Timu yangu ya Simba fanyeni harambee tukomboe nyasi bandia bandarini

Timu yangu ya Simba fanyeni harambee tukomboe nyasi bandia bandarini

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Wasalaam wanabodi,
Mimi kama Mwanachama mtiifu wa club ya Simba SC, naishauri club yangu pamoja na harakati za kunyakua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara, Uongozi uitishe harambee ya kuzikomboa hizo nyasi Bandarini.

Pamoja na ukweli kwamba club nyingi za soka zipo hoi kiuchumi lakini tukumbuke club ina mtaji wa mashabiki ambao wapo tayari kujitoa kwa hali na mali kuona timu inasonga mbele.

Tukiziacha nyasi hizi zikapigwa mnada tutakuwa tumepiga hatua moja kurudi nyuma na ndoto za Kumiliki Simba SC Complex zitakuwa zimefifia.

Naamini club ya Simba inaongozwa na watu wabunifu, wazoefu na wenye ueledi wa kutosha kuweza kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kama hizi. Kuandaa harambee itakuwa rahisi zaidi kuliko club kujitutumua kulipa deni wenyewe.

Ni matumaini yangu mtaufanyia kazi ushauri huu.

Simba Nguvu Moja
 
Samata ameshawalipia, japo ni aibu kwa klabu yenye wanachama na mashabiki lukuki nchini na nje za nchi....
 
samatta amekanusha kuwalipia ,deni lipo tujipange wana simba ,
 
Nawapongeza Simba kwa harakati za ujenzi wa uwanja wa kisasa.

Pili nawatakia kila heri ktk mchakato wa kulipia kodi ili kuzikomboa.
 
Nawapongeza Simba kwa harakati za ujenzi wa uwanja wa kisasa.

Pili nawatakia kila heri ktk mchakato wa kulipia kodi ili kuzikomboa.

ni shs ngapi?, account ya simba iko benki gani? wanashndwa nini kuchukua mkopo?
 
Back
Top Bottom