Timu ya Azam inakwama wapi?

Timu ya Azam inakwama wapi?

King Jody

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2022
Posts
1,834
Reaction score
3,456
Azam ni timu inayomilikiwa na mmoja wa matajiri wakubwa Bongo, inamiliki uwanja wake,

Ina miundombinu yote ya kisasa inayohusiana na mpira wa miguu.

Cha kushangaza Azam haifanyi vizuri kitaifa na kimataifa, Kitu gani kinaikwamisha Azam?
 
Timu ikikosa mashabiki...

1. Wachezaji wanacheza kwa kurelax as long as wanalipwa.. hawana pressure.

2. Timu hata ifanye vibaya hakuna lawama kokote sio kama hizi simba na yanga ukifululiza game kadhaa matokeo mabaya utasikia mashabiki wanavyolalama huku mtaani
 
Ligi ya Tanzania ni ngumu sana ukifungwa game 3 huna ubingwa Azam hana uwezo wa kumudu safari ya kutafuta ubingwa
Simba na Yanga wao Kila mechi kwao ni final na wanataka ushindi ,nguvu maarifa fitina na maandalizi hufanana game one hadi Ile ya mwisho inayowapa kombe
Azam hata asajili vipi hawezi kumudu hiyo hali
 
1. Mpira wa 🇹🇿 una siasa kubwa sana, wenye mpira wao hawataki sio tu Azam, Timu nyengine yyt iwe Juu ya SSC na YNG! Yameshawakuta huko nyuma TUKUYU, MAJI MAJI, MSETO, MTIBWA... Ni vile tu Azam wapo strong ndo mana bado wanajipapatua!

2. Kwa 🇹🇿 Soka ni km dini, SSC & YNG zimewaingia wadau mpk kwenye blood vessels, kila Sector 🇹🇿 imegawanyika between the 2 sides! TFF, Marefa, Makocha, BUNGE, Mawaziri, Uhamiaji, Sisiemu to mention the few! (Rejea kisa cha KIBU Denis)


Kuna kisa kilitokea!

Timu KULWA alikuwa ana game na Azam pale CHAMAZI. Game Saa 10, Waganga na Makomandoo wakafika Chamazi saa 2 Asubuhi wanataka kuingia ndani! Walinzi wa Chamazi wakagoma!
Vuta n'kuvute ikaanza!

Tukio likaripotiwa Mamlaka husika! Hakuna hatua ikachukuliwa! Azam wakaimarisha ulinzi! Pakawa hapatoshi!
Ikawa vurumai. Hawa wanasema tunaingia! Wale wanasema hamuingii!

Kufika saa 8, "yule" Waziri - kama hamtaki hamieni Burundi - akapiga Simu kuamrisha watu Wale waachwe waingie wakafanye wanachotaka!

Ht kwenye Sakata Fei, nguvu kbw ilitumika kutoka "wenye nguvu" akiwemo huyo Bw... alipompigia simu ... dogo alimkataa... ulikuwa wapi siku zote wkt nanyanyaswa..

Ukienda Egypt, Soka Lao limemezwa na AL AHLY na ZAMALEK, Pyramid anahaha kama anavohaha Azam hapa! Serikali yao yote ni ima Al Ahly ama Zamalek!

wkt flani Kenya nao walikuwa kwenye mkwamo km huo... GOR MAHIA .... FC LEOPALDS...

The likes of Zambia...

Hitimisho: Azam wanaweza kuwa na Matatizo yao ya ndani, lkn yana athari ndogo kuliko athari wanazokumbana nazo za SIASA za Soka la Tanzania!
 
Azam hawako serious kwenye ligi. Angalia mechi za Azam dhidi ya Kariako's fc hakika inapigwa mbungi iliyochangamka na unafurahia kuwaona Azam fc.

Njoo Azam akiwa anacheza na hawa pangu pakavu tia mchuzi fc, Azam wanachocheza hakieleweki.


Pia njoo Azam akiwa anacheza kimataifa ni zaidi ya upuuzi, anafungwa hadi na timu za makapuku.

Kwa ufupi ili Azam ifanye vema, inapaswa walete benchi la ufundi lililotimia la nje likiongozwa na kocha anaye-demand uwajibikaji wa kiwango cha juu, yaani ukizingua anakuzingua, pia timu wamwachie kocha na watu wake wafanye kazi bila kuingiliwa na waswahili.
 
Timu haina presha,pili mamluki na wenye njaa wameja kibao kwenye uongozi wa Azam.

Simba na Yanga zina presha za viongozi,matajiri wanao zimiliki ,mashabiki so lazima wachezaji wakaze viuno.
 
Kamuulize JEMEDARI SAIDI KAZUMARI (MTIPA)

Yeye Alikuwa Manager WA Azam ilipokuwa inachukua UBINGWA, anajua siti zote na njia zote za kupita Ili uwe BINGWA.
 
Azam ni timu inayomilikiwa na mmoja wa matajiri wakubwa Bongo, inamiliki uwanja wake,

Ina miundombinu yote ya kisasa inayohusiana na mpira wa miguu.

Cha kushangaza Azam haifanyi vizuri kitaifa na kimataifa, Kitu gani kinaikwamisha Azam?
Hapo. 👉
 
Back
Top Bottom