Time travel na ufunuo wa ufufuko

Najaribu kukuelewa hapa lakini kuna ukakasi kwenye dhana nzima ya time travel hasa linapokuja suala la time synchronization between real time and fantasy time... I mean psychological time... Backward and future while at very present in a single live body
Kwamba mwili mmoja katikati ya wakati halisi je unawezaje kusafiri kifikra hata kama ni ndotoni na Kuishi miaka kenda nyuma ama kuutangulia wakati na kufanya prediction ya yajayo? Nadhani unaipata point yangu hapa
 
Sijakuelewa

Umesema chanzo cha binadamu kuwa na rangi tofauti ni uoto asili, mazingira nk.
Nikauliza mbona uoto asili na mazingira bado yapo lakini hayafanyi binadamu wabadilike rangi.
Yaani mchina awe mwafrika kutokana na kukaa mazingira ya Africa.
Au mwafrika awe mwarabu kutokana na kwenda kuishi Jangwani
 
Nazungumzia chimbuko.... Hayo uliyotaja yote ni matawi
 
Nazungumzia chimbuko.... Hayo uliyotaja yote ni matawi
Hebu fafanua zaidi kipi ni chimbuko na kipi ni matawi kwa sababu swali langu liko kwenye muktadha ule ule niliouliza mara ya kwanza.
 
Hebu fafanua zaidi kipi ni chimbuko na kipi ni matawi kwa sababu swali langu liko kwenye muktadha ule ule niliouliza mara ya kwanza.
Kila jamii unayoiona leo hii ni matawi... Chimbuko lao ni la asili walipotokea kutokana na hali ya hewa mazingira na uoto wa asili
Wanaoishi kwenye baridi kali ya barafu hawawezi kamwe wakafanana na wanaoishi jangwani kwenye joto kali nk... Hivyo asili na chimbuko ndio viliamua aina ya wakazi watakaomudu mazingira husika.. Na si binadamu tu mpaka wanyama na wadudu....
Baada ya hapo waliozaliwa wote ni matawi toka kwenye chimbuko husika
 
wakati halisi je unawezaje kusafiri kifikra hata kama ni ndotoni na Kuishi miaka kenda nyuma ama kuutangulia wakati na kufanya prediction ya yajayo? Nadhani unaipata point yangu
Kama ntakuwa nimekuelewa, unazungumza kuyaona mambo yajayo na wakati huo huo, kusafiri kwa wakati kimwili.
Time travel, kimsingi hii ni nadharia yenye kutafuta uwezekano wa mtu kurudi nyumba au kwenda mbele kwa wakati kimwili pasipo kuathili hali ya mwili ya sasa.
Lakini kusafiri ndotoni ni tofauti na nadharia ya time travel kwa sababu ndotoni: kuyaona mambo ya mbele, ni suala la roho - ndoto zisizo kawaida. Hizi Hazihusiani na kusafiri kimwili. Aidha, muda wa ndotoni hauwezi kupimwa. Lakini nadharia ya time travel muda unapimwa.
Hatahivyo kuna ndoto za kawaida, akili. Matukio ya kila siku katika maisha na Mawazo. Hapa ndiyo utaona unasafiri kimawazo kurudi nyuma au kwenda mbele kimawazo, bado mwili hauhusiki.
Kwahiyo basi ndotoni tunaona maisha tutakayoishi, na ukweli wa badae. Pia mambo yatakayotukia maishani wakati tunaishi maisha ya mwili. Hatusafiri na kuishi miaka au miezi au saa au dakika kadhaa kurudi nyumba au kwenda mbele kwa wakati kimwili, isopokuwa kwa roho tuna-predict yajayo.
 
Nikiwa kijana by then wa miaka 20 niliota ndoto... Ndoto zile tunaita vivid dreams... Nilijiona napitia maisha yajayo mpaka umri wa miaka 80 na ya kwamba hapo ndio kitakuwa kikomo changu... Nitakufa...
Ni kama vile naishi hii ndoto katika maisha halisi... Nilipoanza kujifunza haya mambo ya kiroho nikakutana na kitabu cha LIAO FAN'S FOUR LESSONS... YOU CAN CHANGE YOUR DESTINY.... Nikajikuta kama najisoma

Huwa naikumbuka hii ndoto na huu uhalisia na muingiliano wa halisi na kufikirika ama kuwazika.... Kuna nini kati yake
 
Kiukweli ulichoandika ni kweli kabisa. Wapo watu wanaoota maisha yao yote yatakavyo kuwa hapa duniani.
Shida kubwa huwa ni kutafsiri na kuelewa hizo ndoto. Kwa kweli ukifanikiwa kuelewa ndoto kama hii uliyisema hapa, unakuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kuishi.
Pia, fahamu wapo watu wanaoweza kuongea na watu waliokufa kuhusu mambo yanayokuja kwenye maisha yao.
Kwa hiyo mimi nakuelewa sana unachosema ndugu Mshana Jr.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…