Tigo wameniibia pesa: Naomba uzoefu wenu kupambana na wizi huu

robinson crusoe

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2020
Posts
762
Reaction score
1,236
Leo ni siku kadhaa nikipambana na wizi wa pesa niliyokuwa nayo ndani ya tigopesa. Huduma kwa wateja wameleta hadithi tofauti za aina tatu zote nimekataa. Walianza na kusema zimerudi benki, benki imesema haina ujinga huo.

Wakasema zitarudi baada ya masaa 24 bado hazikurudi. Mwisho wanasema nilikopa wamerudisha mkopo wao, nimekataa sijawahi na sitawahi kukopa tigo. Naona wanajikanyaga tu!

Niongozeni nipambane nao na mara hii natamani mawasiliano na vijana wa Law school ili nipate fidia ya kutosha kutokana na upuuzi huu.
 
Leo ni siku kadhaa nikipambana na wizi wa pesa niliyokuwa nayo ndani ya tigopesa. Huduma kwa wateja wameleta hadithi tofauti za aina tatu zote nimekataa. Walianza na kusema zimerudi benki, benki imesema haina ujinga huo. wakasema zitarudi baada ya masaa 24 bado hazikurudi. Mwisho wanasema nilikopa wamerudisha mkopo wao, nimekataa sijawahi na sitawahi kukopa tigo. Naona wanajikanyaga tu!

Kawasomee albadri
 
Pambania haki yako mkuu. Wapeleke mahakamani. Utapata fidia ya usumbufu.
 
Pole mkuu nenda mahakamani fungua kesi ya madai, wamekupiga kiasi gan kwani?
 
Ilikuwa kiasi gani, na ulitoa kutoka wapi kwenda wapi? Jibu hayo maswali, tuweze kukushauri
Pesa nilihamisha CRDB kwenda tigo. Nikatumia kidogo zikabaki laki 1 na elfu chache, jamaa wakazinyakua. Bahati nzuri nami nimewarekodi ktk mazungumzo yangu na wao kama mara mbili hivi! Sasa naamini nimewashawishi inatosha. naona hawataki kurudisha au wanaleta kuteteana wizi wao. Hadi nimeshaona milioni kadhaa za madai ya usumbufu na personality yangu zinakuja.
 
Kama pesa ilitoka bank na kuja kwenye tigo bila kasoro hakuna shida.

Nenda tigo shop, omba wakupatie 'statement' ya miamala yako ndani ya kipindi hicho pesa ilipopotea.

Muamala ambao huutambui, omba ufafanuzi; ikishindikana, waandikie barua ya kwanza, unataka urudishiwe fedha zako kwa sababu huo muamala huutambui. Barua utaielekeza kwa mtendaji mkuu wa kampuni, na tuma kwa njia ya email ukiambatanisha na 'statement'.​
 
Angalia watu wako wa karibu ukute ndo wamekuliza
Hakuna hilo boss! Si nakwambia jamaa hawa wameanza kubabaika. Mara naambiwa zilirudi benki. Benki imesema haina uhusiano huo na tigo maana kama benki inanidai ingechana kwenye akaunti yangu. baadaye nasingiziwa mikopo ya tigo, kitu ambacho sijawahi kuwazia. Uzuri nimerekodi bhla!-bhla! zao.
 
Shida inaanzia pale ambapo kwa namna moja au nyingine third party ambaye ni crdb anatajwa kwenye hadithi ya miamala yako. Hapo ndipo tigo watakuja kukuacha vizuri mahakamani.

Kesi ingekua tamu kama ungekua unadeal na tigo au agent wake lakini akishahusika third party kuwa mpole tu chukua statement fuatilia kwa kujumlisha na kutoa miamala utajua tatizo
 
Leo ni siku kadhaa nikipambana na wizi wa pesa niliyokuwa nayo ndani ya tigopesa. Huduma kwa wateja wameleta hadithi tofauti za aina tatu zote nimekataa. Walianza na kusema zimerudi benki, benki imesema haina ujinga huo. wakasema zitarudi baada ya masaa 24 bado hazikurudi. Mwisho wanasema nilikopa wamerudisha mkopo wao, nimekataa sijawahi na sitawahi kukopa tigo. Naona wanajikanyaga tu!

Niongozeni nipambane nao na mara hii natamani mawasiliano na vijana wa Law school ili nipate fidia ya kutosha kutokana na upuuzi huu.
Piga TCRA kwa kutumia namba iliyoibiwa, eleza kila kitu kilivyokua, wao watakupa muongozo. Na ukiweza nenda ofisini kwao kabisa
 
Shida inaanzia pale ambapo kwa namna moja au nyingine third party ambaye ni crdb anatajwa kwenye hadithi ya miamala yako. Hapo ndipo tigo watakuja kukuacha vizuri mahakamani.

Kesi ingekua tamu kama ungekua unadeal na tigo au agent wake lakini akishahusika third party kuwa mpole tu chukua statement fuatilia kwa kujumlisha na kutoa miamala utajua tatizo
Kwamba CRDB wanaweza kutoa hela kwenye acc ya tigo pesa?
 
Kwamba crdb wanaweza kutoa hela kwenye acc ya tigo pesa?
Yaonekana ni hatari sana kuweka kiasi kikubwa cha pesa ktk makampuni ya simu. Vijana wa makampuni haya, wana njaa! Huko pitishieni elfu chache tu maana sasa nasikia huwa pia wanadokoa-dokoa elfu 1, 2, na hata mia 5 bila wenye pesa kujua.

Ningeomba kisa hili kitangazwe ili iwe ni alert kwa wengi.
 
Leo ni siku kadhaa nikipambana na wizi wa pesa niliyokuwa nayo ndani ya tigopesa. Huduma kwa wateja wameleta hadithi tofauti za aina tatu zote nimekataa. Walianza na kusema zimerudi benki, benki imesema haina ujinga huo.

Wakasema zitarudi baada ya masaa 24 bado hazikurudi. Mwisho wanasema nilikopa wamerudisha mkopo wao, nimekataa sijawahi na sitawahi kukopa tigo. Naona wanajikanyaga tu!

Niongozeni nipambane nao na mara hii natamani mawasiliano na vijana wa Law school ili nipate fidia ya kutosha kutokana na upuuzi huu.
Turud nyuma kwanza hela yenyewe sh ngap isije ikawa tutamia nguvu nying kumbe hela yenyewe buku
 
Waliwahi nilia 80k zangu hawa Tigo, na nilihamaa kabisa mtandao wao, ni wezi watupu.
 
Hii tigo App ya pesa kuweni nayo makini. kuna tafiti nimeifanya imenifanya kuogopa kutumia
 
Back
Top Bottom