Hakuna hata haja ya kufafanua time traveling bali afafanue time Kama time Kisha aonyeshe ni kivipi au ni katika namna gani inawezekana time traveling..?
Binafsi nachoona hili jambo ni mkanganyiko sana ktk namna ya kulielewa!, nadharia alizozielezea hapo sijui Kama zinawezekana!. Maana kwa namna alivyoelezea yaonyesha Kama muda ni vipande vya mkate! Yani hivyo ndo vinamatukio yalivyo so ni kama mkanda wa VHS yani ukiwa unaangalia muvi tukio lililopita hiyo ni past,tukio lililopo hiyo ni present na tukio lijalo hiyo ni future.
Tunapozungumzia time moja kwa moja tunaigusa space.. na space sidhani Kama inakitu cha namna hiyo cha kunakili matukio kana kwamba ukirudi nyuma au ukienda mbele utayakuta!! Sidhani hili Kama lipo..
Time traveling ambayo ni simpo na nayoielewa ni mfano wa barafu inavyoweza kugandisha kitu kisiharibike kwa wakati huu na hicho kitu unaweza kukitumia baadae!. I mean Kama utaweza kumuweka samaki ktk barafu na akakaa miaka 5 na wakati alitakiwa aharibike so kwa kuweza kumtunza akakaa miaka hiyo mitano bila kuharibika hiyo mi ndo naita time traveling!. So Kama kutapatikana teknolojia ya kuweza kumfreez binadamu then ukaja kumuamsha hata baada ya mwaka mmoja au mia akiwa vilevile basi hiyo ndo naita time traveling!.. hichi kitu naona kitakuja kuwezekana.
Time traveling kwa future naona ni concept inayowezekana ila ya past naomba hapo nikuambie tu sijui na hapa ndugu yangu chukua pop corn nakuwekea na haka ka burudani ujifurahishe..[emoji23]
View attachment 1973641
Watu wanachanganya concept za movie na zile za uhalisia!,time traveling bado haijaweza kudadavuliwa kwa 100%. Zaidi ni nadharia but practically mazingira bado ni magumu.. tukija kwenye nadharia za Albert Einstein Kuna vitu viwili vinaweza kuathiri muda navyo ni speed na gravity. Nakubaliana nae sasa ktk speed hii concept naielewa lkn mpk mtu kufikia hatua ya kupatikana ile effect ya time traveling na kuona kabisa huyu kafanya time traveling into the future ni aidha asafiri ama Kama spidi ya mwanga au karibu na spidi ya mwanga!! Mpaka Sasa hatujaweza kutengeneza kifaa cha namna hiyo ila hii concept ukiifatilia vizuri utaelewa ni kivipi spidi inaathiri muda so nenda kacheki utaelewa vizuri sana.
Gravity hii nayo inaathiri muda pia lakini hii pia mpk kuona moja kwa moja kuwa mtu huyu ame time traveling ni ngumu maana inahitajika gravity kubwa Sana ambayo inapatikana kwenye ma black holes huko.. nako ni mbali kinyama kufikia huko na aidha ukiingia unaweza usitokemo na ukiweza kutoka basi utakuta ni miaka mingi imepita huku duniani hivyo utakuwa ume time traveling into the future. Hapa nimeelezea kwa uchache sana ila fatilia time traveling ya kwenye vitabu vya fizikia achana na muvi utachanganyikiwa bure!
Nenda YouTube search Brian Greene huyu kazielezea hizo concept kiundani zaidi Kama ilivyodadavuliwa kisayansi kabisa na nguli wa fizikia Albert Einstein.