Field Marshall Es,
Hapana mkuu wangu, huwezi kumlaumu Dr.Slaa kwa yaliyotokea Chadema hata kama alikuwa upande wa wazee au kuwaunga wazee kwa sababu Zitto kama msaidizi wake ingebidi amjulishe au hata awe na wajuimbe wa kutosha kugombea nafasi hiyo na sii kufanya mchezo wa sinema kumwona co starring anayekufa ktk tambara tu...
Zitto hakuwa na umri unaoruhusiwa kugombea Urais, hakuwa na caucus nyuma yake isipokuwa washabiki, sasa nini lengo lake kugombea nafasi ambayo anajua wazi haimtahili?..Kisha mkuu wangu ni jambo la kawaida kabisa kwa wazee wa chama kuongea na mgombea alochukua form kutoleta ushindani ambao hauwezi kukisaidia chama. Iwe ubunge au Urais. Na demokrasia ya kweli haiwezi kumtenga Dr. Slaa mapendekezo yake ktk nafasi hiyo. Kama alikuwa akimpendekeza Mbowe basi lilikuwa jukumu lake kusimama nyuma ya Mbowe hata iwe ni uchaguzi wa ndani. Wewe mwenyewe uliona jinsi maseneta walivyojipanga nyuma ya Obama wakamwacha Mama Clinton na wakasema mengi kuhusiana na mama Clinton.
Mwenye makosa hapa ni Zitto mwenyewe alotaka kugombea kisha akaliondoa jina lake yeye mwenyewe wakati tunawaona vigogo wa siasa kama mzee Malecela alilia haki yake hadi dakika ya mwisho pamoja na kwamba wazee wa CCM walimmfuata na kumwomba achomoe jina lake toka ktk wagombea...Hakufanya hivyo hadi wazee wenyewe walipolazimika kuchukua hatua kinyume cha katiba..
Hata hivyo issue hapa sii upinzani kati ya Zitto na Dr.Slaa..isipokuwa ni mila na desturi za chama katika kuugombea nafasi za juu za chama badala ya kutumia njia za kina Don Coleone..hiyo ni party assassin ambayo mheshimiwa Dr. Slaa asingeweza kushiriki! Pili siudhani kama unafahamu kwamba kulikuwepo na makundi tayari ndani ya Chadema!.. toka Zitto achukue ile nafasi ya kamati ya madini kinyume cha mapendekezo ya kamati ya chama chake.. Zitto aligeuka kuwa mshindani ndani ya chama na naweza kusema alionekana kuwa na ambition!..Hiyo ambtion ndiyo ilikuwa tishio kwa chama kizima..
Mkandara
Umri na uenyekiti wapi na wapi mkuu??
Mbatia ni m/kiti NCCR nafikiri hana umri unaosema na kama anao basi kaufikisha jana na mugombea urais alikuwa DR Mvungi sijui huyu hata ana nafasi gani NCCR.