Time travel na Time Machine ni nini ?

Time travel na Time Machine ni nini ?

Habari wakuu nazani nipo jukwaa sahihi kuna maswala machache yananichanganya sikumbuki lini nilisikia hili neno time travel nikawa interested kufuatili lakini nikaambulia kapa sijui ni lugha ilikuwa tatizo au ugumu wa suala lenyewe ninajua,

naomba mwenye uelewe anieleweshe vizuri what is time travel watu wanasema ninaweza post mwaka 20 june 2015 nikiwa leo au nikatravel back to the time kwamba naweza tuma meseji saa 2200 ikafika saa 2159 dakika moja kabla sijaituma,

nina video za you tube hazielezi vizuri hili suala kuna mifano mingi kutoka kwenye quran na bible mfano kwa mungu miaka 1000 ni sawa na siku moja,

karibuni kwa ufafanuzi
cc Monstgala

Its strictly prohibited to travel back in time, kwa sababu binadam tutafanya mambo ya ajabu sana

Mfano unaonaje mtu akarudi nyuma na muda akaenda kuwauwa mitume wote.

Ninachoweza fikili kama man kind wataweza ku crack hii puzzle basi hata uki move back in time the time its self will not allow you to disturb the events.

But travel to the future is possible ukiweza kucross kwenye at the fronts of black hole,it will be ur ticket to future
 
Mkuu kirnaga heri ya mwaka mpya, kama muda tunaona unaflow kutokana na matukio je kusimamisha muda ni sawa na kusimamisha matukio yote yasitokee.

Nafikili muda ni kitu kinachojitegemea.
 
nimekumbuka movie ya superman the move
nna uhakika CERN wanaielewa vyema time ....
 
hii habari ya kuwa na umri sawa na mwanao inahitaji mtu awe dip sana kuielewa.
 
wajuzi njoeni hapa tafadhali....natamani kurudi past hata nkaone. show ya michael jackson 1995
 
Time travel&time machine wala sio concepts ngumu kuzielewa
In Einsteinian kinematics,kitu chochote chenye speed kubwa kuliko zero ni Time machine kwasababu kinauwezo wa dilate mda,

Hata train inaweza kutumika kama time machine device as long as ipo kwenye uniform motion

That's corollary of constancy of the speed of light
 
Habari wakuu nazani nipo jukwaa sahihi kuna maswala machache yananichanganya sikumbuki lini nilisikia hili neno time travel nikawa interested kufuatili lakini nikaambulia kapa sijui ni lugha ilikuwa tatizo au ugumu wa suala lenyewe ninajua,

naomba mwenye uelewe anieleweshe vizuri what is time travel watu wanasema ninaweza post mwaka 20 june 2015 nikiwa leo au nikatravel back to the time kwamba naweza tuma meseji saa 2200 ikafika saa 2159 dakika moja kabla sijaituma,

nina video za you tube hazielezi vizuri hili suala kuna mifano mingi kutoka kwenye quran na bible mfano kwa mungu miaka 1000 ni sawa na siku moja,

karibuni kwa ufafanuzi
cc Monstgala
Katuni ya Mr. Peabody na Sherman inakuhusu.......
 
Ndio maana viongozi wa dini huwa wanasema peponi ni kula bata mwanzo mwisho kumbe walishajua kule hatuzeeki, umri unaganda kama wa Wema Sepetu na Juma Kaseja.
Maana tangu nipo darasa la pili naambiwa wanana 24 yrs na mm sasa nakaribia 27.
 
Kwa kufuata kanuni za Einstein za "Relativity", hakuna muda halisi na muda unategemeana na mwendokasi pamoja na nguvu za uvutano.

Kwa maana hiyo, kadiri unavyozidi kuongeza kasi, ndivyo unavyozidi kuupunguza upitaji wa muda.

Kwa sayansi za Einstein, ukiweza kufikia mwendokasi wa mwanga (299 792 458 m / s) unaweza kuusimamisha muda.

Kinadharia, ukiweza kupita mwendokasi wa mwanga, utaanza kurudi nyuma katika muda na kuweza kujiona wewe mwenyewe unavyokuja.

Nasema kinadharia kwa sababu katika uhalisi, kitu chochote chenye uzito, hata mdogo vipi, hakiwezi kufikia mwendokasi wa mwanga, kwa sababu kila kinavyozidi kukaribia mwendokasi wa mwanga ndivyo uzito wake unavyozidi kukaribia infinity, na kinadharia kitu chochote chenye uzito kikifikia mwendokasi wa mwanga kitakuwa na uzito usio na mwisho.

Kifupi, time travel (kurudi nyuma) kinadharia inawezekana. In fact kila siku ukipanda gari na kwenda mwendo kasi unapunguza kasi ya muda kupita. Kinadaharia, ukiwa umezaliwa na pacha wako hapa duniani, unaweza kumuacha hapa duniani na wewe ukapanda chombo kinachoenda kasi sana kwenda kwenye nyota za mbali, ukirudi, kwa sababu muda utakuwa unapita kwa polepole zaidi kwenye chombo kinachoenda kwa kasi (time dilation) unaweza kukuta pacha wako kazeeka ana mvi wakati wewe bado kijana.

For more on Relativistic time dilation and object contraction see Chapter 28 - ROL

The time dilation wiki is at Time dilation - Wikipedia, the free encyclopedia
u r gud, thank u
 
hii kali,katika topic ambazo nazipitaga bila kuzisoma ndo hii za time travel ,time machine,kumbe kuna mambo yakufikirisha
 
time travel zipo kwenye filamu tu. kiuhalisia mpaka sasa bado kuna wanasayansi wanafanya tafiti na bado hawajaweza kupata theory ya kusapoti time travel.
 
Back
Top Bottom