tiGO yaburuzwa mahakamani kudaiwa fidia ya sh. 26,880,000/=

tiGO yaburuzwa mahakamani kudaiwa fidia ya sh. 26,880,000/=

Nchi yetu inapita kwenye kipindi kigumu. Vijana wetu wengi wana tatizo kubwa kwenye hesabu!! Huyu alimaanisha milioni 26.88 au angesema 26,880,000.

Fikiria mtu anashindwa kujua kuwa milioni 1, ni tofauti kabisa na milioni 1000,000. Milioni 26,880,000, ni sawa na 26,880,000 × 1,000,000 = 26,880,000,000,000; hii ni trilioni 26.88.

Ndo matokeo ya shule za kata hayo
 
kesi ya fidia ya sh. 26,880,000/= dhidi ya tigo (honora plc) itaanza kusikilizwa kesho mahakama ya mwanzo ilala.
 
Kampuni mama ya tiGO Tanzania 'HONORA TANZANIA MOBILE SOLUTIONS LTD' wamefikishwa mahakama ya mwanzo Ilala wakidaiwa fidia ya shilingi milioni 26,880,000/=

Shauri hili namba 270/2024 litaanza kusikilizwa mbele ya hakimu mfawidhi Judith Kobo baada ya tigo kutuhumiwa kuanzia kipindi cha tarehe 30 April mpaka 16 May 2024 kumkata mteja Aitwae Benedict K. Kiasi cha shilingi 118,000/= kinyume cha utaratibu.

Madai haya yamefikishwa mahakamani baada ya hapo awali Mteja kuwasilisha malalamiko yake dawati la malalamiko la tiGO kwa mujibu wa kanuni za benki kuu zinazomlinda mteja za mwaka 2019, ambapo tiGO hawakujibu.

Mteja aliwasilisha malalamiko yake Benki Kuu ya Tanzania kwa mujibu wa kanuni, ambao benki kwa barua yao ya tar 1/9/2024 walimshauri mteja kuwasilisha malalamiko hayo mahakamani ili kupata uamuzi wa mahakama.
Kwa Miranda ya simu hiyo 26.8 m ni pesa ndogo sana hata kama kesi iko primary court.
 
shilingi milioni 26,880,000/= unazijua wewe ?
Elimu ndio tatizo,
Mtu kama huyu anaweza hata kukuambia hiyo figure ni sawa sawa kabisa na Million 26.88.

Hawazi kabisa kama zote ni million, kwanin kwenye numbers kuwe na tofauti na bado iwe sawa?
 
Back
Top Bottom