Haruna na Kotei wameshaaga. Kila nikikumbuka viongozi walivyomtimua Hamisi Tambwe kimizengwe na kutuaminisha kuwa wameleta mtambo wa mabao Nserekuma sina hamu kabisa. Msimu mzima sijui hata alifunga goli ngapi kwenye ligi. Naona kama picha la kihindi linarudi tena. Hivi ilikuwa haiwezekani kuwaondoa tu Juuko, Kwasi na Zana au hata Gyan halafu tukaongeza hao wabrazili wao watatu/wanne kwa mwaka huu. Tukiona wamefanya vizuri ndio ndio wasajiliwe kwa wingi mwakani?
Yaani dunia wakati mwingine haiko sawa kabisa, kwa upande wangu nilitegemea mchezaji wa kwanza kufukuzwa Msimbazi ni Zana Coulibaly (mchezaji wa kocha). Lakini mpaka leo kimya au kashafukuzwa kimya kimya. Ngoja tusubiri tunaweza kuona maajabu ya mwaka ya Kotei na Haruna kunyimwa mkataba na Zana kuendelea kupeta Simba.
Anyway ngoja niweke akiba ya maneno pale hawa wabrazili watakapofanya vizuri angalau niwe na la kusema. Ila kwa sasa bado naamini walau Kotei alitakiwa apewe mkataba hata wa mwaka mmoja kwa ajili mpito.