Timu ya madaktari wa China nchini visiwani Zanzibar yaleta mwanga wa matumaini kwa mama wa miaka 70

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121


Akiwa na umri wa miaka 70, Tuma Saidi Hamadi kutoka kisiwa cha Pemba, Zanzibar alikuwa katika hatihati ya kupata upofu, lakini maisha yake yalibadilika ghafla baada ya kikundi cha 34 cha timu ya madaktari wa China kumfanyia upasuaji wa mtoto wa jicho na kurejesha uwezo wake wa kuona.

Safari ya Hamadi ya kurejesha uwezo wake wa kuona tena ilikuwa na changamoto. Kaka yake Yusuph, daktari wa ganzi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Kisiwani Unguja, amekuwa msaada wake usioyumba.

"Kwa muda mrefu, macho yake yalikuwa hayawezi kuona vizuri, ambapo aliweza kuona vivuli tu visivyo wazi mbele yake. Ilifanya maisha yake kuwa magumu sana na ilikuwa ndio chanzo cha wasiwasi mkubwa kwa familia yetu," alisema. Akiwa amedhamiria kumsaidia dada yake, Yusuph alimpeleka kwa timu ya madaktari wa China waliokuwa hospitalini hapo.

Baada ya uchunguzi wa kina, Zhou Shi, daktari wa macho katika Hospitali ya Umma ya Huai'an katika Mkoa wa Jiangsu mashariki mwa China, aligundua kuwa Bi. Tuma ana mtoto wa jicho kwenye macho yake yote mawili. Zhou alitoa indhari kuwa upasuaji huo utakuwa na changamoto na matokeo yake hayana uhakika kutokana na hali yake kuwa mbaya sana. Licha ya hatari, Yusuph aliiamini timu ya matibabu ya China na akaomba dada yake afanyiwe matibabu.

"NAWEZA KUONA SASA!"

Upasuaji huo ulifanywa kwa uangalifu wa kina na Zhou na timu yake. Kila hatua ilikuwa sahihi na iliyopangwa kwa uangalifu, ikijaza matumaini ya Bi. Tuma kupona. Kesho yake, Zhou aliondoa bendeji kwenye macho ya Hamadi taratibu wakati alipokuwa akitembelea wodini.

Uso wa Hamadi ulichanua kwa furaha huku akishangaa.

"Naona sasa!" Maneno yake yalimfanya kaka yake atokwe na machozi ya furaha, ambaye wakati huo alikuwa ameshikilia mkono wa daktari Zhou kwa nguvu huku akimshukuru kwa Kichina cha kuombea maji lakini cha kugusa moyo: "Asante, asante."

Wakati huu ulikuwa ni taswira ya kina ya uhusiano kati ya daktari na mgonjwa pamoja na urafiki wa kuvuka mpaka ambao umekuwepo kati ya China na Zanzibar.

MATUMAINI NA AFYA KWA WOTE

Hadithi ya Hamadi ni mojawapo ya hadithi nyingi zilizotokana na uwepo wa timu ya madaktari wa China.

Wagonjwa wengi Zanzibar hukosa fursa muhimu za matibabu kutokana na uhaba wa rasilimali na teknolojia iliyopitwa na wakati. Madaktari wa China wameleta ujuzi wa hali ya juu wa matibabu na kutoa vifaa vya upasuaji na dawa, na hivyo kuwezesha wagonjwa wengi kupata matibabu yanayobadilisha maisha yao.

Timu ya matibabu ya China imetekeleza mfano "mdogo na mzuri" wa matibabu kwa kuzingatia ugonjwa wa mtoto wa jicho, ugonjwa ambao umeenea ingawa unaweza kutibiwa. Mbinu yao inachanganya dawa sahihi na mafunzo ya kiufundi ili kuleta afya bora zaidi kwa gharama ya chini na ufanisi wa juu.

KUJENGA UWEZO NA KUFUNGUA UKURASA MPYA

Mchango wa timu ya matibabu ya China umeenea na kuonekana kwenye zaidi ya upasuaji. Hivi karibuni, walifanya upasuaji wa kwanza Zanzibar wa saratani ya mirija ya nyongo ambao ulikuwa mgumu sana, pamoja na taratibu nyingine za msingi kama vile kuondoa vitu visivyo kawaida kwenye mwili kwa watoto na upasuaji wa ini na figo.

Wakati wa upasuaji huu, Madaktari wa China waliwaelezea wenzao wa eneo hilo mbinu za kina, ili kukuza ustadi na uhamishaji wa maarifa. Imani waliyonayo madaktari wenyeji na wagonjwa kwa timu ya matibabu ya China inatilia mkazo matokeo ya kazi yao.

Daktari mmoja aitwaye Rashid alisema baada ya kushuhudia upasuaji tata, anatumai kuja China kujifunza mbinu za juu zaidi za matibabu."

Kuanzia kurejesha uwezo wa kuona hadi kufanya upasuaji wa kuokoa maisha, timu ya 34 ya madaktari wa China sio tu imeleta huduma ya afya ya hali ya juu Zanzibar bali pia imeimarisha uhusiano wa urafiki na ushirikiano kati ya China na Tanzania. Kupitia kujitolea na utaalamu wao, wanaendelea kuleta matumaini na mustakabali mwema kwa maisha ya watu wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…