tiGO wajitenga na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Lissu. Wasema mmiliki wa sasa ni mwingine si yule wa nyakati za shambulio!

Kampuni ya TIGO imesema haihusiki na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Antipas Lisu

HONORA imesema kampuni mama ya Tigo haikuwa mmiliki Wakati Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Antipas Lisu anashambuliwa
----
Dar es Salaam. Kampuni ya Honora Tanzania Public Limited Company ("TIGO") imejitenga na taarifa za kuvujisha taarifa za simu za Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu, ikisema kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa.

Taarifa hiyo inatokana na kesi inayoendelea nchini Uingereza kati ya Kampuni ya Millicom iliyokuwa ikimiliki Tigo na aliyekuwa mfanyakazi wake, Michael Clifford ambaye sasa amefukuzwa kazi.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Guardian la Uingereza la Septemba 24, 2024, Clifford aliwasilisha maelezo yake katika mahakama ya London kuwa, chanzo cha kufukuzwa kwake ni kutoa ripoti ya jinsi kampuni hiyo ilivyotoa taarifa za mawasiliano ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu.

Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa kwenye gari lake alipokuwa akielekea kwenye makazi yake baada ya kuhudhuria vikao vya Bunge jijini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa la Honora Tanzania Public Limited Company leo Septemba 26, 2024 imeleza kutambua taarifa ya kesi inayoendelea nchini Uingereza ya ajira katika mahakama ya London inayomhusisha mfanyakazi wa zamani wa Millicom, kampuni mama ya Tigo hadi mwaka 2022.

“Kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa lilipotokea,” imesema taarifa hiyo.

Imesema japo hawawezi kutoa maoni kuhusu undani wa kesi hiyo kwa kuwa hawahusiki moja kwa moja, bali wanahakikisha ulinzi wa taarifa za wateja wao.

“Tunataka kuwahakikishia wateja wetu na wadau wetu kwamba kulinda data zao binafsi kwa kuzingatia sheria na kanuni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado ni kipaumbele chetu kikuu,” imesema taarifa hiyo.”

Chanzo: Mwananchi
Kenge kabisa, imebadirika jina tu, ila wafanyakazi ni walewale, data centre ni zile zile, hata chip zao ni zile zile, data zilitoka kwenye mitambo Yao zikaenda serikalini,
 
Millicom, kampuni mama ya Tigo hadi mwaka 2022.
Kesi ilifunguliwa 2019.
Kwa hiyo wakati hao HONORA wanaingia huo mkenge 2022, kesi ilikuwa tayari inaendelea kurindima.

Ukinunua, kupewa au kurithi kampuni, unabeba "Assets + Liabilities".

Ni kama ukinunua gari, nyumba, kiwanja au shamba lenye kesi, unakuwa umenunua hiyo mali pamoja na kesi husika.

Waambie watulie tu, hawawezi kuchomoka kwa huo utetezi dhaifu.
 
Tatizo linapokuja ni kwamba inakuwa ngumu kuishitaki Tigo kwasababu zifuatazo:

Taarifa za Lissu zilivuja kipindi ambacho kampuni mama iliyomiliki Tigo ni "Millicom International Cellular public limited company"

Mwaka 2022 hadi sasa kampuni mama mmiliki wa Tigo ni "Honora Tanzania Public Limited company"

Ni sawa na kushambuliwa na jirani, akihama nyumba ni ngumu kuishtaki nyumba yenye jirani mpya,
Nyumba ile ile imebadilishwa bato tu
 
Bado brand ni ileile hivyo mahakama itachambua vipengele vya kisheria
 
Kampuni ya TIGO imesema haihusiki na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Antipas Lisu

HONORA imesema kampuni mama ya Tigo haikuwa mmiliki Wakati Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Antipas Lisu anashambuliwa
----
Dar es Salaam. Kampuni ya Honora Tanzania Public Limited Company ("TIGO") imejitenga na taarifa za kuvujisha taarifa za simu za Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu, ikisema kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa.

Taarifa hiyo inatokana na kesi inayoendelea nchini Uingereza kati ya Kampuni ya Millicom iliyokuwa ikimiliki Tigo na aliyekuwa mfanyakazi wake, Michael Clifford ambaye sasa amefukuzwa kazi.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Guardian la Uingereza la Septemba 24, 2024, Clifford aliwasilisha maelezo yake katika mahakama ya London kuwa, chanzo cha kufukuzwa kwake ni kutoa ripoti ya jinsi kampuni hiyo ilivyotoa taarifa za mawasiliano ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu.

Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa kwenye gari lake alipokuwa akielekea kwenye makazi yake baada ya kuhudhuria vikao vya Bunge jijini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa la Honora Tanzania Public Limited Company leo Septemba 26, 2024 imeleza kutambua taarifa ya kesi inayoendelea nchini Uingereza ya ajira katika mahakama ya London inayomhusisha mfanyakazi wa zamani wa Millicom, kampuni mama ya Tigo hadi mwaka 2022.

“Kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa lilipotokea,” imesema taarifa hiyo.

Imesema japo hawawezi kutoa maoni kuhusu undani wa kesi hiyo kwa kuwa hawahusiki moja kwa moja, bali wanahakikisha ulinzi wa taarifa za wateja wao.

“Tunataka kuwahakikishia wateja wetu na wadau wetu kwamba kulinda data zao binafsi kwa kuzingatia sheria na kanuni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado ni kipaumbele chetu kikuu,” imesema taarifa hiyo.”

Chanzo: Mwananchi
hawa Tigo ni WAPUMBAFU SANA... mmliki mpya huwa analitithi mambo yote ikiwemo wafanyakazi na nyaraka. Waache uzwazwa... wamenichafua sana moyo wangu... utetezi hafifu... sasa ya nini walikuwa wanataka mambo yao yawe kisiri?
Wasome hizi kesi mbili kwanza ndio waje wakanushe uupuuzi wao.
 
Attachments

Tatizo linapokuja ni kwamba inakuwa ngumu kuishitaki Tigo kwasababu zifuatazo:

Taarifa za Lissu zilivuja kipindi ambacho kampuni mama iliyomiliki Tigo ni "Millicom International Cellular public limited company"

Mwaka 2022 hadi sasa kampuni mama mmiliki wa Tigo ni "Honora Tanzania Public Limited company"

Ni sawa na kushambuliwa na jirani, akihama nyumba ni ngumu kuishtaki nyumba yenye jirani mpya,
Bado brand ni ileile hivyo mahakama itachambua vipengele vya kisheria
Tigo sio kampuni. Ni jina tu limekaa mbele
Ni brand name ambayo imesajiliwa kisheria
 
Tatizo linapokuja ni kwamba inakuwa ngumu kuishitaki Tigo kwasababu zifuatazo:

Taarifa za Lissu zilivuja kipindi ambacho kampuni mama iliyomiliki Tigo ni "Millicom International Cellular public limited company"

Mwaka 2022 hadi sasa kampuni mama mmiliki wa Tigo ni "Honora Tanzania Public Limited company"

Ni sawa na kushambuliwa na jirani, akihama nyumba ni ngumu kuishtaki nyumba yenye jirani mpya,
Vipi kama ingekuwa ni deni wanalipwa baada ya kubadilisha mmiliki wangekataa malipo????
Hapo bado hakuna ulichoandika yaani bado tigo Wana kesi ya kujibu
 
Tatizo linapokuja ni kwamba inakuwa ngumu kuishitaki Tigo kwasababu zifuatazo:

Taarifa za Lissu zilivuja kipindi ambacho kampuni mama iliyomiliki Tigo ni "Millicom International Cellular public limited company"

Mwaka 2022 hadi sasa kampuni mama mmiliki wa Tigo ni "Honora Tanzania Public Limited company"

Ni sawa na kushambuliwa na jirani, akihama nyumba ni ngumu kuishtaki nyumba yenye jirani mpya,
Iloyotoa hizo taarifa ni kampuni ya Tigo, siyo kampuni mama.
 
Kwamba mwanamke aliye kwenye ndoa kama ana kesi mahakamani ikitokea ameachwa na mume wake na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine makosa yake yanafutika?
Yafutike wapi? mume mpya lazima awe makini...sio kurukia rukia wake za watu na makandokando yao...
Hawa Tigo wamezua swali jingine, tuone kama wana due diligence waliyofanyiwa kabla ya kununuliwa tuone kwamba hakuna hizo taarifa za kuvuja. kesi ya London imeanika mambo mengi hadi majina ya watu muhimu ukizisoma zote mbili hapa.
 
Attachments

2019 kesi ikaanzishwa. Muda utaongea tu

Back
Top Bottom