Tijikumbishe: Ronaldo De Lima alikumbwa na nini Fainali ya Wold Cup 98

Tijikumbishe: Ronaldo De Lima alikumbwa na nini Fainali ya Wold Cup 98

Mkuu nashangaae sasa hivi Greece kwenye ramani ya soka kama vile wamefifia mambo yamebadilika.

Hata kabla ya pale hawakuwepo kwenye ramani, na baada ya pale walipotea.

Baadhi ya wachezaji walipata pata timu lakini timu ya taifa haikufanya chochote tena.

Hata ushiriki wa Euro na WC hawapati.
 
2004 hujui alichomfanya Mwingeleza dak za 90 au unajisahaulisha magoli ya Zizou?

Kijana kubali kataa kile kizazi kilikuwa bora

Worldcup 98
Euro 2000
Euro 2004
World cup 2006

Miaka hiyo yote nane kizazi kile kilikuwa bora
( iv unakumbuka 2006 France ilikuwa na no 9 ( kumi na 6 kati yao wakiwa wanaongoza ufungaji bora kwenye league wanazocheza? Mpk kocha anashindwa nan wa kupangwa?)

Labda kama umeanza kuangalia mpira juzi but kizazi cha Zidane/Thuram/Lizarazu/Deschamps/blanc etc kilikuwa bora sana
Mbona mnaruka World Cup ya 2002 pale South Korea na Japan,au hicho kizazi chenu cha dhahabu akikushiriki mwaka huo?
 
Ni mkasa wa aina yake, dakika kadhaa kabla ya mchezo wa fainali ya kombe la dunia mwaka 1998 pale nchini Ufaransa, katika mechi iliyokuwa inazikutanisha Ufaransa Vs Brazil kulitokea tukio la kushangaza sana.

Mshambuliaji bora wa wakati huo, Ronaldo De Lima alipatwa na ugonjwa wa ghafla na kuondolewa kwenye kikosi cha kwanza.

Dakika kadhaa baadae, akapata nafuu akapangw ingawa inaaminika alifosiwa. Kwenye fainali akawa mdembwedo kweli. Mpaka leo kuna nadharia nyingi juu ya tukio hilo. Je nini hasa kilimkuta Ronaldo?

Degedege, najiuliza ingekuwaje kama Ronaldo angekuwa fit 100% pengine Ufaransa wasingebeba World Cup
 
Wanasema Alipata "gedegede" aah!!!! Alipata degedege

Wengine wanadai france walifanya yao..

Wengine wanasema Adidas walifanya yao ili zizzou ambae alikuw chini ya adidas annyanyue ndoo.
Hii inakuja kwa nguvu ya ushindani wa biashaka kati ya nike(mdhamini wa ronaldo de lima) na adidas(mdhamini wa zinedine yazid zidane, zizzou)
Ahsante
 
Back
Top Bottom