Hili ni swali gumu kwakuwa hata ukiniuliza muda nini nitashindwa kukujibu... Lakini naweza kusema tu ya kwamba muda ni saa (sio ya kuvaa mkononi) muda ni dakika muda ni sekunde muda ni wakati na muda ni nyakati
Safi kabisa,ngoja nikuwekee baadhi ya maandiko yanayozungumzia muda,kisha nitakwambia muda ni nini na vipi unatambulika.
Anasema Allah aliye juu :
1. Naapa kwa Zama!
2. Hakika binaadamu bila ya shaka yumo katika khasara,
3. Ila wale walio amini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri. (al 'Asr : 1 - 3)
Akasema tena :
43. Je! Huoni ya kwamba Mwenyezi Mungu huyasukuma mawingu, kisha huyaambatisha, kisha huyafanya mirundi? Basi utaona mvua ikitoka kati yake. Na huteremsha kutoka juu kwenye milima ya mawingu mvua ya mawe, akamsibu nayo amtakaye na akamuepusha nayo amtakaye. Hukurubia mmetuko wa umeme wake kupofua macho.
44. Mwenyezi Mungu hubadilisha usiku na mchana. Hakika katika hayo yapo mazingatio kwa wenye kuona. (an Nur : 43 - 44)
N akasema Mola mtukufu :
1. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi, na akafanya giza na mwangaza. Tena baada ya haya walio kufuru wanawafanya wengine sawa na Mola wao Mlezi. (al An'am : 1)
Akasema tena Mola wetu mlezi :
36. Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya Mwenyezi Mungu tangu alipo umba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko mine mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo. Na piganeni na washirikina wote kama wao wnavyo pigana nanyi nyote. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu. ( at Tawbah : 36 )
Akasema tena Allh aliye juu :
33. Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea. ( al Anbiyai : 33 )
Ukisoma maandiko hayo huku ukiwa unatafakari utajua muda ni nini na ni nini kinakujukisha muda.
Narudi kukupa hitimisho la muda ......