Timbulo ampongeza Alikiba na kumkosoa Diamond, kisa kolabo na wasanii wa nje

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Timbulo amesema wasanii wa Bongo wajifunze kutoa kazi zao kwa lengo la kujitangaza nje ya nchi kuliko kutengemea wasanii wa nje ambao muda mwingine hawana mchango wowote.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Vibaya’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa mfano mzuri kolabo ya Diamond na Davido kwani kolabo hiyo ilimtangaza zaidi Davido hapa nchini kuliko Diamond nchini Nigeria.

“Kumshirikisha msanii wa nje ni kumleta hapa, tumemjua Davido baada ya kushirikishwa na Diamond baada hapo Davido alikuwa kama Mtanzania vile, anavyopingwa utasema anatokea Manzese vile lakini Davido hakumsaidia kule. Chukua mziki upeleke kule, Darassa ame-trend mpaka Afrimma hakumshirikisha msanii yeyote wa nje” amesema Timbulo.

Timbulo aliendelea kwa kusema Alikiba ameweza kushinda tuzo bila kolabo na msanii wa nje na kueleza hivyo ndivyo inatakiwa.

“Mfano Turudi hapa hapa, Alikiba amefanya kazi nyingi na amefikia hatua amechukua tuzo za MTV si kwa kolabo ni kazi za nyumbani, kwa hiyo tunaweza kufanya siyo lazima kolabo nje watu wasikariri” amesisitiza.



Bongo 5
 
timbulo yule aliekataliwa kolabo na vanessa ?
eti kisa Vanessa hamjui Timbulo
 
tangu vanessa aseme hamjui jamaa mpaka leo hayuko poa
 
Amefanya utafiti gani wa kuthibitisha kuwa Wasanii wa Bongo baada ya kufanya collabo hawatambuliki Nchi za wasanii waliofanya colabo nao??? Elimu ni kitu kizuri sana fanya vyote usikose elimu
 
Timbulo ana stress ni wachache tu watamshtukia. Vanessa alimkana on air kuwa hamjui Pia Kuna collable nyingi za mastaa wa hapa hapa jamaa kaomba kanyimwa
 
Timbulo ili aendelee kushine kama zamani ilibdi aendelee tu kucopy nyimbo za kina maxmalea(spelling sahihi sizijui) ila ni wale jamaa wa cameroon cjui aliowaibia melody ya zile ngoma zake mbili Domo langu na waleo wakesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…