Tigo wanashirikiana na matapeli kutapeli mawakala wao?

kimaus

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
582
Reaction score
707
Wanajamvi, naandika uzi huu nikiwa na hasira kali sana.

Mimi nina ka kabiashara kangu ambapo pia nimeweka uwakala wa Tigopesa na mitandao mingine. Mke wangu anasimamia hako ka biashara, hata line za mitandao za pesa kasajili kwa jina lake.

Jana kaja mteja wa kiume kutoa pesa, katoa kama kawaida na jina likatoka la kike.

Baada ya dakika kadhaa wakala akapokea sms toka tigo kuwa muamala aliofanya umesitishwa. Akapiga simu tigo kuuliza akaambiwa kweli aliyetoa pesa kasitisha muamala, hivyo asubiri baada ya masaa 24 watasikiliza pande zote mbili kujua nani ana uhalali.

Mke akasubiri mpaka leo hii, alipopiga simu akaambiwa mbona huo muamala umesharudishwa kwa mteja aliyeusitisha!!

Ikabidi aende ofisi za tigo Mbagala Zakhem kwa kuwa ofisi ipo Mbande wilaya ya temeke, amefika pale mtumishi wa tigo anamjibu eti "ulipaswa umuangalie aliyetoa kama ndiye mwenyewe", really?

Mimi nikafuatilia kwenye ofisi zingine za tigo nikaambiwa kuwa kwa kawaida muamala wenye utata huwa unasitishwa lkn haupelekwi popote mpaka wahusika waitwe, wasikilzwe, uangaliwe mnara unaosoma kwa wakala je ni huo huo ndipo muamala umefanyika au la, na kama ni huo huo bna pesa ilitolewa kihalali, basi wakala anapewa pesa zake.

Mnara unaosoma ni mmoja, wahusika hawajaitwa wote kusikilizwa, badala yake tigo wanaruhusu pesa kurudi kwa mtu aliyetoa!!!

Maana yake sasa mawakala watakuwa wanatapeliwa kwa sababu kila mtu atatoa pesa kwa wakala alafu anausitisha muamala.

Ninachokiona hapa mtumishi wa tigo ameshirikiana na matapeli kututapeli kwa sababu hakufuata protocol za kazi yake.

Hili suala litafika mpaka TCRA kama tigo hatarudisha muamala wetu japo ni wa 120k tu, lkn hiyo ndiyo faida yenyewe.
 
Kama tigo, tumejitaidi kuboresha na kuimarisha mifumo yetu ya data base hivyo sio katika kusema Tigo inahusika na mfumo huu bali inatokea uwepo wa uzembe wa mtoa huduma kutozingatia sheria za kifedha na Electronic tunazo zitoa kila siku kuwa makini na utoaji huduma za kifedha.
Sasa kama unakiri inawezekana kuna uzembe, kwa nini useme si kweli?
 
Kama tigo, tumejitaidi kuboresha na kuimarisha mifumo yetu ya data base hivyo sio katika kusema Tigo inahusika na mfumo huu bali inatokea uwepo wa uzembe wa mtoa huduma kutozingatia sheria za kifedha na Electronic tunazo zitoa kila siku kuwa makini na utoaji huduma za kifedha.
Mteja kaja katoa fedha kihalali, alafu wakala ana pay the price?
 
Kama tigo, tumejitaidi kuboresha na kuimarisha mifumo yetu ya data base hivyo sio katika kusema Tigo inahusika na mfumo huu bali inatokea uwepo wa uzembe wa mtoa huduma kutozingatia sheria za kifedha na Electronic tunazo zitoa kila siku kuwa makini na utoaji huduma za kifedha.
Kwa nini mrudishe pesa kwa mteja aliyetoa pesa kwa wakala bila ya kumpigia wakala? Kwa nini mrudishe muamala wenye utata bila ya kuwaita wote, kufuata protocol zenu wenyewe za kuangalia mnara ulitumikq? Hamuoni kuwa hamkwepi kuwa accomplice?
 
Wanajamvi, naandika uzi huu nikiwa na hasira kali sana.

Mimi nina ka kabiashara kangu ambapo pia nimeweka uwakala wa Tigopesa na mitandao mingine. Mke wangu anasimamia hako ka biashara, hata line za mitandao za pesa kasajili kwa jina lake.

Jana kaja mteja wa kiume kutoa pesa, katoa kama kawaida na jina likatoka la kike.

Baada ya dakika kadhaa wakala akapokea sms toka tigo kuwa muamala aliofanya umesitishwa. Akapiga simu tigo kuuliza akaambiwa kweli aliyetoa pesa kasitisha muamala, hivyo asubiri baada ya masaa 24 watasikiliza pande zote mbili kujua nani ana uhalali.

Mke akasubiri mpaka leo hii, alipopiga simu akaambiwa mbona huo muamala umesharudishwa kwa mteja aliyeusitisha!!

Ikabidi aende ofisi za tigo Mbagala Zakhem kwa kuwa ofisi ipo Mbande wilaya ya temeke, amefika pale mtumishi wa tigo anamjibu eti "ulipaswa umuangalie aliyetoa kama ndiye mwenyewe", really?

Mimi nikafuatilia kwenye ofisi zingine za tigo nikaambiwa kuwa kwa kawaida muamala wenye utata huwa unasitishwa lkn haupelekwi popote mpaka wahusika waitwe, wasikilzwe, uangaliwe mnara unaosoma kwa wakala je ni huo huo ndipo muamala umefanyika au la, na kama ni huo huo bna pesa ilitolewa kihalali, basi wakala anapewa pesa zake.

Mnara unaosoma ni mmoja, wahusika hawajaitwa wote kusikilizwa, badala yake tigo wanaruhusu pesa kurudi kwa mtu aliyetoa!!!

Maana yake sasa mawakala watakuwa wanatapeliwa kwa sababu kila mtu atatoa pesa kwa wakala alafu anausitisha muamala.

Ninachokiona hapa mtumishi wa tigo ameshirikiana na matapeli kututapeli kwa sababu hakufuata protocol za kazi yake.

Hili suala litafika mpaka TCRA kama tigo hatarudisha muamala wetu japo ni wa 120k tu, lkn hiyo ndiyo faida yenyewe.
Tafuta mwanasheria atakuongoza
 
Back
Top Bottom