1. Mpira wa 🇹🇿 una siasa kubwa sana, wenye mpira wao hawataki sio tu Azam, Timu nyengine yyt iwe Juu ya SSC na YNG! Yameshawakuta huko nyuma TUKUYU, MAJI MAJI, MSETO, MTIBWA... Ni vile tu Azam wapo strong ndo mana bado wanajipapatua!
2. Kwa 🇹🇿 Soka ni km dini, SSC & YNG zimewaingia wadau mpk kwenye blood vessels, kila Sector 🇹🇿 imegawanyika between the 2 sides! TFF, Marefa, Makocha, BUNGE, Mawaziri, Uhamiaji, Sisiemu to mention the few! (Rejea kisa cha KIBU Denis)
Kuna kisa kilitokea!
Timu KULWA alikuwa ana game na Azam pale CHAMAZI. Game Saa 10, Waganga na Makomandoo wakafika Chamazi saa 2 Asubuhi wanataka kuingia ndani! Walinzi wa Chamazi wakagoma!
Vuta n'kuvute ikaanza!
Tukio likaripotiwa Mamlaka husika! Hakuna hatua ikachukuliwa! Azam wakaimarisha ulinzi! Pakawa hapatoshi!
Ikawa vurumai. Hawa wanasema tunaingia! Wale wanasema hamuingii!
Kufika saa 8, "yule" Waziri - kama hamtaki hamieni Burundi - akapiga Simu kuamrisha watu Wale waachwe waingie wakafanye wanachotaka!
Ht kwenye Sakata Fei, nguvu kbw ilitumika kutoka "wenye nguvu" akiwemo huyo Bw... alipompigia simu ... dogo alimkataa... ulikuwa wapi siku zote wkt nanyanyaswa..
Ukienda Egypt, Soka Lao limemezwa na AL AHLY na ZAMALEK, Pyramid anahaha kama anavohaha Azam hapa! Serikali yao yote ni ima Al Ahly ama Zamalek!
wkt flani Kenya nao walikuwa kwenye mkwamo km huo... GOR MAHIA .... FC LEOPALDS...
The likes of Zambia...
Hitimisho: Azam wanaweza kuwa na Matatizo yao ya ndani, lkn yana athari ndogo kuliko athari wanazokumbana nazo za SIASA za Soka la Tanzania!