Timu ya Tanganyika, Gossage Cup 1961

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
TIMU YA TANGANYIKA GOSSAGE CUP 1961

Majina ya wachezaji wote na maelezo ya ziada kayatoa John Limo baada ya kumfikishia hii picha.

Tumshukuru kwa kutufanyia hisani hii:

Kutoka kushoto: Henrick Martin, Hemed Seif, John Lyimo, Washokera, Yusuf Mwamba, Yahaya Mbike, mbele ni Aziz Abdullah, nyuma Ayubu Mohamed, Mohamed Mzee, Juma Mrisho, Maulid Abedi, Mattias na Miraji Salum.

Zaidi ingia:https: //www.mohamedsaidsalum.com/kalamu-ya-mwandishi/timu-ya-tanganyika-gossage-cup-1961
 
Huyu matthias ndio yule baki kisiki kutoka mkoa wa tabora au yupi? maana safu yao ya ulinzi alikuwa matthias na juma mrisho ndio ulikuwa mkoba ila sijamuona mshambuliaji machachari yunge mwanansali hapo.
 
Mzee juma mrisho yako katika mashindano ya Gossage nadhani ulikuwa Uganda akapata simu kuwa huku Tanzania mkewe kajifungua mtoto wa kiume akaambiwa atoe jina akasema aitwe gossage kisha akakata simu. Nae baadae alikuja cheza mpira kwa kiwango chake.
 
Picha namba 3, mbona namuona Mzee Karume akiwasalimia hapo?

Enzi hizo za 1961 bado Zanzibar na Tanganyika zilikuwa nchi mbili tafauti.
 
Picha namba 3, mbona namuona Mzee Karume akiwasalimia hapo?

Enzi hizo za 1961 bado Zanzibar na Tanganyika zilikuwa nchi mbili tafauti.
Unajua siku mapinduzi yanatokea Zanzibar huyo mzee alikua wapi? Hu muungano ulikuwepo hata kabla sahihi hazijawekwa
 
Picha namba 3, mbona namuona Mzee Karume akiwasalimia hapo?

Enzi hizo za 1961 bado Zanzibar na Tanganyika zilikuwa nchi mbili tafauti.
Biti...
Picha nilizoweka ni za nyakati tofauti.
 
Unajua siku mapinduzi yanatokea Zanzibar huyo mzee alikua wapi? Hu muungano ulikuwepo hata kabla sahihi hazijawekwa
Najua sana kama alikuwepo Tanganyika kwa kuogopa asikamatwe pindi lile jaribio kama halikufanikiwa. Yeye na Babu walikuwa Dar, Babu alikuwa akitafutwa na utawala mpya wa mwezi mmoja.
 
Najua sana kama alikuwepo Tanganyika kwa kuogopa asikamatwe pindi lile jaribio kama halikufanikiwa. Yeye na Babu walikuwa Dar, Babu alikuwa akitafutwa na utawala mpya wa mwezi mmoja.
Hiyo picha ni baada ya Jan 1964.
 
Najua sana kama alikuwepo Tanganyika kwa kuogopa asikamatwe pindi lile jaribio kama halikufanikiwa. Yeye na Babu walikuwa Dar, Babu alikuwa akitafutwa na utawala mpya wa mwezi mmoja.
So hu muungano ni kama wana ndoa ambao walikua wanafanya mambo yote ya ndoa kabla ya kurasimishwa either kanisani, msikitini au kwa mkuu wa wilaya, in other words ile ya tarehe 26-04-1964 ndio ndoa ili rasimishwa but ukweli tayari tulikua tumeungana siku nyingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…