Timu ya Al Ahly wapitishia mizigo dirishani badala ya mlangoni

labda walikua wanawahi siti ka DCM za mbagala Je...
 
Na ndo tatizo la kuwaza uchawi, hata ukimtuma mwanao unga wakati anaingiza ndani ukamwagika kidogo mlangoni ukalala bila kuona asubuhi ukiamka unapata hofu kuwa wachawi wamekuja na kumwaga unga unga.
Hebu tupe sababu za kisayansi za kupitisha vitu dirishani wakati mlango upo
 
Hebu tupe sababu za kisayansi za kupitisha vitu dirishani wakati mlango upo


Sababu si lazima ziwe za kisayansi inawezekana ni sababu za kawaida au zikawa za kucheza na saikolojia tu.

Kama mimi nakuja kupigana na wewe na nina taarifa kuwa wewe unaamini katika ushirikina na safari hii umeuweka uchawi wako mlangoni moja ya mbinu nzuri ya kuua ujasiri wako ni kupitia dirishani huku wewe ukiona na nikipita tayari nimeshakupiga kisaikolojia.

Uchawi haufanyi kazi kwenye mpira. Ingekuwa unafanya kazi mazoezi ya nini? Usajili wa gharama wa nini? Si unatengeneza timu ya mateja ambao hawalipwi wanapewa wali nyama tu halafu unaloga.
 
Kila timu na mipango yake. Huwezi jua labda baada ya mechi na kesho wanapanga kuweka kambi yao hapa TZ wakiisubiria mechi na CRB? Simba wenyewe isingekuwa masuala ya gharama walitakiwa baada ya mechi ya Botswana waruke moja kwa moja huko Kaskazini kuwasubiria Wydad. Itawasaidia kuzoea hali ya hewa ambayo sasa hivi ni baridi na pia kujiandaa kwa utulivu zaidi.

Labda cha kushangaza ni kwa nini hao Al Ahly hawakuwa na maandalizi mazuri zaidi ya usafiri.
 


Ni rahisi kupitishia dirishani, mara zote ndo tunafanya hivyo tukiwa na watu wengi, haihusiani na chochote.
 
Naona umesahau Yanga kutumia mipango isiyo rasmi kuingia kwa Che Nkapa. Na bado umesahau Yale aliyoyafanya Jesus Moloko na wapuuzi wenzake siku ya derby ya Kariakoo. Al Ahly wameshajua janja njanja yenu.
 
Nawatakia Kila lakheri al ahyl Cairo
Wengine baya lolote liwapate
 
Kama wao hawa amini ushirikina hawakua na haja ya kufanya hizo mambo
 
Wapi tupichapicha🤔
 
Wakizichezesha hizo gari tutakata rufaa.
 
Utopolo walivoeneza propaganda za ahly kufanyiwa umafia hapa tz walifikiri itaishia kwa simba tuu
 
Kama wao hawa amini ushirikina hawakua na haja ya kufanya hizo mambo
Inawezekana ni Mind games ya kuwatoa mchezoni iwapo wana taarifa kuwa mpinzani anaamini katika uchawi na ameweka uchawi mlangoni.

Kama wewe ni mkristo halafu Ukaenda kwa mwarabu kuomba ushirikiano wa biashara halafu siku ya kukutana ukavaa kanzu haikufanyi wewe kuwa unauamini uislamu.
 
Kitendo cha kufanya mind games za kushirikisha kinaonyesha una imani hizo, utatofautishaje mind game na reality?
 
Ila timu yenu inapopita milango isiyo ya kawaida au wachezaji wenu kumwaga vitu usanjani mnaona kitu cha kawaida, subiri kipigo chenu kinakuja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…