Ni mkasa wa aina yake, dakika kadhaa kabla ya mchezo wa fainali ya kombe la dunia mwaka 1998 pale nchini Ufaransa, katika mechi iliyokuwa inazikutanisha Ufaransa Vs Brazil kulitokea tukio la kushangaza sana.
Mshambuliaji bora wa wakati huo, Ronaldo De Lima alipatwa na ugonjwa wa ghafla na kuondolewa kwenye kikosi cha kwanza.
Dakika kadhaa baadae, akapata nafuu akapangw ingawa inaaminika alifosiwa. Kwenye fainali akawa mdembwedo kweli. Mpaka leo kuna nadharia nyingi juu ya tukio hilo. Je nini hasa kilimkuta Ronaldo?