule ambaye yupo makini anawabananisha wanakosa hoja basi wanaanza kuuliza maswali kibao yasiyo na kichwa. Eti mteja anaulizwa kama tatizo hilo linakwepo hata akihama eneo alilopo sasa mmeniajiri mpaka mnipe hiyo kazi ya kusurvey!
 
Mkuu, ukiona hivyo ujue unawasiliana na mtu ambaye hana uwezo wa kushughulikia tatizo lako.

Hivi umewahi kujiuliza ni akina nani hasa hao walioajiriwa kutatua changamoto za kimtandao - CV zao zikoje?

Unadhani ni wabobevu fulani wa masuala ya kiufundi yahusuyo mtandao au tu ni maprofeshono waongeaji wa kuwapooza wateja - almaarufu kama customer care?
 
Kama vile ulikuwepo wakati nachapana nao maswali muda sio mrefu ndugu yangu.

Hizi kampuni zinahitaji sheria yakuwa wanawajibishwa kwa mafaini ndio watajirekebisha.

Kuna kamtandao ka1 ikifika jioni huduma ya pesa kipengele hadi kaamue kenyewe na mawingu au mvua ikiwepo ndio omba bahati.
 
Hua namind sana napiga simu alafu naambiws niangalie settings kwa jambo ambalo halina settings kwenye simu
 
Unawapa taarifa ya mtandao kusuasua wanalazimisha kukuelekeza settings za simu usipokuwa makini wanajidai wameshasolve tatizo na wanakukatia simu

Kwa yule ambaye yupo makini anawabananisha wanakosa hoja basi wanaanza kuuliza maswali kibao yasiyo na kichwa. Eti mteja anaulizwa kama tatizo hilo linakwepo hata akihama eneo alilopo sasa mmeniajiri mpaka mnipe hiyo kazi ya kusurvey!
ulitegemea labda utajibiwaje, inaonekana tayar ulikuwa na majibu
 
Mkuu, ukiona hivyo ujue unawasiliana na mtu ambaye hana uwezo wa kushughulikia tatizo lako.

Hivi umewahi kujiuliza ni akina nani hasa hao walioajiriwa kutatua changamoto za kimtandao - CV zao zikoje?

Unadhani ni wabobevu fulani wa masuala ya kiufundi yahusuyo mtandao au tu ni maprofeshono waongeaji wa kuwapooza wateja - almaarufu kama customer care?
Na hii ndiyo hasa hata mimi naona hivyo
Maana hata juzi yametokea kwa TANESCO nimepiga huduma kwa wateja ya wilayani wananilazimisha kufanya kitu ambacho mimi nimeshajaribu kabla na ikashindikana mwisho wananiambia ujinga ujinga nikajiongeza nikapiga makao makuu kumbe ni ishu ndogo tu nikaambiwa shida ni nini na wakatumiwa taarifa zangu kwenye mifumo yao huko warekebishe basi wakanipigia kwa upole hadi nikaona huruma tena

Nikaona kumbe kuna maeneo wanaajiriwa watu ambao ni watupu kichwani kiasi kwamba hata kutraki taarifa za mteja kwenye mfumo mtu hawezi
 
Back
Top Bottom