Time For Change: Sema "hapana" ngwe ya pili ya JK

Time For Change: Sema "hapana" ngwe ya pili ya JK

Field Marshall Es,
Hapana mkuu wangu, huwezi kumlaumu Dr.Slaa kwa yaliyotokea Chadema hata kama alikuwa upande wa wazee au kuwaunga wazee kwa sababu Zitto kama msaidizi wake ingebidi amjulishe au hata awe na wajuimbe wa kutosha kugombea nafasi hiyo na sii kufanya mchezo wa sinema kumwona co starring anayekufa ktk tambara tu...

Zitto hakuwa na umri unaoruhusiwa kugombea Urais, hakuwa na caucus nyuma yake isipokuwa washabiki, sasa nini lengo lake kugombea nafasi ambayo anajua wazi haimtahili?..Kisha mkuu wangu ni jambo la kawaida kabisa kwa wazee wa chama kuongea na mgombea alochukua form kutoleta ushindani ambao hauwezi kukisaidia chama. Iwe ubunge au Urais. Na demokrasia ya kweli haiwezi kumtenga Dr. Slaa mapendekezo yake ktk nafasi hiyo. Kama alikuwa akimpendekeza Mbowe basi lilikuwa jukumu lake kusimama nyuma ya Mbowe hata iwe ni uchaguzi wa ndani. Wewe mwenyewe uliona jinsi maseneta walivyojipanga nyuma ya Obama wakamwacha Mama Clinton na wakasema mengi kuhusiana na mama Clinton.

Mwenye makosa hapa ni Zitto mwenyewe alotaka kugombea kisha akaliondoa jina lake yeye mwenyewe wakati tunawaona vigogo wa siasa kama mzee Malecela alilia haki yake hadi dakika ya mwisho pamoja na kwamba wazee wa CCM walimmfuata na kumwomba achomoe jina lake toka ktk wagombea...Hakufanya hivyo hadi wazee wenyewe walipolazimika kuchukua hatua kinyume cha katiba..

Hata hivyo issue hapa sii upinzani kati ya Zitto na Dr.Slaa..isipokuwa ni mila na desturi za chama katika kuugombea nafasi za juu za chama badala ya kutumia njia za kina Don Coleone..hiyo ni party assassin ambayo mheshimiwa Dr. Slaa asingeweza kushiriki! Pili siudhani kama unafahamu kwamba kulikuwepo na makundi tayari ndani ya Chadema!.. toka Zitto achukue ile nafasi ya kamati ya madini kinyume cha mapendekezo ya kamati ya chama chake.. Zitto aligeuka kuwa mshindani ndani ya chama na naweza kusema alionekana kuwa na ambition!..Hiyo ambtion ndiyo ilikuwa tishio kwa chama kizima..

Mkandara
Umri na uenyekiti wapi na wapi mkuu??

Mbatia ni m/kiti NCCR nafikiri hana umri unaosema na kama anao basi kaufikisha jana na mugombea urais alikuwa DR Mvungi sijui huyu hata ana nafasi gani NCCR.
 
- Mkulu Nyani, ahsante sana kwa kuniwahi maana huu wako ndio ukweli wenyewe, ni kwamba nani wa kushika hiyo nafasi ambaye ni bora kuliko JK, mbona hatujamsikia au kuwa kimya ni moja ya skills better than JK?

- Binafsi baada ya yote yaliyojiri politically in the last five weeks, sina nguvu sana na wala imani katika uwezo wetu wa-Tanzania kufanya tofauti na walioko kwenye power sasa hivi, labda atajwe japo mmoja tumchambue!

- Nilikuwa nina imani sana na Zitto na Chadema kwa ujumla kwa mbele ya safari, lakini wamenikatisha tamaa kabisaa, labda watoto wetu lakini kwenye hii generation, labda itokee miracle!

Respect.

FMEs!

Katika wale wapiganaji ndani ya CCM hakuna anayefaa kwa urais?
 
Katika wale wapiganaji hakuna anayefaa kwa urais?

- Mkuu jibu swali ndio uulize swali na utajibiwa, swali langu la msingi ni nani anayeyefaa kushika urais kuliko Kikwete kwa sasa, now jibu that ndio uulize na utajibiwa au uchune mkuu!

- Waberoya, acha utoto mkuu taifa linateketea sasa lets talk taifa na sio emotions ambazo haziwezi kulisaidia taifa, I am for real mamen sio fugazz, unapotaka kujadili taifa na mimi ni lazima uwe umejitayarisha sio kukurupuka! Na hata ukitaka kufuata njia ya personal kama ulivyoamua nako pia nipo mzima sana mkuu, bingwa wa hoja wa dunia hapa huwa anafuta hoja zangu na kunizuia nisiingie mpaka apitishe agenda zake, wewe huu mfupa unaomshinda fisi huuwezi mkuuu wangu na usinitishe maana sitishiki na you know that tena better!

Respect.

FMEs!
 
- Kuacha Dr. Slaa hao wengine wamefanya nini hasa cha maana?
- Halafu na yeye Dr. Slaa baada ya yote yaliyojiri huko Chadema hivi majuzi, anapata wapi tena ile moral authority aliyokuwa nayo siku zote huko nyuma? Iwapo anashiriki kwenye demokrasia makini inayotumia busara za wazee wa chama ambao hawamo kwenye katiba ya chama kumuengua kiongozi mwenziwe, tena msaidizi wake katika kugombea uongozi wa juu wa chama hicho, sasa akipewa Jamhuri itakuwaje?

- Ina maana hata hawa mafisadi anaowalalia macho kuwafichua atawapeleka huko huko kwenye baraza la wazee wa chama, badala ya kufuata katiba ya jamhuri, ndiyooo! si ukweli tumeuona kwa macho yetu na tumeusikia kwa masikio yetu tena na wahusika wote wa hiyo cinema hapa JF, au?

Inasikitisha sana, hili taifa tumelaaniwa tu tutaendelea kudanganyana na kuzunguka hapa hapa tulipo!

Respect.

FMEs!

Pamoja na respect yako. Najua utanitolea mbovu kama kawaida.
Ila wewe ni mtaalamu wa kula matapishi yako.

Respect FMEs!
 
- Mkuu jibu swali ndio uulize swali na utajibiwa, swali langu la msingi ni nani anayeyefaa kushika urais kuliko Kikwete kwa sasa, now jibu that ndio uulize na utajibiwa au uchune mkuu!

FMEs!

Kaka, sina lingine yale yameisha,mbona nimeuliza mkuu, kuwa katika wale wapiganaji ndani ya CCM hakuna anayefaa kwa urais, maana test yao kubwa ili wawe kweli wapiganaji ni kushindana na JK! hapo wataaminika kweli wana malengo mazuri.

MKJJ anasema (sema hapana),they have to say no, if JK will pass without contesting, after all JK yuko kwenye ile list of shame , na ameprove kwa kutofanya lolote miaka hii, minne!

Akijitokeza katika wale wapiganaji, akagombea urais, kwa nini niende kwenye CCM-B( chadema)? ila wasipojitokeza ndio unaona thread kibao na watu kweli wanaanza kuwashtukia!

Anyway, nani anafaa kwa urais zaidi ya JK? nadhani ulitaka niulize hivi! CCM namfahamu Magufuli tu, maneno machache vitendo vingi.

Mkuu, sina kinyongo yale yameisha believe me, usiende mbali huko,

kama utataka nisijibu post yako yeyote, sema tu, sina hiyana mie!
 
Pamoja na respect yako. Najua utanitolea mbovu kama kawaida.
Ila wewe ni mtaalamu wa kula matapishi yako.

Respect FMEs!

- Respect tena hoja yako ni nini hasa mkuu? Bwa! ha! ha! Siasa sio jeshi mkuu ikibadilika na wanasiasa tunabadilika, Dr. Slaa ni shujaa wangu sana lakini kwenye hili la mauza uza ya Chadema, amenishangaza sana sikutegemea kabisa kwamba atakubaliana na maamuzi ya kuwasikiliza wazee wa chama badala ya katiba ya chama,

- kwa hili sitamsamehe yeye wala viongozi wote waliohusika huko, CCM mpaka leo tunahangaika sana kwa sababu bado tunaishi na maamuzi yale yale ya miaka 40 iliyopita na hawa wa sasa wanayarudia yale yale, kama kwa kuwa na haya mawazo ni kula matapishi yangu then be it!

Respect.

FMEs!
 
- Dr. Slaa ni shujaa wangu sana lakini kwenye hili la mauza uza ya Chadema, amenishangaza sana sikutegemea kabisa kwamba atakubaliana na maamuzi ya kuwasikiliza wazee wa chama badala ya katiba ya chama,

Respect.

FMEs!

Ulichosema hapa ni ukweli, sidhani kama kuna ubishi, na ninapenda unapokuwa mkweli hivi, wewe mwenywe na chama chako ruhusu uwe subject of truth or facts!

Mtu akibisha kuwa yaliyotokea CHADEMA hivi majuzi ni ufisadi ,nadhania atakuwa anapigana na ukuta wa matofali, na mtu akibisha kuwa CCM wote mafisadi naye anapigana na ukuta wa zege!
 
Kaka, sina lingine yale yameisha,mbona nimeuliza mkuu, kuwa katika wale wapiganaji ndani ya CCM hakuna anayefaa kwa urais, maana test yao kubwa ili wawe kweli wapiganaji ni kushindana na JK! hapo wataaminika kweli wana malengo mazuri.

MKJJ anasema (sema hapana),they have to say no, if JK will pass without contesting, after all JK yuko kwenye ile list of shame , na ameprove kwa kutofanya lolote miaka hii, minne!

Akijitokeza katika wale wapiganaji, akagombea urais, kwa nini niende kwenye CCM-B( chadema)? ila wasipojitokeza ndio unaona thread kibao na watu kweli wanaanza kuwashtukia!

Anyway, nani anafaa kwa urais zaidi ya JK? nadhani ulitaka niulize hivi! CCM namfahamu Magufuli tu, maneno machache vitendo vingi.

Mkuu, sina kinyongo yale yameisha believe me, usiende mbali huko,

kama utataka nisijibu post yako yeyote, sema tu, sina hiyana mie!

- Mkuu kwani MMJ amewahi kufanya nini zaidi ya hao wapiganaji, si wote kazi yao ni kuongea tu maneno mengi kama sisi wengine, Wapiganaji ni viongozi waliochaguliwa na wananchi kuongoza majimbo yao sasa kama hawafai basi ni wajibu wa wananchi kuwapiga chini kwenye kura.

- Binafsi nina-side na wapiganaji kwa sababu kama Mwalimu, wanaongea lugha ninayoikubali na inayokubalika na wananchi wengi ndio maana kama sio wao Busanda na Biharamulo tungekula chuya, lakini ni haki yako kuwaona hawafai na ni mafisadi si unajua katika politics inakubalika kuwa na maoni mbali mbali.

- Maghufuli, siamini kwamba anafaa baada ya kumuona kwa macho yanbgu akiwauzia ndugu zake nyumba za serikali, badala ya wastaafu wa serikali kama sheria ya bunge ilivyotaka, sasa akipewa urais huyu itakuwaje na sheria? yale yale tu!

- Halafu ni lini umewahi kusikia Maghufuli akipingana na Rais wa sasa hadharani? Au akipingana na CCM hadharani? Si mmesema kwamba hizi ndio sifa za anayeweza kum-replace Muungwana sasa hivi.

Heshima zaidi kwa finally kujadili hoja, that all I could ask na repst tena mkuu.

Respect.

FMEs!
 
Mkandara
Umri na uenyekiti wapi na wapi mkuu??

Mbatia ni m/kiti NCCR nafikiri hana umri unaosema na kama anao basi kaufikisha jana na mugombea urais alikuwa DR Mvungi sijui huyu hata ana nafasi gani NCCR.

Mkuu mfano wako haupendizi hata kidogo kwani CVCM wao huchagua mwenyekiti baada ya kupita kiti cha Urais tena mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu. hao NCCR ndio kama hivyo sidhani kama Mbatia hakuchaguliwa against Dr. Mvungi ambaye alikuwa mwenyekiti hapo awali.

Kama unakumbuka niliwahi kuuliza ni utaratibu upi upo Chadema na kwa maelezo mengi ikiwa ni pamoja na Dr.Slaa mwenyewe.. nikinukuu baadhi ya majibu yake alizungumzia pia umri wa Zitto. Inaonyesha wazi Mbowe ndiye atasisi tena kugombea kiti cha Urais..
Ni utaratibu nisioukubali wala kuupendekeza lakini ndivyo ilivyo. Kwa hiyo pengine Zitto aligombea kiti hicho akitarajia kuwa mgombea wa chama kiti cha Urais...Na kama shieria inasema tofauti nashindwa kuelewa kwa nini Zitto alikubali ushauri wa wazee.
Na sii kweli wazee walikiuka sheria au katiba ya chama hata iwe mumuengua Zitto kwa sababu zipo taratibu ktk kila chaguzi. kama mnakumbuka yule mgombea wa Chadema Mbeya vijijini alienguliwa jina lake. Mgombea mwingine wa CCM akapita kwa makosa sawa na yule wa Mbeya lakini waheshimiwa hawakuyaona makosa hayo!..
Binafsi nilitegemea Zitto angesimama ngangari hadi chama kieleze kwa nini kimefikia hatua ya kuondoa jina lake lakini niliposikia Zitto mwenyewe kajiondosha.. then hatuna kesi.

Mkuu ukienda futa kesi mahakamani na mshtakiwa kaachiwa huru.. kisha ijulikane ulifanya hivyo kutokana na ushauri wa wazee.. Iweje sisi tuseme hao wazee walikiuka katiba au sheria ya nchi..Zitto alifuta kesi mwisho wa mazungumzo, kuendelea kuwalaumu viongozi wa Chadema hizi ni propaganda chafu..If anything wa kumlaumu ni Zitto, mimi binafsi sina makubwa zaidi ya kukubali matokeo isipokuwa nitawalaumu hao wapambe walokuja na JEURI YA KWAPA -kunuka bila kidonda! jeuri ambayo ilimpekea Zitto kubwabwaja ovyo..
 
- Mkuu kwani MMJ amewahi kufanya nini zaidi ya hao wapiganaji, si wote kazi yao ni kuongea tu maneno mengi kama sisi wengine, Wapiganaji ni viongozi waliochaguliwa na wananchi kuongoza majimbo yao sasa kama hawafai basi ni wajibu wa wananchi kuwapiga chini kwenye kura.

- Binafsi nina-side na wapiganaji kwa sababu kama Mwalimu, wanaongea lugha ninayoikubali na inayokubalika na wananchi wengi ndio maana kama sio wao Busanda na Biharamulo tungekula chuya, lakini ni haki yako kuwaona hawafai na ni mafisadi si unajua katika politics inakubalika kuwa na maoni mbali mbali.

- Maghufuli, siamini kwamba anafaa baada ya kumuona kwa macho yanbgu akiwauzia ndugu zake nyumba za serikali, badala ya wastaafu wa serikali kama sheria ya bunge ilivyotaka, sasa akipewa urais huyu itakuwaje na sheria? yale yale tu!

- Halafu ni lini umewahi kusikia Maghufuli akipingana na Rais wa sasa hadharani? Au akipingana na CCM hadharani? Si mmesema kwamba hizi ndio sifa za anayeweza kum-replace Muungwana sasa hivi.

Heshima zaidi kwa finally kujadili hoja, that all I could ask na repst tena mkuu.

Respect.

FMEs!

Mkuu FMES nakubaliana na wewe kwa baadhi ya mambo. Kweli Magufuli ni mchapa kazi lakini hastahili hata kwa asilimia 20 kuwa rais wa Tanzania. Mfano mzuri ni kuwauzia ndugu zake nyumba za serikali, nasikia pia aliwahi kuzuia ujenzi wa daraja pale kivuko ambao ulikuwa ni msaada kutoka uarabuni, kisa hakupewa 10%(wanaoujua vizuri wanaweza kunisahihisha), ni mtu anayependa sifa, na alizirai baada ya kusikia hajateuliwa kuwa waziri mkuu haya mambo yanaweza kukupa picha yeye ni mtu gani, power maniach. Sijui kama tunahitaji rais kama huyo.
Zitto ameonesha true colours, naona hata ubunge hafai anayosema hayana udhati, na yye mwenyewe anaonekana kuwa ni mtu wa self interest. tayari ameibomoa Chadema, sasa hivi Chadema imekuwa lame kutokana na utoto ulioonekana kwenye mkutano wake. Naunga mkono alichofanya Slaa na wazee a Chadema, kweli it is not constitutional lakini ni vizuri zaidi kuliko wangemuacha akivuruge kabisa Chama.

Lakini usiwe pessimistic sana, kuna watanzania wanaoweza kuiongoza nchi far better ya tulivyoona kwenye miaka hii mitano. Siamini hata kidogo wanaosema hakuna anayeweza kuongoza ila Kikwete. It is not about anyone but JK, it is about someone else who can do things in a different way.

Kwenye miaka hii mitano, hakuna kimsingi kilichofanyika, ukilinganisha na miaka mitano iliyopita, kama kipo not significant at all. Sioni kama ni busara kama tutakuwa na miaka mingine mitano kama hiyo.

Ni kweli kwa siasa za Tanzania, kwa kizazi cha sasa ni vigumu sana kupata mtu ambaye atacheza game in a style that we all wish, and in a style that will take us forward. But vigumu does not mean haiwezekani.
 
No no no! Haya ya kum invoke Mungu hayana nafasi.

Unajua Tanzania na Afrika nzima kwa ujumla wangekuwa wanafikiri kama mimi tungekuwa mbali sana kimaendeleo. Basi tu....

common sense is not common......
 
- Mkuu kwani MMJ amewahi kufanya nini zaidi ya hao wapiganaji, si wote kazi yao ni kuongea tu maneno mengi kama sisi wengine, Wapiganaji ni viongozi waliochaguliwa na wananchi kuongoza majimbo yao sasa kama hawafai basi ni wajibu wa wananchi kuwapiga chini kwenye kura.

FMEs!

MKJJ ana act kama masterminder, brain, catalyst, stimulant, !

Kikanisa tunaamini binadamu ni viungo na kila mmoja ana act kwa nafasi yake , MKJJ akiwa kiongozi hawezi kuandika hizo post atafanya yaliyo ya uongozi na tutampima kwa nafasi yake.

Kwa sasa kwa nafasi yake ameweza kuwa kama nilivyokueleza, ana-analyse mambo, anakufanya uwaze, ujione mjinga, uangalie pembeni na kusonga mbele, ameweza kuandika nakala mbalimbali, na kuamsha wengi walio lala, na ana kijarida chake Cheche! amefanya kwa nafasi na uwezo wake na kwangu mimi amefanikiwa na in this planet ame ADD VALUE TU HUMAN EXISTENCE! kuliko professors wengi vyuo vyetu vikuu, kuliko mimi na pengine wewe!

Hao wengine(viongozi) wanatakiwa wachuke mawazo na changamoto za akina MKJJ na wengine na kuziweka into practise! Ndiyo maana Sir Isaac Newton alikuwa scientist, Einstein alikuwa scientist, it took engineers (like me)to take their theories and put into action! ndiyo maana kuna wanasayansi na wahandisi na madoctor!

Viongozi hao wanaoongea wako katika position ya kutekeleza na kufanya kitu kikaonekana, ndiyo maana(May 25, 1961, President John F. Kennedy ALISEMA lazima waende mwezini) wakaenda!

Tunataka viongozi wa kuleta matokeo, wa kutatua matatizo, na sio kuyakimbia. we need brains at the top.

Kuhusu Magufuli, well kama wewe mwana CCM unasema hafai kwa hizo sababu nisemeje? nakubaliana na wewe.

But the question still there, unafikiri nani anaweza kuwa rais mbali ya JK, hata kama JK atakuwa tena rais lakini tujue kuwa kuna wana CCM kama FMES wanakili kuwa wako wengine wanafaa, hii nayo itakuwa dalili nzuri.
 
Jamani Jamani msiwe wasahaulifu kiasi hicho... Mkapa kaiacha nchi kama Bush alivyoiacha Marekani...nchi ikiwa ktk matatizo makubwa ya Kiuchumi..

Reli ya kati ilikuwa haifanyi kazi, hatuna ndege wala shirika la ndege zaidi ya Precission tuliiona ktk daraja la Emirates, Umeme wa mgao tena kwa week, maji shida generator za watu binafsi zimetapakaa miji yote, visima vya maji ndio ilikuwa idara ya maji nchini..Mazao mikoani hayana maghala wala usafiri -magari yote makubwa safari zake ni Zambia, Congo na nchi za jirani kwa sababu hatukuwa na kitu kabisa cha kusafirisha nje..Hata mashirika ya ndege yalikata safari zake Tanzania kwa asilimia 50.. Kivukoni usafiri hakuna, mbuga ziliendelea kuuzwa, nyumba za serikali, mashirika yoote ya serikali yaliyobakia yalikuwa katika hali mbaya ajabu tukianza na hiyo Tanesco..Ni wakati watu waliweza kuiba hata BoT for christ sake!... BoT. Anayebisha hata moja hapo anifahamishe!.. jamanin haya hayakuwa maisha yetu na hali halisi ya Tanzania mwaka Dec 2004, jamani!
Leo mnakuja hapa na kusema JK ni mbovu kuliko woote waliotangulia!..Nooooo wakuu zangu hatumtendei haki hata kidogo. JK kasimamisha kazi zote za Mafisadi pamoja na kwamba hajawapeleka mahakamani. Kama angeachia yale yaliyokuwa yakitendeka toka wakati wa Mkapa hadi leo hii sijui tungebakiwa na kipi?

Binafsi sikubaliani na mtazamo huu ingawa nakubali kabisa kwamba JK ni msanii ana mapungufu mengi tu lakini sii kumweka kundi moja na viongozi waliotangulia..Trust me he is better of,
pamoja na kwamba hafai!
 
Who's the alternative? Or it's just Anybody But Kikwete (ABT)....

Kwa sababu mpaka sasa sijaona kiongozi yeyote aliyeonesha uongozi madhubuti na uliotukuka hususan ikija kwenye masuala ya ufisadi na muunganiko wake kwenye utawala mbovu vis-a-vis utawala bora.

Oh well....

Kwani watu wasipiganie kubadilisha system ya kupata viongozi wa kuchaguliwa? System ya sasa haina check and balance. Na hilo ndilo tatizo kubwa.
 
Jamani Jamani msiwe wasahaulifu kiasi hicho... Mkapa kaiacha nchi kama Bush alivyoiacha Marekani...nchi ikiwa ktk matatizo makubwa ya Kiuchumi..

Reli ya kati ilikuwa haifanyi kazi, hatuna ndege wala shirika la ndege zaidi ya Precission tuliiona ktk daraja la Emirates, Umeme wa mgao tena kwa week, maji shida generator za watu binafsi zimetapakaa miji yote, visima vya maji ndio ilikuwa idara ya maji nchini..Mazao mikoani hayana maghala wala usafiri -magari yote makubwa safari zake ni Zambia, Congo na nchi za jirani kwa sababu hatukuwa na kitu kabisa cha kusafirisha nje..Hata mashirika ya ndege yalikata safari zake Tanzania kwa asilimia 50.. Kivukoni usafiri hakuna, mbuga ziliendelea kuuzwa, nyumba za serikali, mashirika yoote ya serikali yaliyobakia yalikuwa katika hali mbaya ajabu tukianza na hiyo Tanesco..Ni wakati watu waliweza kuiba hata BoT for christ sake!... BoT. Anayebisha hata moja hapo anifahamishe!.. jamanin haya hayakuwa maisha yetu na hali halisi ya Tanzania mwaka Dec 2004, jamani!
Leo mnakuja hapa na kusema JK ni mbovu kuliko woote waliotangulia!..Nooooo wakuu zangu hatumtendei haki hata kidogo. JK kasimamisha kazi zote za Mafisadi pamoja na kwamba hajawapeleka mahakamani. Kama angeachia yale yaliyokuwa yakitendeka toka wakati wa Mkapa hadi leo hii sijui tungebakiwa na kipi?

Binafsi sikubaliani na mtazamo huu ingawa nakubali kabisa kwamba JK ni msanii ana mapungufu mengi tu lakini sii kumweka kundi moja na viongozi waliotangulia..Trust me he is better of,
pamoja na kwamba hafai!

Mkandara:

Kwa uchambuzi wangu finyu wa kisiasa, watanzania bado mnatafuta kiongozi atakayejichunga mwenyewe kama vile Nyerere. Viongozi kama hao ni wachache na kuwapata ni kucheza bahati nasibu.

Kinachotakiwa ni kuwepo kwa system ya check and balance. Kiongozi anaposhindwa basi kuwepo na vyombo vya kumuondoa na vilevile kuangalia utendaji wake wa kazi.

Kwa mfano hakuna nafasi ya uongozi katika CCM isiyohitaji kutoa chochote. Ukiambiwa gharama za mtu kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa vijana wa wilaya, wewe mwenyewe utashangaa. Kwa sababu mwenyekiti huyu anashiriki katika kura za maoni ya kuchagua mbunge.

Hivyo hata huyo shujaa wenu Mwakyembe, inawezekana amepita kwa kuhongahonga wilayani.

Na sasa kimefika kipindi karibu kila mtu amepata nafasi kwa kuonga. Je ni nani atakeyemnyooshea kidole mwenzake?
 
Mimi kura yangu nahifadhi mfukoni kwa sababu JK hanipi matumaini na wapinzani wananikoroga akili tu...hadi sasa hivi bado siwaelewi kabisa, labda aje mpinzani atakayegombea urais kupitia tiketi ya chama cha upinzani kitachotokea baada ya CCM kumegeka.
 
Niseme nini kisichojulikana? Alishinda kwa asilimia nyingi ya kura akijaza mioyo ya watanzania matumaini ya mwanzo mpya wa ujenzi wa taifa lao. Watu walitaraji mabadiliko. Walichopata badala yake ni mwendelezo wa sera ya uzembe, itikadi ya ufisadi na siasa za kubebana na ahadi za kuzugana. nchi yetu inastahili uongozi bora. Hatuitaji miaka mingine 5 ya viongozi walioshindwa. No 2nd term 4 kikwete. Yes i said it.
Mkuu mwanakijiji umerudi,afazali tumepumua kwa kukuona,maana tulihofu mafisadi ya ccm yasijekuwa yamekuteka.
Mkuu si kwa kikwete tuu bali ccm kwa jumla tuseme HAPANA
 
Nani anaweza kumfunda Lowasa aachane na mambo ya pesa ajikite kwenye uongozi wa nchi? Nani? Hilo likiwezekana basi anafaa. Hakuna kwenye upinzani. Wazuri bado wako hukohuko CCM.
 
Back
Top Bottom