tiGO wajitenga na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Lissu. Wasema mmiliki wa sasa ni mwingine si yule wa nyakati za shambulio!

Tatizo linapokuja ni kwamba inakuwa ngumu kuishitaki Tigo kwasababu zifuatazo:

Taarifa za Lissu zilivuja kipindi ambacho kampuni mama iliyomiliki Tigo ni "Millicom International Cellular public limited company"

Mwaka 2022 hadi sasa kampuni mama mmiliki wa Tigo ni "Honora Tanzania Public Limited company"

Ni sawa na kushambuliwa na jirani, akihama nyumba ni ngumu kuishtaki nyumba yenye jirani mpya,
Huna uelewa wa sheria
 
Je, kampuni ya simu ikiuzwa manunuzi ananunua ikiwa na taarifa zake zote za wateja wa zamani au anaanza upya kwa kudelete taarifa zote za awali?
Je, ukinunua shamba lina bangi utaweza kujitoa kirahisi kwa kusema bangi nimeikuta imeshakomaa tayari?
Kampuni itakapouzwa kufidia madhila ya Lissu ndipo wataanza kusakana
 
Tatizo linapokuja ni kwamba inakuwa ngumu kuishitaki Tigo kwasababu zifuatazo:

Taarifa za Lissu zilivuja kipindi ambacho kampuni mama iliyomiliki Tigo ni "Millicom International Cellular public limited company"

Mwaka 2022 hadi sasa kampuni mama mmiliki wa Tigo ni "Honora Tanzania Public Limited company"

Ni sawa na kushambuliwa na jirani, akihama nyumba ni ngumu kuishtaki nyumba yenye jirani mpya,
Kumbuka kampuni ni going concern, it can be sued, or it can sue. Kama kuna mteja au staff aliibia kampuni kipindi kile hawezi kushtakiwa sasa hivi?!
 
Hivi nikikopa salio katika mtandao wa simu ikiwa inamilikiwa na mtu X alafu baadae umiliki ukahamia mtu Y nikiwa bado sijalipa deni,je, nikiweka vocha hilo deni litakatwa au halitakatwa kwa sababu mmiliki kabadilika!?
 
Kampuni ya TIGO imesema haihusiki na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Antipas Lisu

HONORA imesema kampuni mama ya Tigo haikuwa mmiliki Wakati Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Antipas Lisu anashambuliwa
----
Dar es Salaam. Kampuni ya Honora Tanzania Public Limited Company ("TIGO") imejitenga na taarifa za kuvujisha taarifa za simu za Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu, ikisema kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa.

Taarifa hiyo inatokana na kesi inayoendelea nchini Uingereza kati ya Kampuni ya Millicom iliyokuwa ikimiliki Tigo na aliyekuwa mfanyakazi wake, Michael Clifford ambaye sasa amefukuzwa kazi.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Guardian la Uingereza la Septemba 24, 2024, Clifford aliwasilisha maelezo yake katika mahakama ya London kuwa, chanzo cha kufukuzwa kwake ni kutoa ripoti ya jinsi kampuni hiyo ilivyotoa taarifa za mawasiliano ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu.

Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa kwenye gari lake alipokuwa akielekea kwenye makazi yake baada ya kuhudhuria vikao vya Bunge jijini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa la Honora Tanzania Public Limited Company leo Septemba 26, 2024 imeleza kutambua taarifa ya kesi inayoendelea nchini Uingereza ya ajira katika mahakama ya London inayomhusisha mfanyakazi wa zamani wa Millicom, kampuni mama ya Tigo hadi mwaka 2022.

“Kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa lilipotokea,” imesema taarifa hiyo.

Imesema japo hawawezi kutoa maoni kuhusu undani wa kesi hiyo kwa kuwa hawahusiki moja kwa moja, bali wanahakikisha ulinzi wa taarifa za wateja wao.

“Tunataka kuwahakikishia wateja wetu na wadau wetu kwamba kulinda data zao binafsi kwa kuzingatia sheria na kanuni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado ni kipaumbele chetu kikuu,” imesema taarifa hiyo.”

Chanzo: Mwananchi
Hiyo inawahusu tuu, mradi ni kampuni ya Tigo!
 
Lissu, Lissu
Tigo ilishauzwa kitambo kama haujui ,
Mmiliki mpya wa Tigo na zantel ni Rostam Abdulasul Aziz ambae hahusiki na lolote lile ,
Sasa bwana lissu ataishtaki kampuni hewa ambayo haipo
Kama lissu alikua anategemea mabilioni ya serikali ajue keshakosa muda mrefu.
Lissu ajue kabisa , kwake na amsterdam wake sio ushindi bali ni maumivu,
Tigo hawahusiki na shambulio lake kwa namna yoyote ile ,
Rostam alikwaa umiliki wa hizo kampuni baada ya kuuza hisa zake za Vodacom miaka ya magufuli,
Lissu bye bye
 
Tatizo linapokuja ni kwamba inakuwa ngumu kuishitaki Tigo kwasababu zifuatazo:

Taarifa za Lissu zilivuja kipindi ambacho kampuni mama iliyomiliki Tigo ni "Millicom International Cellular public limited company"

Mwaka 2022 hadi sasa kampuni mama mmiliki wa Tigo ni "Honora Tanzania Public Limited company"

Ni sawa na kushambuliwa na jirani, akihama nyumba ni ngumu kuishtaki nyumba yenye jirani mpya,
Hilo kisheria halipo mkuu,Tigo ni Tigo sawa sawa na ukinunua nyumba yenye kaburi!
 
Tatizo linapokuja ni kwamba inakuwa ngumu kuishitaki Tigo kwasababu zifuatazo:

Taarifa za Lissu zilivuja kipindi ambacho kampuni mama iliyomiliki Tigo ni "Millicom International Cellular public limited company"

Mwaka 2022 hadi sasa kampuni mama mmiliki wa Tigo ni "Honora Tanzania Public Limited company"

Ni sawa na kushambuliwa na jirani, akihama nyumba ni ngumu kuishtaki nyumba yenye jirani mpya,
Hujui sheria hata corporate law hujui bora utulie usome maoni ya wengine usilete maoni ya kingumbaru.
 
Kampuni ya TIGO imesema haihusiki na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Antipas Lisu

HONORA imesema kampuni mama ya Tigo haikuwa mmiliki Wakati Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Antipas Lisu anashambuliwa
----
Dar es Salaam. Kampuni ya Honora Tanzania Public Limited Company ("TIGO") imejitenga na taarifa za kuvujisha taarifa za simu za Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu, ikisema kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa.

Taarifa hiyo inatokana na kesi inayoendelea nchini Uingereza kati ya Kampuni ya Millicom iliyokuwa ikimiliki Tigo na aliyekuwa mfanyakazi wake, Michael Clifford ambaye sasa amefukuzwa kazi.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Guardian la Uingereza la Septemba 24, 2024, Clifford aliwasilisha maelezo yake katika mahakama ya London kuwa, chanzo cha kufukuzwa kwake ni kutoa ripoti ya jinsi kampuni hiyo ilivyotoa taarifa za mawasiliano ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu.

Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa kwenye gari lake alipokuwa akielekea kwenye makazi yake baada ya kuhudhuria vikao vya Bunge jijini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa la Honora Tanzania Public Limited Company leo Septemba 26, 2024 imeleza kutambua taarifa ya kesi inayoendelea nchini Uingereza ya ajira katika mahakama ya London inayomhusisha mfanyakazi wa zamani wa Millicom, kampuni mama ya Tigo hadi mwaka 2022.

“Kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa lilipotokea,” imesema taarifa hiyo.

Imesema japo hawawezi kutoa maoni kuhusu undani wa kesi hiyo kwa kuwa hawahusiki moja kwa moja, bali wanahakikisha ulinzi wa taarifa za wateja wao.

“Tunataka kuwahakikishia wateja wetu na wadau wetu kwamba kulinda data zao binafsi kwa kuzingatia sheria na kanuni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado ni kipaumbele chetu kikuu,” imesema taarifa hiyo.”

Chanzo: Mwananchi
Ukinunua mzigo kampuni ambayo ni limited liability

Unakuwa responsible na makandokando yake yotee

Madeni,staff,mifumo and everything

So wasijitoe ufahamuu

Lazima Mh Lissu avune makubwa kwao na watalipaa au watafungiwa mifumo hadi wamlipe Mh kwa fidia atakayo amua na mwanasheria wake
 
Back
Top Bottom