Timu ya Ushauri kwa Diamond haiwajibiki vema

Ukiwa na hela unakosa uhakika kabisa kwamba mtu kakufata wewe au pesa.

Kama mwanamume namuelewa mond sana,na alianzaga kuyasema haya toka hazijachanganya kipindi yuko na wema.

Kwa sasa hata wanawake wote wakisema wanampenda,haitazidi jinsi anavyopendwa na mama yake aliyempenda tokea akiwa si lolote si chochote kwa wengine,tena hata wanaye hakutakiwa awataje ila mama yake tu.
 
Kuhusu mama yake we acha tuu, kuna ya sirini mengi mno ambayo zuchu ameamua kuyavumilia
 
Sisi timu wasafi tunamkubali hivyo hivyo, aendelee kutupia zaidi
 
Ninahisi Diamond ameanza kuufanyia kazi ushauri wangu kuhusu Majukumu ya Mama yake Mzazi. Juzi nimeona clips zinamuonyesha Mama anacheza na Mjukuu wake kutoka Kenya. Pia nimeona muonekano wa Mama alionekana hakika ni Mama na Bibi ( very decent). Sina maana kuwa Mama dangote akae tu nyumbani, hapana, ninachomaanisha ahusike kwenye mambo yatakayo reflec Umama wake na Ubibi wake. Hata anapokwenda kwenye shughuli za Muziki wa Mwanae basi wampe heshima yake kama Mama na sio kumchezesha sawa na ZUCHU au KAJALA. Pia apunguze kuonekana sana kwenye shughuli za Muziki za Mwanae, Ifike siku akihudhuria basi iwe ni headlines kwenye vyombo vya habari kuwa Mama alikuwepo kwenye tamasha hilo .

KIJANA WANGU DIAMOND BIG UP SANA
 
Japo maisha siyo kutesa kila siku, ila pesa ndiyo kila kitu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…