Simulizi la Adamu, ukisoma utaona Adamu anafanya kosa. Nasi tunaitwa Mwanadamu/Wanadamu - uzao wa Adamu. Maana yake ni kwamba kutoka kwa Adamu tumerithi kosa alilolifanya.
Ukisoma Historia inaonyesha ya kuwa Adamu aliomba msamaha na akasamehewa,na hakuna mja kubeba mzigo wa mwingine,hakuna kurithi katika dhambi,na Mola aliye juu anasema :
18. Na mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Na aliye topewa na mzigo wake akiomba uchukuliwe hautachukuliwa hata kidogo, na angamwomba jamaa yake. Hakika wewe unawaonya wale wanao mcha Mola wao Mlezi kwa ghaibu, na wanashika Sala. Na anaye jitakasa, basi anajitakasa kwa ajili ya nafsi yake. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu. ( Faatir : 18)
Pili,jalia kama kweli tumerithi,je ni kosa gani ambalo tumelirithi ni lile la kula tunda ? Lakini mbona Adamu aliomba msamaha na akasamehewa ? Na kwanini tulirithi kosa ambalo sisi hatukulifanya ?
Utakatifu na asili ya Mungu kwa Adamu iliharibiwa na Adamu. Nasi uzao wake tumerithi uharibifu wa Adamu.
Mwanadamu daima yupo katika hasara isipokuwa wale kuhusiana kuhusu subira na kufanya mema. Mola aliyajua yote haya na uhuru ulikuwa kwa Adamu na akili na tahadhari alipewa kama ilivyo kwetu,kwahiyo kukosea ni katika maumbile ndio maana kuna moto na kuna pepo,na mbora kati mwanadamu ni yule mwenye kukosea kisha akatubia.
Nakuuliz swali,nani alikwambia kwamba sisi tumerithi kosa alilotenda Adamu ? Je ni Yesu alisema maneno hayo au nani alisema maneno hayo ?
Ndugu yangu, watangulizi wako ni Adamu.
Kuhusu swali lako la kwanza. Nakusihi nenda google, andika "ugunduzi wa maandishi". Pia search kabla ya ugunduzi wa maandishi utapata majibu yako.
Kaka ushawahi kusoma Elimu ya uhakiki wa habari ?
Mimi kama habari hazina "Sanadi" yaani "Chain" ya wapokezi mpaka kwa wenye maandiko yenyewe habari hiyo huwa inakosa utahibiti na huwa naishusha daraja ya kuwa Kweli,mpaka iwe na chain iliyoshikana.
Vipi niangalie ugunduzi wa Maandishi wakati Adamu alifunzwa majina ya kila kitu ?