Time travel na Time Machine ni nini ?

Time travel na Time Machine ni nini ?

shalet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
3,430
Reaction score
3,547
Habari wakuu nazani nipo jukwaa sahihi kuna maswala machache yananichanganya sikumbuki lini nilisikia hili neno time travel nikawa interested kufuatili lakini nikaambulia kapa sijui ni lugha ilikuwa tatizo au ugumu wa suala lenyewe ninajua,

naomba mwenye uelewe anieleweshe vizuri what is time travel watu wanasema ninaweza post mwaka 20 june 2015 nikiwa leo au nikatravel back to the time kwamba naweza tuma meseji saa 2200 ikafika saa 2159 dakika moja kabla sijaituma,

nina video za you tube hazielezi vizuri hili suala kuna mifano mingi kutoka kwenye quran na bible mfano kwa mungu miaka 1000 ni sawa na siku moja,

karibuni kwa ufafanuzi
cc Monstgala
 
Last edited by a moderator:
Mkuu shalet, Heri ya mwaka mpya. "Time travel" na "time machine" hivi ni vitu viwili vinavyohusiana kwa maana kwamba muda pamoja na kuwa concept ngumu kabisa kueleweka tunautazama kama mstari wenye uelekeo i.e. past, present na future na kwakuwa tuna perception hiyo basi tunaweza kusema kwa nini kusiwe na uwezekano wa kusafiri kutoka katika present kwenda future au past? Ili usafiri kwenda mbele ya muda au nyuma utahitaji kifaa kitakachokuwezesha na hivyo time machine ndio kifaa hicho.

Hiyo ni kwa ufupi zaidi lakini tunaweza kuexpand mawazo haya kutegemeana na wapi hasa unataka kujikita ili kuelewa zaidi. Mfano katika ulimwengu maeneo tofauti yako katika vipindi tofauti vya muda, kuna nyota zilizo mbali sana na zinaweza kuwa ziko katika muda uliopita na ukifanikiwa kusafiri kwa kasi sana na kufika kule basi utakuwa umerudi nyuma ya muda. Hii ni sawa na kwamba nyota hizo tunavyoziona sasa ni jinsi zilivyokuwa miaka mamilioni yaliyopita.

Concept ya muda ndio inaweza kukufumbua macho zaidi kuhusu kusafiri katika vipindi vyake tofauti kwa kuwa pamoja na uhalisia tunaouona na kuufafanua muda ni sehemu ndogo tu ya ukweli wa muda wenyewe ni kitu gani. Kama binadamu tuko "programmed" kuuona muda jinsi tunavyouona na unapotoka kidogo katika program hii unaweza kushangaa ni jinsi gani muda ulivyo na hapo ndipo unaweza kupata picha ni jinsi gani unaweza kwenda katika vipindi tofauti theoretically na labda vipindi hivi vina-exist kwa pamoja i.e past, present na future ni sequences za muda zilizopo kwa wakati mmoja.
 
Dah Monstagala afadhali unerudi mkuu, niliyamiss sana madude yako humu ndani.
 
Kwa kufuata kanuni za Einstein za "Relativity", hakuna muda halisi na muda unategemeana na mwendokasi pamoja na nguvu za uvutano.

Kwa maana hiyo, kadiri unavyozidi kuongeza kasi, ndivyo unavyozidi kuupunguza upitaji wa muda.

Kwa sayansi za Einstein, ukiweza kufikia mwendokasi wa mwanga (299 792 458 m / s) unaweza kuusimamisha muda.

Kinadharia, ukiweza kupita mwendokasi wa mwanga, utaanza kurudi nyuma katika muda na kuweza kujiona wewe mwenyewe unavyokuja.

Nasema kinadharia kwa sababu katika uhalisi, kitu chochote chenye uzito, hata mdogo vipi, hakiwezi kufikia mwendokasi wa mwanga, kwa sababu kila kinavyozidi kukaribia mwendokasi wa mwanga ndivyo uzito wake unavyozidi kukaribia infinity, na kinadharia kitu chochote chenye uzito kikifikia mwendokasi wa mwanga kitakuwa na uzito usio na mwisho.

Kifupi, time travel (kurudi nyuma) kinadharia inawezekana. In fact kila siku ukipanda gari na kwenda mwendo kasi unapunguza kasi ya muda kupita. Kinadaharia, ukiwa umezaliwa na pacha wako hapa duniani, unaweza kumuacha hapa duniani na wewe ukapanda chombo kinachoenda kasi sana kwenda kwenye nyota za mbali, ukirudi, kwa sababu muda utakuwa unapita kwa polepole zaidi kwenye chombo kinachoenda kwa kasi (time dilation) unaweza kukuta pacha wako kazeeka ana mvi wakati wewe bado kijana.

For more on Relativistic time dilation and object contraction see Chapter 28 - ROL

The time dilation wiki is at Time dilation - Wikipedia, the free encyclopedia
 
mkuu MONSTGALA/MGALANJUKA nafurahi kukuona tena ukitema nondo hapa jukwaani baada ya kitambo kidogo kupita
welcome back mkuu
endelea kutulisha chakula cha ubongo

.made in mby city.
 
Asante NICOLAX, tuko pamoja.
 
Last edited by a moderator:
mkuu KIRANGA nashukuru kwa ufafanuzi wako pamoja na hizo link
huwa nafurahi sana tunapokua upande mmoja wa hoja na ww ila cyo kule kwenye PROVE BLAHBLAH IS/ISN'T BLAHBLAH

.made in mby city.

Those debates are equally stimulating if you apply yourself.
 
nina video za you tube hazielezi vizuri hili suala kuna mifano mingi kutoka kwenye quran na bible mfano kwa mungu miaka 1000 ni sawa na siku moja,

karibuni kwa ufafanuzi
cc Monstgala

"Miaka 1000 ni sawa na siku moja" Kuna kitu kizito katika phrase hiyo angalau kwa approach tofauti za sayansi juu ya muda. Unajua unapoangalia muda kisaikolojia basi lazima utajikuta unauona muda kama hali fulani inayo-flow hasa kwenda mbele bila ya kurudi nyuma. Yani muda uliopita ni halisi kwa kuwa kuna matukio yalifanyika na sasa hayawezi kuingiliwa- kwamba yameshatokea. Pia muda ulipo (sasa) ni halisi kwa kuwa kuna matukio yanayofanyika lakini kwa moda ujao (future) hauna uhalisia mpaka pale matukio yake yatakapofika basi utakuwa halisi - kwa maana hiyo tunahisi kwamba muda ujao (future) unaweza kuingiliwa na matukio yake kubadilishwa. Hii ni tensed theory ya muda na ndiyo inabeba au inashabihiana na psychological arrow of time. Lazima uwe na ubongo kutambua hali hii ndio maana inakuwa ni hali ya kisaikolojia.

Lakini nadharia nyingine haiendani sana na hii maana inauelezea muda kwa njia tofauti sana. Kwamba je muda unaflow? au kwa kiswahili kizuri muda unapita? Hapana muda haupiti wala hauendi popote. Muda kupita ni jambo la kufikirika na gumu kuelewa lakini kwa mifano rahisi unaweza kung'amua uhalisia wake. Kwa nini muda haupiti? au hau-flow kama tunavyohisi na kuona kisaikolojia? Kama muda unapita basi lazima kuwe na spidi au mwendo wake halisi usiobadilika hata kunapokuwa hakuwa reference scale. Reference scale ni matukio au vitu vinavyosaidia kuona/kupima tofauti ya muda mfano saa, mzunguko wa Jua, events au hata sisi binadamu wenyewe etc. Yani muda bila vipimo je upo? Ni kitu halisi pale kunapokuwa hakuna chochote kinachotukia?

Pasipo na time reference basi muda hauendi wala haurudi. Ile "sasa" inabaki hapo hapo maana hakuna tukio na hii tayari inasambaratisha wazo la kuwa muda ni kitu kinacho-flow hivyo kama nje ya universe pasipo na chochote muda hauendi na hii ni sawa na kwamba muda kwenda ni matokeo ya sisi kuwa na reference objects ambazo kwazo tunahisi hii flow.

Hii ni nadharia ya tenseless na inapendekeza kwamba past, present na future zinatokea kwa pamoja na vipindi vyote hivi vya muda ni halisi. Nadharia inawakilisha muda kwa mapana zaidi kuliko ile ya kwanza na hapa ndipo hii phrase ya "Miaka 1000 ni sawa na siku moja" kwamba tunavyouona muda kama binadamu wenye ulimwengu kama reference ni tofauti na muda wenyewe ulivyo kwamba past, present na future ni illusion kama Eistein alivyosema. Na relativity theory inachangia nadharia hii kwamba "reality is relative" kwa maana ya kwamba kila kitu kinapata uhalisia au kinaweza kufafanuliwa kwa kuwa na reference ya vitu vingine ulimwenguni.

Naweza kukupa mifano zaidi kuhusu uhalisia wa mambo unavyotegemea reference.
 
Hii ni sawa na kwamba nyota hizo tunavyoziona sasa ni jinsi zilivyokuwa miaka mamilioni yaliyopita.
Heri ya mwaka mpya kwako pia, nimeanza kupata idea kidogo kuhusu jinsi tunaziona nyota nazani kuna thread yako moja niliisoma inahusu mambo hayo lakini katika hali ya kawaida tunaona matukio haya reverse mfano ukuaji wa miti kitu kupata kutu au maisha yetu yenyewe hayarudi nyuma kwamba ukizaliwa unakua unazeeka na unakufa na kama backward time trvael inawezekana je mtu unaweza kurudi ukayazuia baadhi ya matukio yalikwisha tokea,
shukrani,
 
Kwa kufuata kanuni za Einstein za "Relativity", hakuna muda halisi na muda unategemeana na mwendokasi pamoja na nguvu za uvutano.

Kwa maana hiyo, kadiri unavyozidi kuongeza kasi, ndivyo unavyozidi kuupunguza upitaji wa muda.

Kwa sayansi za Einstein, ukiweza kufikia mwendokasi wa mwanga (299 792 458 m / s) unaweza kuusimamisha muda.

Kinadharia, ukiweza kupita mwendokasi wa mwanga, utaanza kurudi nyuma katika muda na kuweza kujiona wewe mwenyewe unavyokuja.

Nasema kinadharia kwa sababu katika uhalisi, kitu chochote chenye uzito, hata mdogo vipi, hakiwezi kufikia mwendokasi wa mwanga, kwa sababu kila kinavyozidi kukaribia mwendokasi wa mwanga ndivyo uzito wake unavyozidi kukaribia infinity, na kinadharia kitu chochote chenye uzito kikifikia mwendokasi wa mwanga kitakuwa na uzito usio na mwisho.

Kifupi, time travel (kurudi nyuma) kinadharia inawezekana. In fact kila siku ukipanda gari na kwenda mwendo kasi unapunguza kasi ya muda kupita. Kinadaharia, ukiwa umezaliwa na pacha wako hapa duniani, unaweza kumuacha hapa duniani na wewe ukapanda chombo kinachoenda kasi sana kwenda kwenye nyota za mbali, ukirudi, kwa sababu muda utakuwa unapita kwa polepole zaidi kwenye chombo kinachoenda kwa kasi (time dilation) unaweza kukuta pacha wako kazeeka ana mvi wakati wewe bado kijana.

For more on Relativistic time dilation and object contraction see Chapter 28 - ROL

The time dilation wiki is at Time dilation - Wikipedia, the free encyclopedia

Mkuu kirnaga heri ya mwaka mpya, kama muda tunaona unaflow kutokana na matukio je kusimamisha muda ni sawa na kusimamisha matukio yote yasitokee.
 
"Miaka 1000 ni sawa na siku moja" Kuna kitu kizito katika phrase hiyo angalau kwa approach tofauti za sayansi juu ya muda. Unajua unapoangalia muda kisaikolojia basi lazima utajikuta unauona muda kama hali fulani inayo-flow hasa kwenda mbele bila ya kurudi nyuma. Yani muda uliopita ni halisi kwa kuwa kuna matukio yalifanyika na sasa hayawezi kuingiliwa- kwamba yameshatokea. Pia muda ulipo (sasa) ni halisi kwa kuwa kuna matukio yanayofanyika lakini kwa moda ujao (future) hauna uhalisia mpaka pale matukio yake yatakapofika basi utakuwa halisi - kwa maana hiyo tunahisi kwamba muda ujao (future) unaweza kuingiliwa na matukio yake kubadilishwa. Hii ni tensed theory ya muda na ndiyo inabeba au inashabihiana na psychological arrow of time. Lazima uwe na ubongo kutambua hali hii ndio maana inakuwa ni hali ya kisaikolojia.

Lakini nadharia nyingine haiendani sana na hii maana inauelezea muda kwa njia tofauti sana. Kwamba je muda unaflow? au kwa kiswahili kizuri muda unapita? Hapana muda haupiti wala hauendi popote. Muda kupita ni jambo la kufikirika na gumu kuelewa lakini kwa mifano rahisi unaweza kung'amua uhalisia wake. Kwa nini muda haupiti? au hau-flow kama tunavyohisi na kuona kisaikolojia? Kama muda unapita basi lazima kuwe na spidi au mwendo wake halisi usiobadilika hata kunapokuwa hakuwa reference scale. Reference scale ni matukio au vitu vinavyosaidia kuona/kupima tofauti ya muda mfano saa, mzunguko wa Jua, events au hata sisi binadamu wenyewe etc. Yani muda bila vipimo je upo? Ni kitu halisi pale kunapokuwa hakuna chochote kinachotukia?

Pasipo na time reference basi muda hauendi wala haurudi. Ile "sasa" inabaki hapo hapo maana hakuna tukio na hii tayari inasambaratisha wazo la kuwa muda ni kitu kinacho-flow hivyo kama nje ya universe pasipo na chochote muda hauendi na hii ni sawa na kwamba muda kwenda ni matokeo ya sisi kuwa na reference objects ambazo kwazo tunahisi hii flow.

Hii ni nadharia ya tenseless na inapendekeza kwamba past, present na future zinatokea kwa pamoja na vipindi vyote hivi vya muda ni halisi. Nadharia inawakilisha muda kwa mapana zaidi kuliko ile ya kwanza na hapa ndipo hii phrase ya "Miaka 1000 ni sawa na siku moja" kwamba tunavyouona muda kama binadamu wenye ulimwengu kama reference ni tofauti na muda wenyewe ulivyo kwamba past, present na future ni illusion kama Eistein alivyosema. Na relativity theory inachangia nadharia hii kwamba "reality is relative" kwa maana ya kwamba kila kitu kinapata uhalisia au kinaweza kufafanuliwa kwa kuwa na reference ya vitu vingine ulimwenguni.

Naweza kukupa mifano zaidi kuhusu uhalisia wa mambo unavyotegemea reference.
nashukuru sana nimeanza kupata mwanga sasa juu ya muda na maelezo yanaeleweka hapo bolded ni muhimu pia ukipata nafasi thanks,
 
Mkuu kirnaga heri ya mwaka mpya, kama muda tunaona unaflow kutokana na matukio je kusimamisha muda ni sawa na kusimamisha matukio yote yasitokee.

Muda, kama nilivyosema hapo juu, si mmoja kwa matukio yote.

Hili si wazo jepesi kulielewa.

Muda unategemea na mwendokasi wa kitu, pamoja na nguvu za uvutano.

Kitu chenye mwendokasi mkubwa, kwa sababu ya mwendokasi huo, kinapunguza kasi ya kipita kwa muda.

Kitu ambacho kipo katika nguvu ya uvutano kubwa sana (kwa mfano karibu na nyota kama jua, au karinu na "black hole") kinapunguza kasi ya kipita kwa musa.

Kujibu swali lako, kusimamisha muda ni kusimamisha matukio yote kwa kile kitu kilichosimamisha muda, lakini hilo halina maana matukio yote yatasimama kwa ulimwengu wote. Matukio yataendelea ulimwenguni, lakini kwa kile kitu kilichosimamisha muda, muda utakuwa umesimama, na hivyo matukio yote yatasimama.

Nikirudi kwenye mfano wa mapacha wawili waliozaliwa siku moja, halafu walipofika miaka kumi Kulwa akapanda starship iliyokwenda kwa kasi ya mwanga (ukienda kwa kasi ya mwanga unasimamisha muda, hii haiwezekani kama nilivyoonyesha hapo juu ila natumia kama mfano kujibu seali lako). So Kulwa akisafiri kwa muda wa miaka 50 kwa mujibu wa Doto, alirudi duniani atamkuta Doto ana miaka 60 wakati Kulwa atakuwa na miaka ile ile 10.

Kwa Kulwa, matukio yote yatasimama. Kwa Doto na wengine wote duniani, matukio yataendelea kama kawaida.
 
Kwa kufuata kanuni za Einstein za "Relativity", hakuna muda halisi na muda unategemeana na mwendokasi pamoja na nguvu za uvutano.

Kwa maana hiyo, kadiri unavyozidi kuongeza kasi, ndivyo unavyozidi kuupunguza upitaji wa muda.

Kwa sayansi za Einstein, ukiweza kufikia mwendokasi wa mwanga (299 792 458 m / s) unaweza kuusimamisha muda.

Kinadharia, ukiweza kupita mwendokasi wa mwanga, utaanza kurudi nyuma katika muda na kuweza kujiona wewe mwenyewe unavyokuja.

Nasema kinadharia kwa sababu katika uhalisi, kitu chochote chenye uzito, hata mdogo vipi, hakiwezi kufikia mwendokasi wa mwanga, kwa sababu kila kinavyozidi kukaribia mwendokasi wa mwanga ndivyo uzito wake unavyozidi kukaribia infinity, na kinadharia kitu chochote chenye uzito kikifikia mwendokasi wa mwanga kitakuwa na uzito usio na mwisho.

Kifupi, time travel (kurudi nyuma) kinadharia inawezekana. In fact kila siku ukipanda gari na kwenda mwendo kasi unapunguza kasi ya muda kupita. Kinadaharia, ukiwa umezaliwa na pacha wako hapa duniani, unaweza kumuacha hapa duniani na wewe ukapanda chombo kinachoenda kasi sana kwenda kwenye nyota za mbali, ukirudi, kwa sababu muda utakuwa unapita kwa polepole zaidi kwenye chombo kinachoenda kwa kasi (time dilation) unaweza kukuta pacha wako kazeeka ana mvi wakati wewe bado kijana.

For more on Relativistic time dilation and object contraction see Chapter 28 - ROL

The time dilation wiki is at Time dilation - Wikipedia, the free encyclopedia

Mkuu kuna movie Mpya inahusu hayo mambo jamaa alimuacha binti yake Duniani akaenda anga za juu na alimuahidi bintiye akirejea watakuwa umri sawa... Alipokuwa juu ya anga aliweza kuenya kwenye black hole kwa muda mfupi ambapo kama angezunguka basi angetumia miaka kadhaa... na aliporejea Duniani bintiye alikuwa na umri zaidi yake... Sayansi hii inaonesha ukiwa anga za juu mabadiliko ya mwili ni kidogo mno almost no kuzeeka.. Pengine ndio maana watu wa Dini husema Mbinguni huzeeki no kula no matatizo... Movie hiyo niliitizama inaitwa Interstaller

Yeah, hiyo movie nataka kuiangalia, nimeambiwa ni nzuri sana.

Idea uliyoisema ndiyo hiyo hiyo niliyoielezea hapo juu.

Yote yametoka katika Einsteins theory of relativity. Ukitaka kuelewa time travel soma vizuri Einsteins theory of relativity.

Misingi yake mikuu ni.

1. Muda si kitu fixed, vitu tofauti vinaona muda unapita kwa kasi tofauti kitegemeana na mwendokasi na uvutano. Unavyozidi kuongeza mwendokasi au uvutano unapunguza kasi ya upitaji wa muda.Time dilation.

2. Uzito si kitu fixed. Kitu kimoja kinaweza kuwa na uzito tofauti kutegemea na mwendokasi au uvutano. Unavyozidi kuongeza mwendokasi au uvutano inazidi kuongeza uzito.

3. Ukubwa si kitu fixed. Kitu kimoja kinaweza kuwa na ukubwa tofauti kutegemea na mwendokasi au uvutano. Unavyozidi kuongeza mwendokasi au uvutano ndivyo unavyozidi kuongeza ukubwa wa kitu.

4. Kadiri ya kitu chochote chenye uzito kinavyozidi kukaribia mwendokasi wa mwanga, ndivyo ukubwa wake ma uzito wake unavyozidi kukaribia infinity.

5. Kuufikia mwendokasi wa mwanga ni sawa na kuusimamisha muda kwa hicho kikichoufikia mwendokasi wa mwanga.

6. Kuupita mwendikasi wa mwanga ni sawa na kurudi nyuma katika muda kwa hicho kilichoupita mwendokasi wa mwanga.

7. Kwa kuwa tushaona katika 4 hapo juu kwamba kwa chochote chenye uzito, hata uwe mdogo vipi, kuufikia mwendokasi wa mwanga ni kama sawa na uzito wa hicho chochote kufikia infinity, tutahitaji infinity energy kusogeza kidogo tu uzito huu, seuze kuusogeza katika mwendokasi wa mwanga. Kwa maneno mengine, haiwezekani kuufikia mwendokasi wa mwanga.

8. Kama haiwezekani kuufikia mwendokasi wa mwanga, haiwezekani kurudi nyuma katika muda, kwa sababu ili kurudi nyuma katika muda inatubidi sio tu tuufikie mwendokasi wa mwanga, bali pia tuupite.

9. Kuna habari Einstein aliziita "spooky action at a distance" ambazo zinaonyesha kuna uwezekano wa mahusiano ya mwendokasi mkubwa kuliko mwanga, lakini mahusiano haya hayawezi kutumika kutuma habari zozote. Ni kama random action tu.

10. The next frontier is teconciling Einsteins relativity with Quantum theory.
 
Last edited by a moderator:
Muda, kama nilivyosema hapo juu, si mmoja kwa matukio yote.

Nikirudi kwenye mfano wa mapacha wawili waliozaliwa siku moja, halafu walipofika miaka kumi Kulwa akapanda starship iliyokwenda kwa kasi ya mwanga (ukienda kwa kasi ya mwanga unasimamisha muda, hii haiwezekani kama nilivyoonyesha hapo juu ila natumia kama mfano kujibu seali lako). So Kulwa akisafiri kwa muda wa miaka 50 kwa mujibu wa Doto, alirudi duniani atamkuta Doto ana miaka 60 wakati Kulwa atakuwa na miaka ile ile 10.

Kwa Kulwa, matukio yote yatasimama. Kwa Doto na wengine wote duniani, matukio yataendelea kama kawaida.
kweli muda sio suala rahisi kueleweka lakini nashukur nimepata mwanga kwenye bold ngonya nicheki clip ya mkuu hapo chini kama nitakuwa na swali nitakuja tena thanks
 
Back
Top Bottom