Time travel na ufunuo wa ufufuko

Mashaka yangu ni kwamba, unatafsiri na kuelewa maandiko matakatifu: Biblia na Quran kama elimu ya historia. Kama unafikiri maandiko matakatifu ni historia unapotoka.
Ni makosa kuelewa moja kwa moja na wakati wote kwamba, Quran na Biblia ni elimu ya historia.
Hivi vitabu ni teolojia na siyo elimu ya historia. Kila simulizi katika Biblia au Quran linakusudia teolojia: Mungu na mwanadamu.
 
. Nani wa kwanza kuandika Historia ya mtu wa kwanza ? Na ilikuwa lini ?
2. Je kwanini tuizingatie historia ya mtu wa kwanza na kuifanya hoja ? Ni upi ukweli wake ?
3. Historia inasemaje kuhusu mtu wa kwanza kuumbwa na ilijuaje hilo ?
Simulizi la Adamu, ukisoma utaona Adamu anafanya kosa. Nasi tunaitwa Mwanadamu/Wanadamu - uzao wa Adamu. Maana yake ni kwamba kutoka kwa Adamu tumerithi kosa alilolifanya.
Utakatifu na asili ya Mungu kwa Adamu iliharibiwa na Adamu. Nasi uzao wake tumerithi uharibifu wa Adamu.
Ndugu yangu, watangulizi wako ni Adamu.
Kuhusu swali lako la kwanza. Nakusihi nenda google, andika "ugunduzi wa maandishi". Pia search kabla ya ugunduzi wa maandishi utapata majibu yako.
Maswali yako: la pili na tatu. Tafadhali jifunze elimu ya historia na sayansi ya historia ya mwanadamu.
 
Ndugu,hakika ukinenacho ni sahihi mara dufu.Mimi pia nimewahi kulipa kipaumbele jambo hili.Mimi nilienda mbali zaidi kwa kuona kufa au kutokufa ni jambo la hiari.
 
Ndugu,hakika ukinenacho ni sahihi mara dufu.Mimi pia nimewahi kulipa kipaumbele jambo hili.Mimi nilienda mbali zaidi kwa kuona kufa au kutokufa ni jambo la hiari.
Nina hizo hisia pia.. Halafu naona kuna siku wafu wote watafufuka sio kiimani la hasha bali katika uhalisia wake
 
Nimekujibu hivi: umbile ni kadiri ya kuonekana. Tunatambua umbile kwa kuonekana. Nje ya hapo ni vigumu kutambua umbile.
Kaka swaki langu bado liko pale pale,je kuna roho bila umbile ?

Unaposema Mola ni roho kisa hujamuona huu ni uongo,sababu Mola ana umbile,ila kwa utaratibu wake hajaweka au hajatufanya tuweze kumuona tukiwa duniani,ila huko peponi tuta muona kama tuonavyo jua la saa sita mchana,yaani hakuna atakae mwambia mwenzie "Embu sogea na mimi nimuone" ,yaani kila mtu anamuona.
Uhusiano upo ila hakuna kufanana hata kwa bahati mbaya.
 
Huoni kama unajijibu?
Hapa wote tupo duniani na Mungu hajajifunua kwetu wazi wazi.
Sasa kitu ambacho hakijajifunua wazi unawezaje kujua umbo lake, hata kama kina umbile?
 
Uhusiano upo ila hakuna kufanana hata kwa bahati mbaya.
Wewe upo kwa sababu walikuwepo watangulizi wako, wazazi.
Unakataa kwamba hufanani na watangulizi wako? Tukichunguza mwili wako na pia wazazi wako tutakuta mnafanana baadhi ya viungo au mwonekano.
Lakini pia tabia. Tukitazama tabia yako hatutaona ikitofautina na watangulizi wako.
 
Jaman time travel ni jambo la kutaalam kidogo sasa naona bahadhi wana lazimisha vitu
 
Na tunfanye mwanadamu kwa mfano wetu (WETU)???!!??!) LAKIN ni kabla ya adam ajala tunda.
 
Nimekujibu hivi: umbile ni kadiri ya kuonekana. Tunatambua umbile kwa kuonekana. Nje ya hapo ni vigumu kutambua umbile.
Ndio maana nikauliza kwamba kuna roho bila umbile ? Jibu sahihi ni kuwa hakuna roho bila umbile,ile si kila umbile mwanadamu unaweza kuliona,kuna mipaka na wakati mahususi.
Hivyo simulizi la Adamu siyo ushahidi kwamba Adamu ndiyo alikuwa mtu wa kwanza kuumbwa.
Kujua hilo, utaona kwamba simulizi la Adamu ni la wakati wa baberi. Inakadiriwa kama miaka 500 hivi kabla ya Kristo.
Kwanza sio "Baberi" sahihi ni "Babeli" au "Baabili".

Pili,kuwepo simulizi hilo hakuonyeshi ya kuwa Adamu si mtu wa kwanza kuimbwa,bado hujaonyesha ushahidi huo. Na nani alisimulia simulizi hilo kwa mara ya kwanza ?

Sababu bado hujaonyesha ushahidi wa kuonyesha Adamu sio mtu wa kwanza,nakusaidia kwa mtindo huu,ni nani mtu wa kwanza ? Kama humjui kwanini ujengee hoja kitu usicho kijua ?

Unaweza kuniambia kitambo cha umri kutoka Musa mpaka Yesu ilikuwa ni miaka mingapi ?
Namaanisha hivi: hakuna mtu anaejua mtu wa kwanza kuumbwa aliitwa nani.
Ukweli hatahivyo, unabaki kuwa mtu aliumba.
Sasa ndio utuambie wewe umejuaje kama mtu wa kwanza sio Adamu ? Na utuambie chimbuko la mtu huyo ni nini ?

Huku mwisho naona umesema "Ukweli hata hivyo ,unabaki kuwa mtu aliumba". Hivi ndivyo ulikusudia kuandika au ulimaanisha "kuumbwa" ? Maana nina maswali pia kutokana na kauki yako hii.
 
Na tunfanye mwanadamu kwa mfano wetu (WETU)???!!??!) LAKIN ni kabla ya adam ajala tunda.
Mtu huyu anakusudiwa nani ?

Mlitakiwa muwe mnafundishwa lugha kama somo la msingi katika Elimu ya Dini.

Lugha huwa ina hukumu.
 
Huoni kama unajijibu?
Hapa wote tupo duniani na Mungu hajajifunua kwetu wazi wazi.
Sasa kitu ambacho hakijajifunua wazi unawezaje kujua umbo lake, hata kama kina umbile?
Kwanza nukta ya msingi hukutakiwa ukiri ya kuwa Mola ni Roho tu kisa hujawahi kumuona,ulitakiwa aidha ukae kimya au uulize ili upewe faida.

Mimi tangu mwanzo nilikwambia kabisa kwamba Mola ana umbile na umbile lake halifanani na kiumbe chochote,mathalani leo hii tunaambiwa ya kuwa "Birika" lina mkono lakini mkono wa Birika si sawa na mkono wako japokuwa nyote mna mikono.

Mwishoni umeuliza swali zuri sana,nina jua umbile la Mola wangu kutokana na yeye mwenyewe Mola wangu alivyojielezea na vile ambavyo ameelezewa na mtume wetu Muhammad amani ya Allah iwe juu yake bila kuongeza wala kupunguza.
 
Msingi wa hoja yetu ni sisi kufanana na Mola kama ulivyo nukuu andiko la "Tumfanye mtu kwa mfabo wetu".

Huku ulipoingilia ni pakutokea,namaanisha umekosea,wazazi ni watu ladhalika mimi ni mtu,lazima tufanane,ila Mola wetu sio mtu.

Naendelea ....
 
Simulizi la Adamu, ukisoma utaona Adamu anafanya kosa. Nasi tunaitwa Mwanadamu/Wanadamu - uzao wa Adamu. Maana yake ni kwamba kutoka kwa Adamu tumerithi kosa alilolifanya.

Ukisoma Historia inaonyesha ya kuwa Adamu aliomba msamaha na akasamehewa,na hakuna mja kubeba mzigo wa mwingine,hakuna kurithi katika dhambi,na Mola aliye juu anasema :

18. Na mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Na aliye topewa na mzigo wake akiomba uchukuliwe hautachukuliwa hata kidogo, na angamwomba jamaa yake. Hakika wewe unawaonya wale wanao mcha Mola wao Mlezi kwa ghaibu, na wanashika Sala. Na anaye jitakasa, basi anajitakasa kwa ajili ya nafsi yake. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu. ( Faatir : 18)

Pili,jalia kama kweli tumerithi,je ni kosa gani ambalo tumelirithi ni lile la kula tunda ? Lakini mbona Adamu aliomba msamaha na akasamehewa ? Na kwanini tulirithi kosa ambalo sisi hatukulifanya ?

Utakatifu na asili ya Mungu kwa Adamu iliharibiwa na Adamu. Nasi uzao wake tumerithi uharibifu wa Adamu.

Mwanadamu daima yupo katika hasara isipokuwa wale kuhusiana kuhusu subira na kufanya mema. Mola aliyajua yote haya na uhuru ulikuwa kwa Adamu na akili na tahadhari alipewa kama ilivyo kwetu,kwahiyo kukosea ni katika maumbile ndio maana kuna moto na kuna pepo,na mbora kati mwanadamu ni yule mwenye kukosea kisha akatubia.

Nakuuliz swali,nani alikwambia kwamba sisi tumerithi kosa alilotenda Adamu ? Je ni Yesu alisema maneno hayo au nani alisema maneno hayo ?
Ndugu yangu, watangulizi wako ni Adamu.
Kuhusu swali lako la kwanza. Nakusihi nenda google, andika "ugunduzi wa maandishi". Pia search kabla ya ugunduzi wa maandishi utapata majibu yako.
Kaka ushawahi kusoma Elimu ya uhakiki wa habari ?

Mimi kama habari hazina "Sanadi" yaani "Chain" ya wapokezi mpaka kwa wenye maandiko yenyewe habari hiyo huwa inakosa utahibiti na huwa naishusha daraja ya kuwa Kweli,mpaka iwe na chain iliyoshikana.

Vipi niangalie ugunduzi wa Maandishi wakati Adamu alifunzwa majina ya kila kitu ?
 
Maswali yako: la pili na tatu. Tafadhali jifunze elimu ya historia na sayansi ya historia ya mwanadamu.

Hapa ndipo nilipoona udhaifu wako ndio maana nikakuuliza maswali yale.

Misingi ya uandishi wa Historia katika upande wenu na upande wa secular una madhaifu sana na hili nimeliona mpaka kwako na umejaribu kutenganisha Historia na vitabu vya dini,jambo ambalo ni kosa kubwa.

Msingi mkuu wa Historia ni kurudi kwenye asili,lakini swali la msingi vipi utarudi kwenye asili ? Hapa lazima uwe na mtiririko ulioshikana wa mapokeo ya habari mpaka katika mizizi,pia unatakiwa uhakiki ukweli wa wapokezi na kujua tabia zao na kujua wakina walimu wao na kujua ukweli wao. Hili waandishi wa upando huo huwa hawalizingatii hilo,ndio maana historia zao huwa zinakuwa kama habari za kubuni.

Naongeza faida juu ya Historia na yote yanayo husu historia nitakapo kujibu post yako # 121.

Naendelea ....
 
Mashaka yangu ni kwamba, unatafsiri na kuelewa maandiko matakatifu: Biblia na Quran kama elimu ya historia. Kama unafikiri maandiko matakatifu ni historia unapotoka.

Hasemi maneno haya isipokuwa mtu ambaye hajui Historia ni nini na vitabu vya dini vina husu,vitabu vya dini hasa Injili,Torati,Zaburi na Qur'aan hivi vimejumuisha sheria,historia na kumpwekesha Mola mmoja muumna mbingu na ardhi na vyote vilivyomo.

Ndio maana vitabu hivi vikaitwa muongozo,kwanza vinatoa habari za watu walio pita na mambo yao waliyoyafanya ili kuwa funzo kwa umma husika na kuwaidhika,pili hutoa bishara juu ya mambo yajayo. Mathalani katika Qur'aan ina historia za watu wa kale na inatuoasha habari namna ulimwengu ulivyoumbwa hii yote ni Historia,ina sheria na mafundisho ya namna ya kumpwekesha Mola.

Kwahiyo kw ujumla wake vitabu vya dini muongozo na ndani yake kuna historia,sasa unapotaka kutenganisha viwili lazima utuambie kwanini ?
Ni makosa kuelewa moja kwa moja na wakati wote kwamba, Quran na Biblia ni elimu ya historia.
Hivi vitabu ni teolojia na siyo elimu ya historia. Kila simulizi katika Biblia au Quran linakusudia teolojia: Mungu na mwanadamu.
Yaani kwa ufupi ndani ya vitabu hivyo vina historia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…