Niseme nini kisichojulikana? Alishinda kwa asilimia nyingi ya kura akijaza mioyo ya watanzania matumaini ya mwanzo mpya wa ujenzi wa taifa lao. Watu walitaraji mabadiliko. Walichopata badala yake ni mwendelezo wa sera ya uzembe, itikadi ya ufisadi na siasa za kubebana na ahadi za kuzugana. nchi yetu inastahili uongozi bora. Hatuitaji miaka mingine 5 ya viongozi walioshindwa. No 2nd term 4 kikwete. Yes i said it.
Mzee Mwanakijiji unajua kuna wakati watu wachache sana wanweza kuona hatari inayokuja mbele, na watu wachache zaidi wanaweza kuwashtua wenzao juu ya hiyo Tsunami inayokuja kama Nuhu alivyofanya wakati wa Gharika, kama Roti wakati wa Sodoma na Gomora.
Bw. George Bush Jr. alipokuwa anajiandaa kwenda kipindi cha pili cha Urais wake kuna Bw. Mmoja anaitwa Michael More (google) alimpinga vibaya sana, na aliwaonya wamarekani wasifanye kosa la kumchagua huyo mtu tena, alitengeneza Documentaries, alifanya interviews kwenye redio, Tv, Magazeti, aliandika makala na barua za wazi, lakini mwisho wa siku wamarekani wengi hawakumuelewa, wakamchagua tena George Bush.
Matokeo kila mtu ameyaona, sio tu ameiacha Marekani mahala pagumu bali ameiweka dunia nzima njia panda, inawayawaya kama mlevi, Dunia imekuwa ya mahangaiko, maisha yanapanda kila kukicha, hata Huko Kijijini kwangu nilikokuwa na uhakika angalau wa kunywa chai na magimbi au Viazi mambo yako tofauti.
Naamini ni watanzania wachache sana tunaokusikiliza, na wachache zaidi tunaokulewa, na watakuwa wachache zaidi watakao chukua hatua. Tumebaki na maswali yetu ya nani atabadili, kweli hakuna mtu kati ya watanzania wote tupatao mil.40 anayeweza kuongoza Vizuri kuliko JK?
Mimi nazidi kukupa Moyo, Mkuu nimekusikia, nakuelewa, nitachukua hatua, umekuwa Chachu kwangu umenichachusha. I am saying
"No 2nd Term 4 JK"