Time For Change: Sema "hapana" ngwe ya pili ya JK


Mkandara
Umri na uenyekiti wapi na wapi mkuu??

Mbatia ni m/kiti NCCR nafikiri hana umri unaosema na kama anao basi kaufikisha jana na mugombea urais alikuwa DR Mvungi sijui huyu hata ana nafasi gani NCCR.
 
 
 
 
 
 
 
 
Mkandara
Umri na uenyekiti wapi na wapi mkuu??

Mbatia ni m/kiti NCCR nafikiri hana umri unaosema na kama anao basi kaufikisha jana na mugombea urais alikuwa DR Mvungi sijui huyu hata ana nafasi gani NCCR.

Mkuu mfano wako haupendizi hata kidogo kwani CVCM wao huchagua mwenyekiti baada ya kupita kiti cha Urais tena mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu. hao NCCR ndio kama hivyo sidhani kama Mbatia hakuchaguliwa against Dr. Mvungi ambaye alikuwa mwenyekiti hapo awali.

Kama unakumbuka niliwahi kuuliza ni utaratibu upi upo Chadema na kwa maelezo mengi ikiwa ni pamoja na Dr.Slaa mwenyewe.. nikinukuu baadhi ya majibu yake alizungumzia pia umri wa Zitto. Inaonyesha wazi Mbowe ndiye atasisi tena kugombea kiti cha Urais..
Ni utaratibu nisioukubali wala kuupendekeza lakini ndivyo ilivyo. Kwa hiyo pengine Zitto aligombea kiti hicho akitarajia kuwa mgombea wa chama kiti cha Urais...Na kama shieria inasema tofauti nashindwa kuelewa kwa nini Zitto alikubali ushauri wa wazee.
Na sii kweli wazee walikiuka sheria au katiba ya chama hata iwe mumuengua Zitto kwa sababu zipo taratibu ktk kila chaguzi. kama mnakumbuka yule mgombea wa Chadema Mbeya vijijini alienguliwa jina lake. Mgombea mwingine wa CCM akapita kwa makosa sawa na yule wa Mbeya lakini waheshimiwa hawakuyaona makosa hayo!..
Binafsi nilitegemea Zitto angesimama ngangari hadi chama kieleze kwa nini kimefikia hatua ya kuondoa jina lake lakini niliposikia Zitto mwenyewe kajiondosha.. then hatuna kesi.

Mkuu ukienda futa kesi mahakamani na mshtakiwa kaachiwa huru.. kisha ijulikane ulifanya hivyo kutokana na ushauri wa wazee.. Iweje sisi tuseme hao wazee walikiuka katiba au sheria ya nchi..Zitto alifuta kesi mwisho wa mazungumzo, kuendelea kuwalaumu viongozi wa Chadema hizi ni propaganda chafu..If anything wa kumlaumu ni Zitto, mimi binafsi sina makubwa zaidi ya kukubali matokeo isipokuwa nitawalaumu hao wapambe walokuja na JEURI YA KWAPA -kunuka bila kidonda! jeuri ambayo ilimpekea Zitto kubwabwaja ovyo..
 
 
No no no! Haya ya kum invoke Mungu hayana nafasi.

Unajua Tanzania na Afrika nzima kwa ujumla wangekuwa wanafikiri kama mimi tungekuwa mbali sana kimaendeleo. Basi tu....


common sense is not common......
 
 
Jamani Jamani msiwe wasahaulifu kiasi hicho... Mkapa kaiacha nchi kama Bush alivyoiacha Marekani...nchi ikiwa ktk matatizo makubwa ya Kiuchumi..

Reli ya kati ilikuwa haifanyi kazi, hatuna ndege wala shirika la ndege zaidi ya Precission tuliiona ktk daraja la Emirates, Umeme wa mgao tena kwa week, maji shida generator za watu binafsi zimetapakaa miji yote, visima vya maji ndio ilikuwa idara ya maji nchini..Mazao mikoani hayana maghala wala usafiri -magari yote makubwa safari zake ni Zambia, Congo na nchi za jirani kwa sababu hatukuwa na kitu kabisa cha kusafirisha nje..Hata mashirika ya ndege yalikata safari zake Tanzania kwa asilimia 50.. Kivukoni usafiri hakuna, mbuga ziliendelea kuuzwa, nyumba za serikali, mashirika yoote ya serikali yaliyobakia yalikuwa katika hali mbaya ajabu tukianza na hiyo Tanesco..Ni wakati watu waliweza kuiba hata BoT for christ sake!... BoT. Anayebisha hata moja hapo anifahamishe!.. jamanin haya hayakuwa maisha yetu na hali halisi ya Tanzania mwaka Dec 2004, jamani!
Leo mnakuja hapa na kusema JK ni mbovu kuliko woote waliotangulia!..Nooooo wakuu zangu hatumtendei haki hata kidogo. JK kasimamisha kazi zote za Mafisadi pamoja na kwamba hajawapeleka mahakamani. Kama angeachia yale yaliyokuwa yakitendeka toka wakati wa Mkapa hadi leo hii sijui tungebakiwa na kipi?

Binafsi sikubaliani na mtazamo huu ingawa nakubali kabisa kwamba JK ni msanii ana mapungufu mengi tu lakini sii kumweka kundi moja na viongozi waliotangulia..Trust me he is better of,
pamoja na kwamba hafai!
 

Kwani watu wasipiganie kubadilisha system ya kupata viongozi wa kuchaguliwa? System ya sasa haina check and balance. Na hilo ndilo tatizo kubwa.
 

Mkandara:

Kwa uchambuzi wangu finyu wa kisiasa, watanzania bado mnatafuta kiongozi atakayejichunga mwenyewe kama vile Nyerere. Viongozi kama hao ni wachache na kuwapata ni kucheza bahati nasibu.

Kinachotakiwa ni kuwepo kwa system ya check and balance. Kiongozi anaposhindwa basi kuwepo na vyombo vya kumuondoa na vilevile kuangalia utendaji wake wa kazi.

Kwa mfano hakuna nafasi ya uongozi katika CCM isiyohitaji kutoa chochote. Ukiambiwa gharama za mtu kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa vijana wa wilaya, wewe mwenyewe utashangaa. Kwa sababu mwenyekiti huyu anashiriki katika kura za maoni ya kuchagua mbunge.

Hivyo hata huyo shujaa wenu Mwakyembe, inawezekana amepita kwa kuhongahonga wilayani.

Na sasa kimefika kipindi karibu kila mtu amepata nafasi kwa kuonga. Je ni nani atakeyemnyooshea kidole mwenzake?
 
Mimi kura yangu nahifadhi mfukoni kwa sababu JK hanipi matumaini na wapinzani wananikoroga akili tu...hadi sasa hivi bado siwaelewi kabisa, labda aje mpinzani atakayegombea urais kupitia tiketi ya chama cha upinzani kitachotokea baada ya CCM kumegeka.
 
Mkuu mwanakijiji umerudi,afazali tumepumua kwa kukuona,maana tulihofu mafisadi ya ccm yasijekuwa yamekuteka.
Mkuu si kwa kikwete tuu bali ccm kwa jumla tuseme HAPANA
 
Nani anaweza kumfunda Lowasa aachane na mambo ya pesa ajikite kwenye uongozi wa nchi? Nani? Hilo likiwezekana basi anafaa. Hakuna kwenye upinzani. Wazuri bado wako hukohuko CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…